Fix mashuhuri za kinadada

Fix mashuhuri za kinadada

The Tomorrow People

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2013
Posts
2,689
Reaction score
2,859
Haya ni baadhi ya maneno wakina dada hutumia sana kudanganya au kujikweza;

1. Una kitu rohoni halafu unajibu niko poa tu usijali. Huku umenuna balaa pengine hata usoni humtazamani unamkomoa nani sasa? Halafu ukikutana na mwanaume kauzu anakujibu okay basi weee unatamani ungesema la moyoni fasta hahahahaaa!

2. Nipe dakika 5 tu wakati unajua utachukua nusu saa nzima! Kwani ukimwambia nipe dakika 30 atakufa, matokeo yake ukitoka uko unakumbana na malalamiko kibao au ushampotezea mtu mood ya mtoko!

3. Usinitumie meseji tena! Hahahahaaaa anakujibu poa au anakaa kimya halafu dakika

5 nyingi unajikuta umemtext wewe mwenyewe! Au anakujibu sawa Dadeki ghafla unatamani usingetamka ulichotamka! Kama huimaanishi usiitamke unaweza jiona bure ujue! labda tu kama una mwanaume anayejua kudekeza kama huyu wangu LOL!! 4. Nipe muda nifikirie halafu wakati jibu tayari unalo! Fanya hivi kama una mpango na huyo mtu kama huna mpango naye mwambie tu hapo hapo kuwa eeh bwana ee hii kitu hapana! Usimpe mtu matumaini hewa bwana! 5. Sina hisia naye kabisa, Ananitaka mi simtaki au sisi marafiki tu! Halafu huyo huyo usiye na hisia naye anamuibukia rafiki yako au mtu wako wa karibu unaanza kununa au roho kuumia! Huwa unaumia nini kama huna hisia naye na nyie ni marafiki tu! Roho mbaya zinaanzaga hivi!!

6. Ex wangu hayupo mawazoni kabisaaaa huku unamstalk kimya kimya, habari zake zote unazo, kila analofanya unajua, tunadanganya watu ila mioyoni tunajua ex huyo bado yuko mawazoni vinginevyo hata mahali alipo usingejua! Heheheee ni kawaida tu ex mmoja kurudi rudi kichwani ila dhambi ujue hahahahaaaa!

7. Siko afteryour money mimi hahahahahaaaa the biggest lie of all times! Pesa hii hii iliyomsaliti Yesu wewe uione haina thamani wakati maisha yenyewe haya haya na kipato ndio hiko hiko weweeee!! labda utamke haya kwa mwanaume asiye na kitu kabisa hapo sawa! ila mtu ana feZa zake za maana ujifanye hujawahi kuziwazia mmmmmmh Dada muogope Mungu jamani anakuona ujue hahahahahaaaaa!! Ila labda!!

8. Mimi huwa sili sana. Khaaaaa! Team somefood mnajijua, yaani kwenye kidate cha kwanza unajinywesha mimaji maji sijui nini na nini huku tumbo linanguruma mpaka unakumbuka viporo vyako home kula mama kula tu! Tangu mwanzo ajue mwenzangu ana appetite ya maana ila ule kwa kiasi sio ujifanye wewe sio mlaji. Kama ni chispi agiza chipsi zako kula futa zooote!... kudonoa donoa sio inshu bwana umekilipia au kimelipiwa heshimu hela mama!!

9. Nipe namba nitakupigia halafu unajua wala huna mpango nayo! Aaaah jamani mwambie tu hapana sio kumsubirisha mwenzio kila simu ikiingia anajua ni wewe. Anajisonyesha uko siku mbili tatu hadi azoee ashachoka mwili na akili. Mwambie tu ukweli Hapana na umaanishe! next time atakuheshimu zaidi kuliko kuchukua namba ya mtu halafu mkikutana anajikuta unabeba dhambi ya uongo kujitetea why?! Kwanini?!

10. Am Single and I love it! Hapa wale akina single and not attached!...maana unaweza kuwa single ila attached to someone ni vile hamjaoana kisheria tu. Ila single ya not attached and am loving it! Mh shoga like really? sema haki ya mama…. Upweke unaupenda wewe?? Au zile Happy meeeee huku moyoni full mafundo ya roho. Wanaume wanaboa sana ila kusema huna mtu kabisa na una furaha I doubt it! Mapenzi yana raha yake weweeeee achaaaa!! Ila kama kweli Bravo maana wewe si wa kawaida!

11. Sina cha kuvaa huku kabati limejaa nguo, sasa sijui zilizojaa kabatini ni za kuvua au vipi? Tunacomplicate kweli mambo! 12. Mama anaumwa. Shangazi kalazwa nyumba inavuja msamvu. Hahahahaaaa haya mambo ya kusingizia majanga au watu wagonjwa ili upewe hela na Bae sio fresh aisee! Midomo uumba ujue! Hebu sema shida yako waziwazi kama ni ya maana atakupa kama si ya maana hadi udanganye jishtukie mwenyewe unatumiaje pesa kwa mambo yasiyo na maana. Vinginevyo anayekupenda hata ukimuomba elfu kumi ya chanuo atakupa mwenyewe akijiongeza kuna la ziada hapo!!

13. Sina hela jamani hapa nimetoka kulipa ada ya dogo sijui nini na nini. Huku unazo ila hutaki msaidia Bae. Ila wewe ukipewa excuse unanuna! Ikiwa anakusaidia siku akiyumba usitafute sababu kakope umsaidie na wewe…. Isiwe tu hatoiiiii halafu kiiiiila siku anakulilia shida mh hahahahaaaa Mwanaume huyo mh!

