UNAAMKA KABURINI, UMEZUNGUKWA NA MAITI NA HAUKUMBUKI KITU. UNAFANYA NINI?
Mwanaume mmoja anaamka katikati ya giza. Hajui yuko wapi. Mwili wake una maumivu na huku kichwani hamna anachokumbuka.
Anajipekua mfukoni mwake na kubaini kuna funguo na kiberiti cha gesi. Anawasha kiberiti aangaze mazingira. Anagundua yuko ndani ya shimo kubwa na amezingirwa na maiti lukuki!
View attachment 2958972
Anashtuka.
Anatazama juu, anamwona mwanamke mmoja akiwa amesimama kando ya shimo. Anaomba msaada na mwanamke huyo anamtupia kamba.
View attachment 2958973
Mwanaume huyo anatoka kaburini na kwenda moja kwa moja kwenye nyumba fulani ambamo humo ndani anakuta watu watano; mwanamke mchina alomsaidia pamoja na watu wengine wanne.
Kati yao wanaume ni watatu na mwanamke ni mmoja. Wote hawa hamna anayekumbuka kitu isipokuwa mwanamke yule mchina, na mwanamke huyo ni bubu, hawezi kuongea.
Sasa watu hawa wanashukiana maana haijulikani nani ni rafiki na nani ni adui, achilia mbali hawajui wamefikaje hapa.
Lakini mashaka makubwa yapo kwa bwana huyu alotoka kaburini, kwanini yeye amezindukia huko na ingali wenzake wameamkia ndani?
Je, huyu sio muuaji?
View attachment 2958974
Muda kidogo watu wale wengine wanapata vitambulisho vyao vya leseni na kufahamu majina yao; Luka, Michael, Nathan na Sharon, ila huyu alotoka kaburini yeye bado hajulikani.
Pia yule mwanamke mchina, hamna anayemfahamu ingali wote hawa wameamka na kumkuta hapa.
Wanakagua humu ndani na bwana yule alotoka kaburini anabaini kuna kalenda iliyozungushiwa tarehe 8, yani siku mbili zijazo, lakini haijulikani siku hiyo kuna kitu gani haswa.
Wanapata mashaka.
Anaulizwa mwanamke mchina lakini atasema nini na yeye kuongea hawezi?
Baadae kidogo, mwanamke huyo mchina akiwa amebebelea taa, anakimbilia msituni pasipo kuaga.
Upesi wanamfuatilia anapoelekea na huko porini wanaona miili ya watu waliokufa ikiwa imefungiwa kwenye miti.
View attachment 2958975
Hawaelewi watu hao ni kina nani na kwanini wamefungiwa hapo.
Wanamkuta mchina kwenye kijumba fulani akiwa anamlisha chakula mwanamke mmoja aliyefungwa mikono.
Mwanamke huyo anapomwona mwanaume yule alotoka kaburini, anapandwa na hasira kali akitaka kumshambulia.
Hali inakuwa tete.
Mwanamke huyo anatulizwa na kitako cha bunduki, anazirai. Lakini hii inazidi kuongeza maswali juu ya bwana huyu wa kaburini.
Ni nani haswa?
Panapokucha, wanatoka kwenda kuangaza huko nje kutafuta magari kwa maana funguo wameamka nazo mifukoni. Nyumbani anabaki Michael na mwanamke mchina tu.
Huko porini, wanapata kuyaona magari kadhaa yakiwa yamefunikwa. Ndani ya gari moja, wanaipata picha waliyopiga wote kwa pamoja lakini haina sura ya bwana yule wa kaburini.
Yeye bado ni kitendawili..
View attachment 2958976
Wanacheki magari hayo na kubaini hayana mafuta ya kutosha. Kidogo wanakumbana na mwanamke mchina akiwa anakimbia kwa hofu. Wanamfuata mwanamke huyo na kufika eneo wanalomkuta Michael akiwa anajifia, ameshambuliwa na bwana mmoja alokuwa anajaribu kumsaidia.
Bwana huyo ni kama zombi mwenye kiu ya damu.
Wanammaliza kwa risasi kisha yule bwana alotoka kaburini akiwa pamoja na Sharon wanarudi kwenye yale magari kuchukua mojawapo ili watafute sehemu ya mafuta au magari yenye mafuta ya kutosha waondoke eneo hili.
Wanafika eneo fulani lenye jengo kubwa, wanatazama ndani na kumwona mtoto wa kiume. Wanamwomba afungue geti lakini ajabu mtoto anashikwa na woga mkubwa anapomwona mwanaume yule alotoka kaburini!
Anamwita mwanaume huyo kwa jina la Jonah lakini hataki kabisa kumfungulia.
Sasa Jonah ni nani?
View attachment 2958978
Walau mwanaume huyu amejua jina lake, lakini kwanini watu wanaokutana naye wanamwogopa kiasi hiki?
Anataka kujua zaidi yeye ni nani na mtoto huyu anaonekana kujua. Analazimisha kuingia ndani kwa kutumia bunduki, Sharon anamsihi asitumie nguvu kubwa na bahati mbaya mtoto anatoroka asijulikane ameelekea wapi.
Wanasonga mbele kidogo, wanakutana na watu wanaokata miti kwa shoka. Jonah anajaribu kuwapazia sauti ili wapate msaada lakini watu hao kumwona Jonah, wote wanacharuka na kuanza kuwakimbiza kama wendawazimu!
View attachment 2958979
Wanafanikiwa kutoroka lakini wanapofika nyumbani wanamkuta Luka akiwa ameshikilia bunduki anawangojea.
Luka sasa anajua huyu Jonah ni nani kwani alikumbana na kamera yenye video ya zamani, humo akaona yale ambayo Jonah alipata kuyafanya.
Kwahiyo Jonah anaposhuka tu kwenye gari anamnyooshea mdomo wa bunduki kisha anamwambia Sharon akae mbali na bwana huyo kwani ni hatari.
Kafanya nini?
Nini haswa kinaendelea hapa?
Kesho yake ni ile tarehe nane ya kwenye kalenda, kuna tukio gani?
Tazama "OPEN GRAVE"
View attachment 2958980