Fikiria kesho, Fikiria Tanzania ya kesho, Fikiria CCM ya kesho

Hizo picha hapo, unaweza zitolea maelezo?

Sent using Jamii Forums mobile app
FB_IMG_1578677028602.jpg
 
Natafakari sana hali ya nchi leo na kesho, mimi sio mganga wa kienyeji lakini nyayo zenu zinanifanya kuyaona ya kesho, na vishindo vikuu vitaanzia asubuhi tu kabla ya kesho yenyewe. Katika siasa za Lumumba naona wazi uamuzi wa busara wa kura mbili, kutakuwa na machaguo mawili tu, ama uchague kulihami taifa au uchague kuruhusu Chakubanga anawiri.

Kimsingi chama cha Mapinduzi baada ya uchaguzi kilifanikiwa kutengezeneza njia iliyotaka kuaminika kuwa ni bora na thabiti ya kuua chama kikuu cha upinzani, katika hili namheshimu sana gwiji la siasa za kimkakati wa ccm Komredi Mzee Kinana, agenda zote za upinzani zilibebwa na ccm japokuwa vilibebwa kinyumenyume, miezi mitatu ile ya utawala baada ya uchaguzi kilikuwa ni kipindi kigumu sana kwa chama kikuu cha upinzani CHADEMA.

Chama tawala kilimkabidhi kada wake John Magufuli aongoze kifo cha upinzania nchini, shabaha ya Kinana ilikuwa kuua upinzania "kisayansi na kwa hoja" akiwa kama mtendaji mkuu, mkakati alioanza nao tangu mwanzoni mwa mwaka 2015 kabla ya uchaguzi mkuu hali iliyompa ufuasi mkubwa wa watz kurudisha imani kwa chama tawala, mwenyekiti wake mpya John Magufuli akaja na mbinu yake mpya ambayo badala ya kuua upinzania kwa njia za kisayansi, yeye akaamua kuua upinzani kikatiba, kisheria na kimamlaka, hali iliyokiongezea umaarufu chama cha upinzania na kivuta huruma ya umma na Jumuiya za kimataifa imeelekezwa kwa upinzani nchini. Kibaya zaidi Magufuli amezalisha upinzani mkubwa ndani ya ccm kuliko hata ule ulio nje yao.

Magufuli sasa atalazimila kupigana vita mbili, vita ya ndani ambayo ni kubwa na ambayo 100% haiwezi kwakuwa yeye sio mwanasiasa kihistoria, vile vile atalazimika kupigana vita ya nje yenye kuongozwa na Mwamba wa siasa za Afrika Freeman Mbowe, lakini kosa kubwa zaidi litakalomgharimu Magufuli ni mwangwi wa gwiji wa sheria na siasa Bwana Tundu Lissu, Kwasasa Lissu anaijua siasa ya Magufuli na anajua vema siasa za provocation za kumtoa nyoka pangoni. Ukweli hii ngoma kama Magufuli haijui ccm atashangaa na roho yake. Magwiji wa ccm yaani wale magodfather wanazichanga karata kisiasa, yeye anazichanga karata kidola. Hali hii inafanya 2019 upinzania kupumua na mateso wanayopitia leo, Magufuli kama anataka kurejea madarakani atalazimika kuelekeza nguvu vita vya ndani kuliko aendelee kuushughulika na vita kwa chadema atakuta mtoto sio wake (Japo hili ameshachelewa muda ni mwalimu mzuri). Hilo naamini washauri wake watamwambia akibisha shauri yake, sisi waandishi wa historia tutakuja kuandika.

CCM wengi wanatambua kuwa Kwenye maswala ya demokrasia ya kuchagua na kuchaguliwa kila mtu ana uhuru wake, lakini wanatambua kwamba chamq chao si chama cha kuchagua na kuchaguliwa, bali ni chama cha amri na maelekezo toka juu, Demokrasia ina gharama yake na maumivu yake, hivyo ndivyo apatavyo Mzee Kikwete, Membe, Chenge, Mkapa, na wengine. Heshimuni hisia za mtu na uhuru wake kidemokrasia ndani ya CCM.

Pengine nilazimike kutoa somo dogo la demokrasia na namna inavyofanya kazi faida na hasara zake. Ndugu zangu katika ulimwengu wa tatu, demokrasia ni kitu kingine kabisa, hakihitaji tafakuri ya chema ama kibaya, demikrasia ni ya wengi wape hata kama wengi hao ni wajinga. Falsafa inasema umma haukosei, hata kama umma huo ni wa wajinga. Umma ni uungu ndio kusema umma unaumba chochote katika dunia. Na ndio tafasiri ya kiroho ya Wayunani wasemao Sauti ya wengi ni Sauti ya Mungu.

