Mphamvu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 10,702
- 3,356
Shirikisho la soka duniani FIFA, limeisimamisha kwa muda timu ya Taifa ya Nigeria kushiriki katika mashindano ya Kimataifa kutokana na Serikali ya nchi hiyo kuingilia kati michezo ya timu hiyo kinyume cha sheria na taratibu za FIFA kwa nchi wanachama.
Uamuzi huo ulifanyika Jumatatu baada ya wajumbe kadhaa wa shirikisho la soka la Nigeria (NFF) kufikishwa mahakamani.
"...wakati wa kusimamishwa kwa muda, shirikisho la NFF halitawakilishwa kwenye mashindano ya kanda, bara Afrika au kimataifa, pamoja na mechi za kirafiki," taarifa hiyo ya FIFA ilisema.
Kufuatia marufuku hii, hatma ya mechi ya wikiendi hii ya Nigeira dhidi ya Guinea mjini Conakry haijulikani.
Chanzo: Hatimaye FIFA yaifungia Nigeria - wavuti.weebly.com