14. Siwezi kuishi bila wewe hapo umetamkiwa go to hell flani ya vitendo, Hunnie! Mama yako mwenyewe anaweza kuishi bila wewe iweje wewe ukashindwe kuishi sababu ya mtu ambaye hujamzaa wala kumlea mmekutana ukubwani uko kila mtu meno 32 yametimia! Inahusu? Uongooooo! Akifa leo utazikwa naye?Mwambie tu naumia roho nitakumiss ila kufa sababu yako aaaaah wapi bwana! i said this once hahahahahahahahaaaa nikaja gundua nilikuwa nang'ang'ania mzigo mzito saaaaana nisingeuweza maishani aliona anitue mapema!!

15. Heheheheheheeeeee niko period!.

NB: Kwa hisani ya laura petty
 
Huu uzi umejaa ukweli mtupu,asante sana kwa kuwatambua pretenders wa kwny mapenzi wanaobore...BIG UP for this thread mdada.
 
Ndoooooorooobooo we.......
mleta mada kumbuka ya kwamba "kuchamba kwingi mwisho unaishia kujipiga kidole".
 
Aha ha ah ah The 2moro pipo umeua, na wewe unahusika kwa yote au?? binafsi umenikamata vilivyo namba 2, 9, 11 na .....! 2 na 9 acha nibadilike kwakweli, ila 9 kuna watu wanaudhi aisee yani mtu unakataa lakini utalazimishwa weee hadi kero, mwisho naamua kumuomba tu, nikigeuka naifuta hapo hapo, kuna wengine watuwezi kumbwatukia mtu, unakuta mpo ktk daladala jamaa anakomaa kuomba namba unakataa anang'ang'ania njia nzima ni kero, kuna wengine wanaamua kubwatuka "bwanaeee sitaki huelewi" sasa yote haya ya nini!! Hiyo 11 sijui huwa inakuaje kuaje yani ndo maana naamua kutafuta nguo asubuhi ili nisifikilie sana kuchagua na kuwahi kuondoka

Nb: Wanawake na vijimambo
 
Mi niongelee #11 tu. . . .

Kusema sina cha kuvaa haina maana hatuna nguo kabisa, maana hatuoni cha kufaa kwa wakati huo. Kuna siku mtu kila nguo unayoifikiria unaona hapana. Hii unaona inabana sana ila ile isobana hujisikii kuivaa, unayotamani kuvaa unaona haifai labda sababu ya joto au unapoenda utakwaza watu and so on. Kwahiyo hatuzingui. .inatokea siku moja moja kila nguo inaonekana SIO.
 
Hahahahahahaaaa hio namba 15 hio hahahahahahaaaa na hio namba tatu hahahahahhaaaaa nimekuwa Nunda kwa kuambiwa hivyo nadhani aiseee!!! Halafu huwa najibu hivyo hivyo, juzi kati tu hapa yametokea halafu siku nne baadae, nikatumiwa text kwa Whatsapp. Ngoja niishie hapa hapa
 
Yote nimeipenda pretenders hapa inabidi wavae miwani hongera sana mleta uzi
 
No 9 tu ndo imenikamata ila nyingine ni pasu pasu sipendi kurefusha mambo
 
Aha ha ah ah The 2moro pipo umeua, na wewe unahusika kwa yote au?? binafsi umenikamata vilivyo namba 2, 9, 11 na .....! 2 na 9 acha nibadilike kwakweli, ila 9 kuna watu wanaudhi aisee yani mtu unakataa lakini utalazimishwa weee hadi kero, mwisho naamua kumuomba tu, nikigeuka naifuta hapo hapo, kuna wengine watuwezi kumbwatukia mtu, unakuta mpo ktk daladala jamaa anakomaa kuomba namba unakataa anang'ang'ania njia nzima ni kero, kuna wengine wanaamua kubwatuka "bwanaeee sitaki huelewi" sasa yote haya ya nini!! Hiyo 11 sijui huwa inakuaje kuaje yani ndo maana naamua kutafuta nguo asubuhi ili nisifikilie sana kuchagua na kuwahi kuondoka

Nb: Wanawake na vijimambo

Penda kubwatukaa ipo siku utakutana...! Jamaa yangu alimtokea na kumkomalia demu alipoambiwa SITAKI NA DEMU KWENYE DALADALA MSELA AKAJIBU "HUTAKI NINI ----- WEWE UJAMBE ETI NISIKWAMBIE UMEKOMAA UNAPUMUA UNAPUMUA...! UNAPUMUA KITU GANI WENZIO unatuvimbisha matumbo.
 
Namba 6 seriously am nobody's EX if we break up I don't know you.
 
Penda kubwatukaa ipo siku utakutana...! Jamaa yangu alimtokea na kumkomalia demu alipoambiwa SITAKI NA DEMU KWENYE DALADALA MSELA AKAJIBU "HUTAKI NINI ----- WEWE UJAMBE ETI NISIKWAMBIE UMEKOMAA UNAPUMUA UNAPUMUA...! UNAPUMUA KITU GANI WENZIO unatuvimbisha matumbo.

Ndo mana sipendi kubwatuka aisee
 
hiyo no. 1 sielewagi kwanini mnafanyaga hivyo?
 
Back
Top Bottom