Fifa yawasimamisha Bin Hammam na Warner | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fifa yawasimamisha Bin Hammam na Warner

Discussion in 'Sports' started by kilimasera, May 30, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Shirikisho la mchezo wa soka duniani Fifa, limewasimamisha kwa muda wajumbe wawili wa kamati kuu, Mohamed Bin Hammam na Jack Warner baada ya kikao cha kamati yake ya maadili siku ya Jumapili.

  Shirikisho hilo sasa litaanzisha uchunguzi kamili juu ya madai kwamba wajumbe wa shirikisho la soka la Caribbean walipewa rushwa.

  Maafisa wawili wa shirikisho hilo Debbie Minguell na Jason Sylvester pia wamesimamishwa.

  Lakini rais wa Fifa Sepp Blatter hakupatikana na hatia yoyote.Petrus Damaseb,makamu mwenyekiti wa kamati ya maadili, alisema haya juu ya Bin Hammam na Warner: "tumeridhika kwamba kuna majibu tunayohitaji kuhusu suala hili."

  Hata hivyo, Fifa imesisitiza kuwa hawana hatia kwa sasa hadi itakapothibitishwa kuwa walihusika katika sakata hilo.

  Kama watapatikana na hatia, wanaweza kufukuzwa kutoka shirikisho hilo na kupigwa marufuku kushiriki shughuli zozote za mpira wa miguu.

  Bin Hammam alikuwa mpinzani pekee wa Blatter katika uchaguzi ujao wa urais wa Fifa lakini alijiondoa mapema siku ya Jumapili.
   
Loading...