o_2
JF-Expert Member
- Jul 20, 2017
- 431
- 388
Shwari?
Wakati tunazaliwa miaka ya 90s kulikuwa na wale mabro ambao wapo na harakati zao za kupiga mishe mishe wapate hela familia zao zipate kula. Mabro wa ukoo, mabroo wa familia kila mtoto alikuwa anatamani kuwa kama kaka yake.
Mabro walikuwa wanafanya juu chini, chochote wakiwezacho ili ile riziki basi waweze kuipata. Hakujalisha kama ilikuwa ni halali ama la. Na Mama zao, familia zao zilikuwa zinawaombea ili basi hustle zao ziwe na mafanikio.
Mabro waliokuwa wanasoma, waliokuwa wanafanya vizuri darasani basi wadogo zao ndio tulikuwa tunawaangalia.
Natamani niwe kama blaza. Bro kaenda shule ya kipaji sekondari. Kijiji kizima anafahamika. Na wewe unatamani kuwa kama bro. Bro kaenda UDSM kasoma education bumu asilimia zote, kamaliza chuo kazi inamsubiria kapata, maisha yanaendelea.
Zama zimebadilika. Role models wengi tumewapoteza kwenye bangi na unga. Vyuoni wamejaa tele na ajira hakuna. Bahati nzuri wazazi wetu hawataki tuwe wabunifu kufanya yale tunayoyataka. Wazazi wanataka tusome lakini tufanikiwe kama mabro miaka hiyo.
Siku hizi vijana tulio wengi tumewekeza maisha yetu kwenye mitandao. Hatuna kazi za maana tupo tupo na mambo ya betting na kupiga story za mipira vijiweni. Dira ya vijana inapotea.
Tumepotea vibaya. Tumesoma tunashindwa kujiajiri. Tumekuwa tegemezi. Sio marole models tena miaka 30 bado haujaanza chochote. Hauna chochote cha kujishughulisha nacho na bado una matumaini ya kuwa na maisha mazuri. Miaka 60 ijayo nchi hii itakuwa nchi ya hovyo kuwatokea.
Vijana wa leo tumejaa stress na hamu za kujiua kila mahali. Tusipoweza kujikomboa sisi wenyewe hakuna atakayeweza.
Vijana wa leo majanga, hao vijana wa kesho sijui itakuaje.
Tuishi.