Genius Man
JF-Expert Member
- Apr 7, 2024
- 3,559
- 7,914
Fighting for Tanzania
"Fighting for Tanzania" ni nini ?
ni uhamasishaji wa mabadiliko chanya kwenye nchi na kupinga vikali matukio ya kiuhalifu na utekaji, matukio yote ya uvunjifu wa haki za binadamu, matukio yote ya matumizi mabaya ya madaraka, matukio yote ya ukiukwaji wa makusudi wa katiba ya nchi, matukio yote ya chaguzi sizizo za haki, matukio yote ya ubaguzi wa rangi, matukio yote ya ubaguzi wa uraia wa afrika mashariki na duniani kote, matukio yote ya kutumia vibaya rasilimali za nchi.
Fighting for Tanzania, ni uhamasishaji wa mabadiliko chanya na sio vurugu, au kuchoma moto ikulu au kituo cha polisi, au kumteka raisi, au aina yoyote ya uhalifu.
Fighting for Tanzania itaisha pale mabadiliko yatako fanyika kwenye nchi na kurudisha utawala wa vitendo wa haki ya kweli na demokrasia na sio mdomo pasipo ubaguzi wowote au aina yoyote isiyofaa.
Natumia uhamasishaji huu kuunga mkono mabadiliko na kuwaunga mkono wote walio tekwa na damu zilizo mwagika katika kupinga mambo yote maovu Tanzania, naunga mkono wapigania haki wanao shikiriwa kwa sababu ya kupigania haki na mabadiliko, naunga mkono wale wote walio pewa ulemavu kwa sababu ya kulipigani taifa.
Naunga mkono haki za wale wote ikiwemo wakenya waliobaguliwa na mamlaka ya Tanzania kutoingia.nchini pasipo kuwa na hatia yoyote au kosa lolote kisheria.
Nahamasisha watanzania kwa hiyari yako weka hii picha ya "Fighting for Tanzania" hapo juu kwenye profile yako kuonesha mshikamano wako kwenye kuhamasisha mabadiliko chanya kwenye taifa bila itikadi za kivyama wala kidini.
Weka hiyo picha kuunga mkono wale wote ambao damu zao zimemwagika kwaajili ya Tanzania, weka kuunga mkono wale wote walio shikiriwa kwa kulipigania taifa na kuongea ukweli bila kujali, weka kwaajili ya kuunga mkono mabadiliko ya kiuchaguzi, weka kwa kuunga mkono wale wotewaliobaguliwa na mamlaka ya Tanzania kuingia nchini.
ukishaweka comment hapo chini "FIGHTING FOR TANZANIA" wewe ni shujaa.