Ndiomaana demokrasia kwa watu makini (great thinkers) huwa hawaipendi, sio kwamba haifai bali ina maumivu makali. Yesu na Mtume Mohamed ni mifano hai ya wao kutopenda demokrasia na athari za demokrasia kwao mpaka leo, Mwisho wake Yesu akauawa kwa demokrasia ya wengi waliosema aamue.....Nani aachiwe Kati ya Hawa wawili?? Watu...Barbara aachiwe... Yesu asulubiwe...! Akasulubiwa na kuuawa kwasababu demokrasia ya wengi iliamua! Hii ndio gharama ya demokrasia.

Tafasiri ya falsafa ya kiroho inasema ililazimika kuwa hivyo ili andiko la Mungu litimie. Inamaana kwamba msimamo wa Mungu kwamba sauti ya wengi ni sauti ya Mungu si kwamba ulibadilika mbele ya watumishi wake Yesu na Mohamed, bali ili neno lake litimie ilikuwa ndio njia sahihi

Akina Karl Max na wengineo nao waliikataa demokrasia, lakini alama za nyakati hutawaliwa zaidi na mjinga... Maamuzi ya wengi yanasikilizwa hata kama ni yakijinga ama yanaliumiza taifa au jamii, ilimradi tumeridhia kwenda kidemokrasia yatupasa tukinywe kikombe hiki cha demokrasia.

Malengo na dhima ya dhana ya demokrasi toka kwa Wagiriki wasisi wa tawala za kidemokrasia ilikuwa ni "waelimishe kwanza" kisha wape uhuru wa kuamua kidemokrasia, lakini mapokeo ya nera yamekuwa "waghiribu kwanza" kwa kofia, kanga na vibaba vya unga na mchele, kisha waelekeze namna ya kuamua ikiwa kiitikadi ama vinginevyo ilimradi wanaamua vile utakavyo na wale wanjanjawanja wapeleke Ununio au Ubelgiji.

Mimi kutoka moyoni, huwa siipendi demokrasia kwakuwa huwa inanitweza muda wote inapowadia fursa ya kuamua kidemokrasi hasa katika mambo yanayohusu maslahi ya taifa. Kwasababu dunia ya leo ni ya kidemokrsia ninalazimika kuipenda demokrasia, kuiishi demokrasia na kuichagua demokrasia, lakini ni wazi, demokrasia ni ujinga uliovuka mipaka na unadumaza dunia ya tatu kusonga mbele, haya ni mawazo ya mjinga mmoja kutoka Mbutu!

Katika siasa na utawala ni jambo mtambuka sana linapokuja suala la demokrasia, Unapoamua kuwa mwanasiasa, tambua kuwa Demkrasia ni gharama na inamaumivu makubwa, ukiachilia mbali uwekezaji mkubwa wa raslimali pesa na muda unaofanywa na wanasiasa wa leo, tumeamua kuwa nchi ya kidemokrasia, chama cha kidemokrasia, tukubali matokeo ya kidemokrasia, tuwaunge mkono watu wetu wanaopatikana kidemokrasia. Na kubwa zaidi turuhusu njia za kidemokrasia zionrkane kwa macho, kwa hisia na zifanye kazi kwakuonekana wazi. Tatizo pekee la demokrasia nikwamba, hata mjinga ana haki ya kuongea na kusikilizwa.

Democrasia hapa kwetu ni Uhuru wa mjinga kuelekezwa kuamua mambo ya msingi.

Nisikuchoshe sana ukiwa hapo karantini, Bado haujachelewa, pata kitabu cha Ujasusi kwa ofa ya Karantini ya #CORONA kwa 25,000/= badala ya bei halisi ya 80,000/=,

Lipia 25,000 kwa 0715865544 au 0755865544 (Yericko Nyerere) kisha tuma majina yako na mahali ulipo, kitabu kitaletwa ulipo.
Nje ya Dar nauli ni 8,000/=

Na Yericko NyerereView attachment 1446865View attachment 1446867
Dishi limecheza wewe siyo bure. Unatuletea habari za kufirika hapa.Yaani hii Chadema iliyokufa inayokimbiwa na wanachama wake kila siku kwa udikteta wa mbowe ndo unataka kutuaminisha eti kitaweza kuikabili CCM. nyie jiandaeni kupambana na NCCR Mageuzi na ACT kuwa chama kikuu cha upinzani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom