Flight 370

Simplicity.

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2013
Posts
2,636
Reaction score
1,664
Ama kweli kila janga lina wanaofaidi! Asubuhi hii nimekaa restaurant moja maeneo ya Knyama napata bfast, karibu yangu kakaa dada mmoja peke yake, sasa kuna jamaa kaja from no where naye kakaa karibu na sisi, amebeba mabegi kama mtalii fulani hivi halafu kavaa kizibao kama vile vya majembe na ubuti mrefuuu! Muda si muda jamaa kaanzisha story huku akiwa ameteka attention ya dada kwamba yeye muda si mrefu katua airport kutoka USA akiwa ametokea Australia, alikuwa kwenye ile timu ya kutafuta Flight 370.

Alivyotaja ile ndege nikashtuka nikadhani anataka kutuambia imepatikana labda! Ana story kibao kueleza jinsi operation ilivyoenda, dada wa watu anasikiliza kwa makini, mie niko busy na bfast lakini alikuwa akiongea kitu chenye ukweli au point kuhusu hiyo flight natikisa kichwa kuonyesha namsupport, so jamaa kakolea kaongea mavitu full chaka, nikasema dada wa watu kama hajui chochote kuhusu hii ndege, mkenge leo atauvaa, maana alivyoendelea na story nikagundua nia yake ni kumkamata yule dada. Karibu niburst na kicheko, nikaamua kusepa. Dah, wabongo wapo vizuri kwenye fix hata za mapenzi!


Anyway, nimepitia tu kuwasalimia.
 
siku nyingine usichanganye viroba wakati wa breakfast
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…