‘Fixed’?

Well, ngoja nami nichangie huu uzi baada ya muda mrefu kwa kutumia established facts na sio conspiracy theories .

Mosi , mimi nilifahamu kuhusu ugonjwa wa Magufuli mara ya kwanza kabisa October 2019 ambapo Kigogo alisema Magufuli baada ya kupatwa na ule moshi usioeleweka akiwa ziarani Ruangwa kuwa amepata shida na yuko kwenye coma na kukimbizwa Ujerumani .

Zitto Kabwe siku hiyo hiyo baada ya tukio la moshi kuhusishwa na coma na safaeu ya Ujerumani alipost picha ya Samia kupita kwenye red carpet pekeyake na kuandika ujumbe huo hiyo ilikuwa ni October 18/2019 ,akiwa na maana sasa nchi itakuwa chini ya Samia masaa machache yajayo akiwa kama rais.



Okay nikirejelea tukio la moshi Ruangwa lilitokea tarehe 15 October 2019.


View: https://youtu.be/sJ9sDOJkh6E?si=Pig6UzRhnMRptnWf
Magufuli aliibuka ghafla siku chache na kuapisha watu huku serikali haikutoa tamko kuhusu habari hizo za uvumi kuhusu ugonjwa wake hii ilikuwa ni 20/October 2019, Ikulu ulipigwa wimbo fulani wa dini wenye ujumbe fulani sijui kama ilikuwa ni kawaida kiprotokali au kuna ujumbe ulikuwa unatumwa[wataalam wa protokali mtusaidie wimbo wa dini kupigwa ikulu ilikuwaje]


View: https://youtu.be/QUkv-1Jq8CA?si=NUggH_moIH8OYxHa
Ok vita ile iliendelea mitandaoni hadi wakati wa kampeni 2020 hapa niliona mimi kwa upande wangu kuna tatizo kwanza.

Magufuli hakuwa na uwezo wa kupiga kampeni mfululilizo kwani alipiga kampeni leo mapumziko siku 5-8 hii haikuwa kawaida hasa kama ilivyokuwa 2015 kulinganisha na mshindani wake Lissu aliyekuwa katoka kwenye matibabu na bado alikuwa imara kupiga kampeni hadi alipofungiwa kihuni na Mahera, haya mapumziko marefu yalitoa picha hakuwa sawa na kuna kitu hakikuwa kawaida bali walificha tatizo.

Pili uwepo na "feni kubwa" [air cooling system] eneo la wazi tu asimamapo au akaapo Magufuli na bado Kigogo akaendelea kuzungumzia feni ile kubwa aliyokuwa akizunguka nayo Magufuli kwenye kampeni, nilijenga maswali inakuwaje katika umati ule na eneo kubwa la wazi kutumia feni ile ilhali mzunguko wa hewa upo wa kutosha?


View: https://x.com/kigogo2014/status/1371701886403887108?t=6Y0lDlYil5WNqoq1qYRpVQ&s=19
Mazishi ya John Kijazi hapa binafsi baada ya kuiona ile picha ya Magufuli niliona sasa hayuko sawa ni kama mtu aliyepata reaction kutokana na matumizi ya antihypertensive na strong diuretics hii ilikuwa ni February 19, 2021.


Ukiangalia kwa mbali kule ile feni ipo bado.

February 27 , Siku ya uapisho wa Bashiru Ally kuwa katibu mkuu kiongozi hii ikawa ndio siku ya mwisho Magufuli kuonekana hadharani na baada ya uapisho hakuongea sana kama ilivyo kawaida yake na hata ule mkutano wa SADC uliotakiwa kufanyika kwa njia ya mtandao siku chache mbele hakushiriki.


View: https://www.youtube.com/live/pZhq-BSS3F0?feature=shared
Baada ya hapo ndio ukaanza ule uvumia mkuu juu ya alipo na ni mzima au mgonjwa.

Akaja mkanushaji wa kwanza alikuwa Kassim Majaliwa akasema Magufuli ni mzima na anachapa kazi hii ilikuwa ni March 12, 2021


View: https://youtu.be/nRTBFINdMn8?si=3x_pgSTL5JSlL4jA
Jioni hiyo hiyo March 12 , 2021 Evarist Chahali akasema Magufuli amefariki akiwa Mzena


View: https://x.com/Chahali/status/1370473711715909638?t=3VAByRqdQ2rN5YdsaTXbIg&s=19
Jioni hiyo hiyo aliyekuwa mkurugenzi wa usalama wa taifa na balozi Namibia , Modestus Kipilimba alikanusha kuwa rais haumwi[Swali langu je serikali haikuwa na msemaji hadi huyu mtu aliyepo nje ya Tanzania atolee maelezo]?


View: https://youtu.be/0MRr9m2QYZo?si=Uj4UdWjpp1GgsrCd
Siku hiyo hiyo Chalamila naye alidai amempigia Magufuli simu asubuhi na ni mzima pia .

Media za Kenya zikaanza kushangaa za Tanzania ziko vipi kimya juu ya kifungu cha katiba juu ya kutoonekana kwa rais ofisini na sababu zake na kipi kifanyike?

Na taarifa zilidai Magufuli kalazwa hospitali mojawapo Kenya kwa tatizo la upumuaji.

Hadi hapo hakuna aliyekuwa na majibu ya kuridhisha watanzania .

Tarehe 15 March 2021 , Samia akiwa ziarani Tanga akahimiza watu washikamane na kudai kukaguliwa ni kawaida hata ukiwa na mafua hata uso wake katika kuongea ulionyesha kuna kitu hakipo sawa.


View: https://youtu.be/0MRr9m2QYZo?si=Uj4UdWjpp1GgsrCd

Tarehe 17 March, 2021 akiwa anatangaza kifo cha Magufuli akasema , Magufuli alilazwa tangu tarehe 6 March , 2021 ila hakutaja sababu ya kulazwa bali sababu ya kifo.


View: https://youtu.be/PMV4GiybKY4?si=CDHm8fvz4vhMK8PA
Je huu ukimya na maswali nani alitakiwa kuyajibu maana katika taaluma ya utabibu chanzo/sababu ya kifo huwa ni jambo la msingi sana je siku 2 nyuma kabla kwanini hakuzungumza hayo nini kilikuwa kinaendelea ?

Siku ya mazishi ya Magufuli ex-CDF Mabeyo alisema ana dokezo ila hawezi kulisema palepale bali anaomba amuone Samia ofisini


View: https://youtu.be/Nz2Ma3BFtcM?si=7GOYVLlzbNcHB9KH
Kikwete aliacha maswali mengi kwenye mazishi hasa aliposema habari ya kifo cha Magufuli alikuwa akifuatilia mitandaoni tu na alipopigiwa simu alidhani ni bwana yule[ Kigogo 2014] je hii inaleta mantiki rais mstaafu kufuatilia taarifa kutoka kwenye account ile ambayo tulikuwa tunafuatilia ambao hatukuwa na uwezo wa kuyajua ya serikalini?


View: https://youtu.be/gXzTvfJX0lo?si=dn4UY0k_hXbIaWgA
Hadi hapo nimejitahidi kuunganisha mnyororo wa matukio juu ya afya ya Magufuli kwa musa wa miaka 2 .

March 2024 Mabeyo akiwa anafanya mahojiano alidai Magufuli alisema amrudishe akafie nyumbani je nyumbani wapi alimaanisha [nyumbani ikulu Magogoni au Chato]

Je ni nyumbani Tanzania sababu hakuwepo Tanzania kama tulivyoambiwa alienda kwanza Kenya baadae India?

Mimi ninafahamu baraza la usalama wa taifa haliwezi "kugrant" kushindwa kumlinda rais hadi likubali arudi na kujifia nyumbani [hapa napo yapo maswali mengi ya kujibiwa mbeleni pia]


View: https://youtu.be/J5EQ0vknTMI?si=TPkmy-2fnABm1ZsC
Baada ya Magufuli kufariki ndio kile kipande cha gazeti kilitolewa cha mwaka 1992 ikipitishwa mchango wa matibabu ya ugonjwa wa moyo ,hiki kipande cha gazeti hakikuwahi kuonekana kabla hadi tarehe 17 March , 2021 ndio kilionekana je kilitunzwa kwa makusudi maalum au kilitafutwa kwa makusudi maalum?

Nikirejea comment yangu mwanzoni kwenye huu uzi March 13 mleta mada alinijibu kuwa je haiwezekani watu kujua udhaifu wako ulipo na ndio wakaamua wapitie hapo hapo?

Huu ni uchambuzi wangu niwakaribishe na wengine kama watakuwa na nyongeza.

Hadi hapo mtagundua kuna mengi baada ya hapa na tukisema uchunguzi uanze kufanyika hakika patarindima na mtabaki midomo wazi.

Kigogo alijuaje mapema kuwa Magufuli alikua na shida ya atria fibrillation?

Mimi nawaacha na kibwagizo kimoja tu je yale mabaya yaliyofanyika enzi za Magufuli mbona bado yapo tu sana je ukosoaji waliokuwa nao Zitto Kabwe na Fatma Karume enzi zile mbona umepoa je kuna nini?

Cc Richard
 
Hoja yako inafikirisha sana.
 
Hapo kwenye Nah weka la
 
Hapa umemaliza kila kitu na Zitto anahusika kabisa
 
A Perfect crime, a who done it, cat out of the bag, or a consipiracy ?????
 
Hmm…..very very interesting….
 
Uzi wameubagaza kuanzia tarehe 17/03/2021 wakaja achia komenti za tarehe 21 kwa tunaouona leo hili jukwaa limetukosea kuondoa baadhi ya michango hiyo... Hivyo basi jukwaa hili ni remote kuna watu wanaamua tusome nini na tuchangie nini.
 
Huyu BAK atakuwa Naye kafa zamani sanaa
 
Vile vifo vya watu waliomzunguga JPM kabla ya yeye mwenyewe vilikuwa jambo la ajabu kweli.
Mungu wangu. Na mimi nahisi wale walitangulizwa. Sijui ndugu zao na watoto wao wanajisikiaje sasa. Kama Mahiga jamani!!! Nahisi ndio alichopitia Mpango, na ndio maana hataki tena kusikia haya mambo. Ila wahusika wajue kuwa haya mambo hayaendi bure. Malipo ni hapa hapa duniani. RIP Magufuli, Mwenyezi Mungu atalipa haya yote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…