Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kinatuhumiwa kupoka ushindi wa Meya wa Jiji la Tanga, na sasa madiwani wa Chama cha Wananchi (CUF) wamegoma kuendelea na shughuli za baraza la madiwani jijini humo, hadi suala la kupata meya halali aliyepokonywa na CCM litatuliwe.
Magdalena Sakaya, Naibu Katibu Mkuu (CUF) Bara amwaambia waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kwamba, uporaji huo hauvumiliki na kukubalika na kwamba madiwani wa CUF wameamua kusitisha shughuli zote za baraza.
“CUF kupitia Naibu Katibu Bara, ilifanya jitihada za kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo kwa kufanya vikao na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Tanga Mwantumu Mahiza ambaye aliahidi kuitisha kikao cha pamoja cha kutafuta ufumbuzi, lakini jambo hilo halikutekelezwa.” amesema Sakaya.
Sakaya ameeleza kuwa baada ya hatua ya awali kutoleta mafanikio alimtafuta George Simbachawene, Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kwa kumuandikia barua na kufanya mazungumzo naye ofisini kwake japo aliahidi kulishughulikia tatizo hilo lakini hadi leo hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
“Baada ya jitihada zote hizo za CUF, kilichofanyika sio kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo bali ni kuficha ukweli kwa kumhamisha Mkurugenzi aliyepindua matokeo na kumpeleka halmashauri nyingine,” amesema Sakaya.
Kwa upande wake Musa Mbarouk, Mbunge wa Tanga Mjini amesema endapo tatizo la Tanga halitatatuliwa maendeleo hayatafikiwa kwani takribani miezi mitano hakuna vikao vilivyofanyika hasa vikao vya bajeti.
Ameongeza kuwa CUF haiko tayari kuacha Jiji la Tanga kuongozwa na Meya asiyehalali na aliyepora demokrasia kwa masilahi yake binafsi na wenzake kwa kuwa wananchi wa Tanga walikataa kuongozwa na CCM ndiyo maana walichagua Mbunge kutoka CUF na madiwani wengi kutoka chama hicho ili Meya awe wa CUF.
Akizungumzia kilichotokea siku ya uchaguzi Mbarouk alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya Daudi Mayeji Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, kukimbia na sanduku la kura na kwenda kujifungia ofisini kwake ili kuzuia kura hizo kutohesabiwa kwa mara ya pili baada ya wajumbe wa CUF kukataa matokeo aliyotangaza ambayo yalikuwa kinyume na kura za wajumbe.
Mayeji alitangaza kura tofauti na matokeo halisi ambayo yalidai kuwa Rashid Jumbe wa CUF amepata kura 18 huku Suleimani Mustafa wa CCM amepata kura 19. Matokeo hayo yalikuwa tofauti nay ale yalisemwa na wakala wa CUF ambaye alisema Mgombea wa CUF amepata kura 20 na mgombea wa CCM amepata kura 17.
Source: Figisufigisu za Umeya zahamia Tanga