Filamu ya kwanza Holywood kutumia soundtrack ya Bongo

Crank Nolasco

Member
Jun 20, 2016
7
7
Filamu inaitwa QUEEN OF KATWE.Ni kisa cha kweli kinachoelezea historia ya binti wa miaka 10 (PHIONA MUTESI) anaeishi katika lindi la umasikini uliokithiri na mama yake (LUPITA NYONG'O )npamoja na wadogo zake baada ya baba yao kufariki na kuwaacha wangali wadogo.

Filamu imetengenezwa KATWE kampala Uganda, Urusi na Sudan na inaakisi moja kwa moja maisha duni kabisa ya familia nyingi za kiafrika. PHIONA hakubahatika kwenda shule hivyo hajui kusoma wala kuandika kama ilivyo kwa wadogo zake. Shughuli kubwa wanayoifanya ni kuamka asubuhi na mapema na kwenda mitaani kuuza mahindi ya kuchemshwa kupata kipato cha kila siku.

Baadae anatokea mwalimu wa michezo(kocha Robert katende) anamfundisha mchezo wa Chess.PHIONA anajifunza kwa bidii usiku na mchana akiamini kuwa Chess huenda ikabadilisha maisha yake na familia yake.

KAMPUNI ILIYOTENGENEZA FILAMU HII NI WALT DISNEY.
Ikumbukwe kuwa kampuni hii si kampuni ndogo ni moja ya kampuni kongwe kabisa HOLYWOOD na kampuni ya mwanzo kabisa kubuni na kutengeneza animation mwaka 1923. Na pia iliendelea kudumu hata kipindi kigumu kabisa kutokea katika soko la filamu hii ilikuwa ni baada ya vita kuu ya pili ya dunia Mwaka 1945. Hii iliendelea kudumu na inafanya vizuri mpaka sasa.

KUTUMIKA KWA NYIMBO.
Sound iliyotumika katika moja ya scene ilitengenezwa na mtayarishaji mkongwe P FUNK Majani na PROF.JAY ndie alieitumia katika nyimbo aliyoipa jina la NIKUSAIDIEJE akiwa amemshirikisha Ferooz. Baadae ikarudiwa na Josee Chameleone kutoka Uganda japo ilileta mgogoro mkubwa.

SWALI ni kwamba je P Funk mwenyewe kanufaika na haki miliki ya kazi yake au hafahamu lolote juu ya hii filamu mpya iliyotoka mwishoni mwa mwaka? Profefa je? Analijua hilo pia. Kwa maana kutumika kwa sound ya P Funk kwenye filamu kubwa Holywood ni lazima malipo yamefanyika sehemu. Wasi wasi wangu ni kwamba wa Tanzania si wafuatiliaji wa mambo na ninawasiwasi pia malipo yamefanyika Uganda kwa Josee Chameleone.
 

Attachments

  • au_movie_poster_queenofkatwe_nr_f515024d.jpeg
    au_movie_poster_queenofkatwe_nr_f515024d.jpeg
    14.2 KB · Views: 43
Nimeiangalia hiyo movies iko vizuri sana na inaakisi mazingira halisi ya kiafrika hasa uswahilini......Lupita Nyong'o ameitendea haki.
 
Sasa kama Jose Chameleone wa hapa jirani kabisa tangu ameahidi kulipa hizo dola 2,000 miaka kadhaa nyuma hadi hii leo hajalipa na wahusika wako kimya hao wa wadaiwa wapya watalipa lini? Kuna tatizo kwenye sheria ya hatimiliki.
 
Sasa kama Jose Chameleone wa hapa jirani kabisa tangu ameahidi kulipa hizo dola 2,000 miaka kadhaa nyuma hadi hii leo hajalipa na wahusika wako kimya hao wa wadaiwa wapya watalipa lini? Kuna tatizo kwenye sheria ya hatimiliki.
Unataka pro alipwe ili iweje.

Kwani wasanii wetu wanavyotumia nyimbo zao hua tunalipa??
 
Mbona hiyo sio ya kwanza kuna movie iliwahi kutoka na sound track ya wimbo wa Saida Kaloli.
 
Unataka pro alipwe ili iweje.

Kwani wasanii wetu wanavyotumia nyimbo zao hua tunalipa??
Mkuu kinachofanyika ni makosa.kikawaida poducer anapotengeneza nyimbo.instrumental inabaki ni ya kwake na japo msanii ataitumia.sasa basi iwapo instrumental hiyo itatumika sehemu nyingine ni lazima producer ajue na aafiki.kilichofanyika hapa ni kwamba imetumika kazi ya p funk hollywood.sehem ambayo kila kitu kinalipwa.sasa malipo hayo hayajaja kwa p.yameenda kwa josee chameleon kitu ambacho ni kosa kubwa
 
Chameleone aliitumia kwa wimbo gani?
Mwaka 2008 mwishon chameleon aliiba beat kwa kificho na akafanya ngoma ikaleta mgogoro baadae wakampiga faini.katika kuliweka sawa hilo chameleon akamtafuta jay wakafanya kazi ile unavyodhan ndivyo sivyo.ilikuwa kitambo kidogo
 
Mwaka 2008 mwishon chameleon aliiba beat kwa kificho na akafanya ngoma ikaleta mgogoro baadae wakampiga faini.katika kuliweka sawa hilo chameleon akamtafuta jay wakafanya kazi ile unavyodhan ndivyo sivyo.ilikuwa kitambo kidogo
Imebidi nichungulie Youtube, aliitumia kwa wimbo Bomboclat akimshirikisha Wessel.
 
Back
Top Bottom