Wasalaam ndugu zangu wote huku JF,
- Nimekuwa nikipata sana ujumbe wa private wakuniulizia nilipo, ninasema hivi nipo isipokuwa majukumu ya maisha yamenizidi mno, nafasi yangu imekuwa ndogo sana hata kushindwa kuwepo hapa in full kama ilivyokuwa kawaida huko nyuma.
- Otherwise, ninaiminia sana JF, kwamba siku zote ina wananchi wengi na hasa wapya pia, wenye nia na madhumuni yale yale yetu wote ya kumkoma nyani na kulisaidia taifa letu kiushauri, ili lijivute japo mbele kidogo. Sina uhakika itanichukua muda gani kumaliza projects mbali mbali nilizojiingiza nazo kwa sasa, ambazo zinanifunga sana kimuda, lakini ni muhimu sana nizifanye sasa kwa manufaa yangu ya baadaye, ili niweze kulifikia lengo langu la kulisaidia taifa letu kwa ufanisi zaidi.
Nawatakia wana-JF, wote kazi njema na majadiliano mema na yenye faida kwa masilahi kwa taifa letu changa.
Respect and Later!
Field Marshall Es, ni Wazee wa Sauti Ya Umeme!