Fedheha kubwa polisi Singida

Fedheha kubwa polisi Singida

KALOKAZA

Member
Joined
Jan 3, 2013
Posts
95
Reaction score
135
Nilikuwa hapa Singida tangu jana, nimekuja kuchukua gari, nikiwa maneo ya stend ya zamani, kulitokea msichana ambaye jina lake Safina analalamika kuwa kulikuwa na kikundi cha wanaume wenye asili ya kiasia, (wahindi) wanamlazimisha kufanya naye mapenzi, kwa mujibu wa maelezo ya Dada huyo ni kuwa walitaka kumbaka walimlazimisha kumshika sehemu zake bila ridhaa.

Watanzania hao wenye asili ya kiasia (wahindi) walitoa pesa kwa Askari, yule Dada akamatwa, ameswekwa lock up, ila waliokuwa wanataka kubaka wanaendelea kudunda nje.

Rafiki zake yule mwanadada Jesca na Debora, waliokuwa wanafahamu uchafu wa vijana hao wamekamtwa asubuhi hii na kuwekwa lock up kwa kosa la kufanya fujo, bila kutajiwa waliyemfanyia fujo.

Polisi wamekamata aliyenusurika kubakwa, wakamwacha mbakaji, wanakamata mashahidi wa aliyetaka kubakwa, wabakaji wapo huru nje, Hayo yapo na yanaendelea kujiri sasa Kituo kikuu cha Polisi Singida, mamlaka husika zifuatilie ukatili huu.
 
Angalia yasije yakakutokea ya Mwangosi.... WAtakwambia "UNATUFUNDISHA KAZI"
 
wewe umechukua hatua gani kama mtanzania mpenda haki, maana haki bila usawa sio haki
 
police wa Tanzania Ni Hatari Sana! Mengi Yanatokea Ya Kikatili Ambayo Hayaripotiwi,kituko Kingine Kimefanywa Na Police Wa Kahama Ktk Kijiji Cha Ilogi,wamemkamata Mdaiwa Na Kumuweka Ndani Siku 2,huo Ni Ukatili Na Ni Kinyume Cha Sheria,mdaiwa Huwa Hawekwi Lock Up,hupelekewa Samasi Ili Akajibu Mashtaka Ya Deni Mahakamani,anapoidharau Amri Ya Mahakama Ya Kumtaka Aende Mahakani,hapo Ndipo Police Kisheria Wanaruhusiwa Kumkamata Na Kumfikisha Mahakamani Kwa Nguvu,kwa Nini Umkamate Mdaiwa? Amekuwa Mwizi? Police Wa Tanzania Ni Hatari Sana!
 
Polepole enyi watu! Hivi sasa jeshi la polisi lina igp mpya ila sijamfahamu bado kwa maana ya utendaji wake. Lakini nakushauri kama unayoysema ni kweli bai, sogelea hapo central ulizia dawati la kijinsia kisha uwape hicho kisa. Hukusikilizwa, mwone rpc
 
Hivi unadhani Polisi wanamsaada? Wao ni pesa tu
 
Nilikuwa hapa Singida tangu jana, nimekuja kuchukua gari, nikiwa maneo ya stend ya zamani, kulitokea msichana ambaye jina lake Safina analalamika kuwa kulikuwa na kikundi cha wanaume wenye asili ya kiasia, (wahindi) wanamlazimisha kufanya naye mapenzi, kwa mujibu wa maelezo ya Dada huyo ni kuwa walitaka kumbaka walimlazimisha kumshika sehemu zake bila ridhaa.

Watanzania hao wenye asili ya kiasia (wahindi) walitoa pesa kwa Askari, yule Dada akamatwa, ameswekwa lock up, ila waliokuwa wanataka kubaka wanaendelea kudunda nje.

Rafiki zake yule mwanadada Jesca na Debora, waliokuwa wanafahamu uchafu wa vijana hao wamekamtwa asubuhi hii na kuwekwa lock up kwa kosa la kufanya fujo, bila kutajiwa waliyemfanyia fujo.

