Flyover Tazara yavuka nusu

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,716
Reaction score
9,051
MRADI wa ujenzi wa barabara ya juu (flyover) katika eneo la Tazara jijini Dar es Salaam umefikia asilimia 58 na unatarajiwa kukamilika Oktoba mwakani.


Flyover Tazara​

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anayeshughulikia ujenzi, Elias Kwandikwa, aliyasema hayo juzi wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa mradi huo.

Kwandikwa alisema serikali inaridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo unaojengwa na kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction Co Ltd.

"Kasi ni nzuri na wanavyoonekana watamaliza kabla ya wakati kwa sababu mwezi wa nne (Aprili) ulikuwa umefikia asilimia 25, mwezi wa saba ulikuwa asilimia 45 na sasa mwezi wa 10 umefikia asilimia 58, wanakwenda vizuri," alisema Kwandikwa.

Alisema mradi huo pindi utakapokamilika utakuwa na umuhimu kwa maendeleo ya nchi kwa sababu wakazi watakuwa wanawahi kufika katika shughuli zao.

"Mradi huu ni muhimu sana, ni kichocheo cha maendeleo, mtu akichelewa kazini kutokana na foleni maana yake atalipwa mshahara hewa, pia akichelewa kwenda sehemu za uzalishaji tija itapungua, sasa 'flyover' ikikamilika wananchi watawahi sehemu za kuzalisha," alisema Kwandikwa.

Rais John Magufuli wakati akiweka jiwe la msingi kuzindua ujenzi wa mradi huo Aprili 16, mwaka jana, alisema gharama za mradi huo ni Sh. bilioni 100 na kati ya fedha hizo Sh. bilioni 93.44 zitatolewa na serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Kimataifa la Maendeleo la (Jica) huku Sh. bilioni 8.3 zikitolewa na serikali ya Tanzania.

Alisema barabara ya juu itakayojengwa itakuwa na njia nne na urefu wa mita 300 kutoka maeneo ya katikati ya jiji la Dar es Salaam kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na itapunguza kero na msongamano wa magari yaendayo na yatokayo JNIA na Bandari ya Dar es Salaam.
 
Hebu weka picha halisi basi ya kinachoendelea pale Tazara ,hiyo uliyoweka ni itakapokamilika
 
Siku itakapozinduliwa watu watajisifia mpaka basi
 
Aisee,,,ubungo interchange WB kafadhili,tazara flyover JICA kafadhili,,,treni mkopo toka Turkey na Credit Suisse,,,pesa zetu na za pension funds zinakwenda wapi?

Kunenepesha kibindankoi ya bashite
 
Ebu jamani tutofautishe flyover na interchange, flyover Ina maana kuna barabara ya juu ambayo inaenda umbali wa kutosha Mf kama Tazara inakuwa flyover Ile barabara ya juu inakuwa na urefu labda wa kutokea Ubungo au Kariakoo otherwise hii ni Interchange!
 
Hivi ile ya kutoka bandarini kwenda Ubungo inabaki hivyo hivyo? Kama ni hivyo ule ugonjwa wa kufikiri madogo (thinking small) bado unatuandama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…