Fire assembly point

shaks001

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
1,246
1,070
Najaribu kufikiria tu inakuwaje lile eneo lililoandikwa 'Fire assembly point'kwenye jengo husika ndipo na moto unawaka eneo hilo na watu ndio wameelekezwa watulie hapo linapotokea janga la moto.
 
Fire assembly point ni moja kati ya maamuzi Muhimu yanayofanywa na Fire risk assessment team wanapotoa cheti cha usalama wa kukabiliana na moto katika jengo au eneo husika.
Bahati kwa hapa kwetu hakuna anayejali sana Hilo.

Sasa ni jambo gani la kuzingatia unapochagua eneo kuwa fire assembly point( eneo la kukusanya watu Iwapo kumetokea moto ama kuna dalili/hisia za kutokea moto)

1. Je kuna umbali wa kutosha kutoka kwenye jengo husika?!
2. Je eneo ni toshelevu kwa idadi ya watu wanaotumia jengo husika?
3. Je ni rahisi kwa watu kufika eneo hilo na kuondoka kwa urahisi Iwapo watatakiwa kuondoka?!

Ukiiangalia hivyo vigezo ni majengo machache sana yanakidhi.
Majengo Mengi fire assembly point zipo mlangoni kabisa na nafasi hakuna.
Lakini ukifuatilia majengo hayo yana certificate za fire safety assessment.

Shukrani kwa kuleta hoja hii.
 
Back
Top Bottom