Polisi wamekamata aliyenusurika kubakwa, wakamwacha mbakaji, wanakamata mashahidi wa aliyetaka kubakwa, wabakaji wapo huru nje, Hayo yapo na yanaendelea kujiri sasa Kituo kikuu cha Polisi Singida, mamlaka husika zifuatilie ukatili huu.

MCHANA: Naona Polisi wanaendelea kuhaha, wanatumika kwenda kwenye nyumba ya dada aliyefanyiwa ukatili huo ili kutoa vitisho, na wanajaribu sasa kumwokoa mhindi aliyefanya ukatili huo, mhindi anamwaga pesa kwa Askari na anajisifu hapa nje ya kituo kuwa hatafanyiwa lolote, yupo bize na simu. Askari nao wanakimbilia kila mmoja anataka afanye kazi ya kusikiliza kesi hii, aibu. wenye vyeo vidogo wanaachiwa wakubwa. Tuendelee kusubiri kusikiliza kauli ya RPC kuhusu ujinga wa askari wake na sinema ya mhindi huyu.
 
police wa Tanzania Ni Hatari Sana! Mengi Yanatokea Ya Kikatili Ambayo Hayaripotiwi,kituko Kingine Kimefanywa Na Police Wa Kahama Ktk Kijiji Cha Ilogi,wamemkamata Mdaiwa Na Kumuweka Ndani Siku 2,huo Ni Ukatili Na Ni Kinyume Cha Sheria,mdaiwa Huwa Hawekwi Lock Up,hupelekewa Samasi Ili Akajibu Mashtaka Ya Deni Mahakamani,anapoidharau Amri Ya Mahakama Ya Kumtaka Aende Mahakani,hapo Ndipo Police Kisheria Wanaruhusiwa Kumkamata Na Kumfikisha Mahakamani Kwa Nguvu,kwa Nini Umkamate Mdaiwa? Amekuwa Mwizi? Police Wa Tanzania Ni Hatari Sana!
Yawezekana ulikuwa ni wizi wa kuhaminiwa na ndiyo maana Polisi wakachukua hatua ya kumkamata.
ikiwa kama ukamataji huo umefanyika kinyume na sheria basi zipo hatua stahiki ambazo zinaweza kuchukuliwa.
 
Nenda kituo cha polisi arusha ndo utajua unyama wa polisi..kuna mtu anaitwa gwakisa ni zaidi ya mangu anafanya anavotaka
 
nina wasiwasi kidogo na mlolongo wa hiyo kesi, huyo dada anafanya shughuli gani hapo singida? alipotaka kubakwa aliripoti polisi? kama aliripoti iweje tena akamatwe yeye aliyeshitaki? nimejaribu kuwaza isije kuwa huyo dada ndio walewale wanaotumia miili kama kitega uchumi kamtoka muhindi ndio sababu kakamatwa.
 
Sasa fedhea inakujaje au majungu yenu tu je tutamuamini nani
 
Mkuu kwani kuleta humu jamvini huoni kama ni msaada?
Ni msaada kwetu maana ametuhabarisha na kumuongezea wingi wa huruma dada yetu, labda angeahirisha safari yake kwa masaa machache na kwenda kituoni kuonana na dada yetu, kisha azipeleke taarifa sehemu husika.Hata hivyo shukrani kwa kuonyesha mfano mwingine wa jinsi gani polisi wakitanznia wanatumika vibayana wageni.
 
Kumuhukumu asie na hatia ni sawa na kumuachia huru mkosaji
 
Ni msaada kwetu maana ametuhabarisha na kumuongezea wingi wa huruma dada yetu, labda angeahirisha safari yake kwa masaa machache na kwenda kituoni kuonana na dada yetu, kisha azipeleke taarifa sehemu husika.Hata hivyo shukrani kwa kuonyesha mfano mwingine wa jinsi gani polisi wakitanznia wanatumika vibayana wageni.
Ungejua wanaopita humu jamvini ungeshukuru kwa msaada aloutoa
 
Back
Top Bottom