Foleni chanzo Cha msongo wa mawazo katika barabara za Jiji la Dar Es Salaam

Foleni chanzo Cha msongo wa mawazo katika barabara za Jiji la Dar Es Salaam

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Imeelezwa kuwa tatizo sugu la foleni katika barabara za jiji la Dar es Salaam linaweza kuongeza msongo wa mawazo kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri, kuchochea uchovu kwa madereva na abiria na hatimaye kuongeza uwezekano wa ajali na vifo barabarani.

Hayo yamebainika katika wiki ambayo jiji hilo limekumbwa na misongamano mikubwa kwenye barabara kuu mbalimbali, hali inayosababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi.

Moja ya barabara inayosababisha foleni ni Mandela Road ambayo foleni yake husababishwa na malori yanayotoka nchi za nje kuingia tanzania na mengi kuharibika na kusababisha foleni.

Wakuu
Barabara zinachimbwa sana mpaka zinatengeneza mitaro ambayo hata Kwa wapita njia sio salama, kama wanashindwa kufanya kazi Kwa wakati huu unaweza kuwa wimbo wa Kila siku tuchangamkee kipindi hiki Cha uchaguzi atoke nani? Aingie nani? Ambaye anaweza kulimaliza suala la foleni katika Jiji la Dar Es Salaam.
 
Back
Top Bottom