Mwana Kwetu
JF-Expert Member
- Jul 12, 2011
- 652
- 607
Mnyonge mnyongeni lakini haki mpeni,Tanesco wanafanya kazi nzuri sana wakati huu ukilinganisha na kipindi chochote cha historia ya nchi yetu,tuwapongeze badala ya kuwakatisha tamaa kwa kuwa hiki ni kipindi cha mpito tu ambacho kina maboresho makubwa na utekelezaji wa miradi mikubwa kupitia REA.siasa zisiiingizwe kwenye mambo ya kisayansi
piga chini magamba october 25Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Ndg Mramba juzi alijitetea alipoulizwa kwa nini umeme ulikatika wakati Lowassa akitangazwa Live na ITV.
Alisema hajihusishi na siasa na pili kukatika kwa umeme kumesababishwa na matengenezo.
Mimi concern yangu ni uongo aliosema kuwa kukatika kwa umeme kutokana na matengenezo. Ninachotaka kieleweke wazi ni kuwa kunamgao wa umeme haswa hapa ARUSHA na ushahidi upo ila kwa sababu walishasema nchi hii hautakuwepo mgawo tena wanasingizia matengenezo.
Uzoefu unaonyesha kuwa matengenezo hufanyika hadi saa 12 au saa 1 jioni lakini kwa hapa Arusha umeme unakatika kwa zamu. Siku tatu unakatika mchana kutwa na siku tatu usiku.
Je kuna matengenezo gani yanafanyika usiku kama sio kudanganya. Kama siyo kudanganya matengenezo gani yanasababisha umeme kukatika zaidi ya mwezi mzima bila taarifa?
Kama kweli ni matengezo kwa mfano hapa Arusha atueleze yanafanyika wapi na kwa nini umeme unakatika hadi usiku ina maana TANESCO wanafanya kazi 24 hrs.
Mateso ni ya zaidi ya mwezi kwa hapa Arusha mjini na vitongoji vyake kwani kwa uzoefu wangu hali kama hii haijawahi tokea ambapo umeme unakatika kwa masaa 10 kwa zaidi ya mwezi sasa bila kuwepo taarifa zozote.
Pale ambapo kuna swala la kukatika kwa umeme Tanesco wanatoa taarifa inayoambatana na sababu za kukatika kwa umeme,hivi leo vijiji vingi vimeunganishwa na huduma ya umeme,je mbona mazuri yanayofanyika hatuyaweki humu jf, tutende haki kwa kutazama mazuri mengi yanayofanyika na tuache siasa kwenye mambo ya msingi,wengine humu jf nadhani si watanzania kwa hiyo hawana uelewa wa kutosha kuhusu yale yanayofanyika katika sekta ya nishati
Mnyonge mnyongeni lakini haki mpeni,Tanesco wanafanya kazi nzuri sana wakati huu ukilinganisha na kipindi chochote cha historia ya nchi yetu,tuwapongeze badala ya kuwakatisha tamaa kwa kuwa hiki ni kipindi cha mpito tu ambacho kina maboresho makubwa na utekelezaji wa miradi mikubwa kupitia REA.siasa zisiiingizwe kwenye mambo ya kisayansi
Acha kuleta porojo hapa...,Sio kweli kwamba mkurugenzi wa Tanesco amedanganya kwa kuwa kinachofanyika sasa ni kuboresha miundo mbinu ya umeme kote nchini,tuache siasa na kupotosha umma kuhusu kukatika kwa umeme katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwa kuwa