Fedha za safari za rais zapigwa panga

ROBERT MICHAEL

JF-Expert Member
Oct 23, 2012
5,056
2,850
Kamati ya bajeti ambayo inayongozwa na mwanasheria mkuu mstaafu Andrew Chenge imepunguza bilioni 11 kutoka kwenye bajeti za safari za Rais kwa mwaka wa fedha ujao.Fedha hizo zitatumika kwenye miradi ya maendeleo.

Mwaka wa fedha ambao unaelekea kuisha Rais alitengewa bilioni 50 kwa ajili ya safari japo ndani ya miezi 2 zilikuwa tayari zimeshatumika.

Kwa hiyo mwaka ujao wa fedha ametengewa bilioni 39 kutoka bilioni 50
==========================================



Chanzo: Nipashe
 
Bado nyingi mnooo hizi ngazi ndo maana kila kukicha watu wanazitamani sasa safiri tu 39 billions honestly urais ni kazi inayolipa number 1 Tanzania hakuna cha udaktari uhandisi hakunaaa inasikitisha mno yaani billion 39 safari tu. Kwani ni lazima kusafiri labda niulize ni lazima?
 
Hicho ni kiini macho,atawatembeleaje 50 cents,Boyz 2men na wengine!
 
Pigwa changa la macho tu !!!! Ina maana hizo fedha zinatengwa kama lump sum na sio kulingana na safari ngapi kwa mwaka, watu wangapi, wapi na matokeo tarajiwa.
 
atatumia presidential decree kuzirudisha...mnataka akae magogoni apate majinamizi?nafikiri usiku jk ana sleep talk akitaja ndege hadi asubuhi..nasikia hela ya ikulu haifanyiwi audit,tutajuaje imepunguzwa,na hata akitumia bilioni 400 tutajuaje?nitoleeni usanii huu nyambaf..
 
Ha ...hawajamtendea haki Rais wangu. Je ni kigezo gani kimetumika kuzipunguza? Kama bilioni hamsini zimetumika kwa miezi 2 hizo mlizotenga mnataka asafiri kwa punda?
 
Mkuu ulitaka wamtengee shillingi ngapi Rais kwenye safari zake.
Mkuu yaani watenge kidogo mno. Hivi tujiulize tu hivi wewe hata kukiwa na kikao au safari ya familia hivi unaweza tumia pesa mara 5000 zaidi ya mshahara au kipato chako?
Ni mwendawazimu tu. Huwa sioni umuhimu wa kusafiri huko. Kama ni kutembeza bakuli basi zinaingia kwenye mfuko uliotoboka. Usishangae hata hizo pesa zote wanazotupa zinaishia kwenye safari. Kwa hiyo kila mwaka tunaenda omba pesa ili rais wetu atembee tembee kwanza hatuendi bwana wao ndo wanaenda kujiombea ngoja wazitumbue. Hatujui huwa wanawashawishi vipi jamaa wale. Si tukomae tu na yetu wandugu
 
Wampangie wastani wa safari moja kwa mwezi yenye kugharimu mil 500.

Kwa hiyo 10b zingetosha na chenji anarudisha

Mkuu hapo nimekupata tuwe na fixed figure za Rais kwa kila mwezi kwa ajili ya safari zake.
 
Mbona wamechelewa sana, Ila wasiishie tu kwa safari za Rais tu, wapunguze mpaka kwenye safari za mawaziri.
 
wasimfanyie khiyana bado hajakutana na Neymar,Suarez,Shwazzniger.na kutembelea Greenland
 
Hicho ni kiini macho, Kama mwaka huu alitengewa 50Bil na ziliisha ndani ya Miezi Miwili, Je Mwaka mzima atakuwa katumia ngapi? Kwa haraka haraka ni 300Bil, je hizo zilizozidi ametoa wapi?
 
Rais anaweza kusafiri wakati wowote hata kama kasma yake haijatengewa fedha kwa vile yeye ndiye afisa masuhuli mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…