Kiutaratibu hata kama NGO ni ndogo; inahitaji iwe na Auditing Report, Annual report na return za kila mwaka kwa Msajili (Registrar).
Tuje kwenye kesi yenu; Kama mfadhili ametaka muambatanishe Certified Auditing Report kutoka kwa Auditor kwenye andiko lenu la mradi na nyie NGO yenu bado changa, haina documents hiyo; mbinu ya kwanza ni kuwasiliana na mfadhili kwanza kama anafikika. Kumuomba na kujadiliana nae juu ya hilo, wafadhili wengi huwa wanaweza kufanya consideration na wakawaruhusu mkaendelea, mkatuma Auditing report badae au mkatuma mbadala wake ambao mara nyingi ni Annual report ya shughuli zenu. Au wanaweza kuwapa namna yeyote mbadala wa kupata taarifa wanayoitaka.
Mbinu ya pili; Ni kuandaa Auditing report kabla ya kutuma andiko lenu. Sasa kwenye uandaaji ndipo watu wengi wa NGO, waga wanaingia mkenge wa kumdanganya mfadhili, kitu ambacho ni kosa kubwa sana. Wafadhili ni bora ukawapa hali halisi, luliko kuwadanganya. Kabla ya kuwapa mradi, mara nyingi wanakuja kufanya "due diligence" kubwa na wanaweza kugundua mliwadanganya kwa kuwapa hesabu za mizania ya fedha za uwongo. Mnaweza kuangukia kwenye fraud, forgery au kujipatika fedha kwa nia ya udanganyifu.
Ushauri wangu; Wafikieni, wapeni hoja yenu kwamba hamna/hamjaandaa hizo hesabu za mizania. Wafadhili wengi ni watu werevu. Ukimdanganya anafahamu, anaweza hata asifanyie kazi andiko lenu na asiwape funding sababu ya "Red flag" pamoja na andiko lenu zuri.
Kila la kheri; ukihitaji ushauri zaidi unaweza nicheki inbox.