Fedha za Rambirambi Lucky Vincent kutumika kukarabati hospitali ya Mount Meru

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,156
2,000
JINAMIZI la matumizi ya fedha za rambirambi kwenda kwa familia za wanafunzi limegeuka kaa la moto kwa kuamuliwa sehemu ya fedha hizo zipelekwe kukarabati Hospitali ya Mkoa wa Arusha Mount Meru.

Fedha hizo ni zinazotakiwa kuwasilishwa kwa familia za wanafunzi 33, walimu na dereva wa basi la Shule ya Lucky Vincent, waliofariki katika ajali iliyotokea wiki chache zilizopita.

Habari zinasema, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo anadaiwa kuwaita wazazi wafiwa akiwataka wakubali Sh milioni 56 walizotakiwa kupewa, zielekezwe kufanya mambo mengine tofauti.

Gumba anadaiwa kutaka fedha hizo zielekezwe katika mambo matatu ambayo ni kuboresha wodi ya wagonjwa mahututi (ICU), kujenga kitengo cha magonjwa ya akili au kuboresha chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru.

Akizungumza mjini hapa jana baada ya Ibada maalumu ya kuombea majeruhi walioko Marekani na wazazi waliopoteza watoto wao kwenye ajali hiyo, mmoja wa wazazi ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alisema wameamua kujitoa kwenye kamati ya kupanga matumizi ya Sh milioni 56 zilizobaki ili kuipa serikali fursa ya kupanga yenyewe matumizi ya fedha hizo.

Mzazi huyo aliyeomba kutotajwa gazetini kwa sababu za usalama wake, alisema wameamua kujitoa kwenye kamati hiyo baada ya kutoona sababu na umuhimu wa kuwapo kwao.

“Mambo mengi sana yalishafanywa na kukamilika, sisi tuliitwa Mei 16, mwaka huu kwa mkuu wa mkoa na kusomewa taarifa ya fedha zilizotumika.

“Baada ya kikao hicho ikaundwa kamati ya kusimamia Sh milioni 56 zilizokuwa zitumike kwa ajili ya kumbukumbu ya watu 35 waliokufa.

"Nilichaguliwa kuwa mmoja wa wanakamati tukiwa wanaume wawili na wanawake Wawili, tuungane na kamati iliyopo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa….wenzangu walikwenda kwenye kikao mimi sikwenda sikuwa na taarifa.

“Sh milioni 56 zilizobakia tuliambiwa tuangalie zifanye nini huku tayari mapendekezo yakiwa ni Hospitali ya Mount Meru kwamba zifanye maboresho chumba cha kuhifadhi maiti, chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) au kuweka kitengo cha magonjwa ya akili badala ya wagonjwa kupelekwa Hospitali ya Mawenzi au Mirembe Dodoma,” alisema mzazi huyo.

Mzazi huyo alidai kwamba Ijumaa iliyopita walikwenda Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa na kueleza nia yao ya kutoendelea kwenye kamati hiyo kama sehemu ya wazazi waliofiwa.

“Tumeona ni vema serikali iendelee na utaratibu wote kwa sababu kitendo pia cha wazazi wafiwa kuwekwa chini ya ulinzi na polisi kule shuleni Lucky Vincent kilitusukuma kuona hatuna sababu ya kuwa sehemu ya kamati,” alisema mzazi huyo na kuongeza:

“Tuliitwa baada ya mambo yote kukamilika, kwa ujumla hatukuridhishwa na fedha za rambirambi kubadilishiwa matumizi.

“Kubwa linalotusikitisha ni kuambiwa kwamba fedha hizo za rambirambi zimetokana na nguvu ya uchangishaji ya mkuu wa mkoa kwa hiyo wana haki ya kuzifanyia utaratibu wao wenyewe,” alisema.

Taarifa inayodaiwa kutolewa na Gambo iliyosambaa katika mitandao mbalimbali ya jamii jana, ilimnukuu mkuu huyo wa mkoa akisema ameona ni vema nguvu kubwa ikapelekwa kuwahudumia majeruhi watatu wanaopatiwa matibabu Marekani.

Kupitia taarifa hiyo, Gambo alisema hadi Mei 20 mwaka huu kutokana na wadau kuendelea kuchangia rambirambi, zimepatikana zaidi ya Sh milioni 67.9, hivyo fedha hizo zitatumika kuwahudumia majeruhi hao.

“Kutokana na wadau kuendelea kuchangia tumebakiwa na Sh milioni 67,993,885, kwa mantiki hiyo busara imeelekeza kuwa nguvu kubwa sasa ipelekwe kwenye kuwahudumia majeruhi maana hata tufanyeje wale ambao Mungu kwa mapenzi yake amewachukua hatuna namna tena ya kuwarudisha,” alisema na kuongeza.

"Jumatatu Mei 22 mwaka huu tutazitumia familia za majeruhi na madaktari wetu waliojitoa kuwasindikiza majeruhi Dola za Marekani 20,000 (Sh 44,720,000), kila familia itapata Dola 5,000, daktari Dola 2500 na muuguzi Dola 2500, kama sehemu ya kuendelea kuwafariji na kuwapunguzia changamoto huko ugenini".

Gambo alisema baada ya matumizi hayo zitabaki zaidi ya Sh milioni 22.2 huku hali za majeruhi zikiendelewa kuangaliwa na fedha zilizobaki zitaendelea kuwekewa utaratibu kupitia timu ya wafiwa wane walioteuliwa na wafiwa wenzao kushirikiana na serikali kuhakikisha mapato na matumizi ya suala hilo yanaeleweka kwa umma.

Alisema pia kuwa ofisi yake imehitimisha rasmi hatua ya kupokea rambirambi ili ipate muda zaidi wa kufuatilia mustakabali wa majeruhi walioko Marekani kwa

matibabu.

Akijibu hoja za fedha kuchepushwa na kupelekwa katika ujenzi wa hospitali, Gambo aliwashangaa watu wanaojadili hewa kwani hakuna fedha iliyopelekwa katika ujenzi.“Mnajadili hewa badala ya taarifa sahihi. Hakuna hela iliyokwenda Mount Meru Hospitali. Mtu ukiwa mnafiki ukiwa kijana ukizeeka unakuwa mchawi,” alijibu Gambo katika moja la magropu ya mtandao wa kijamii wa WhatApp

MEYA
Katika ibada ya jana, mbali na wazazi na walezi waliopoteza watoto wao katika ajali hiyo, wengine weliokuwapo ni Meya. Calist Lazaro madiwani wa Halmashauri ya Jiji hilo na wengine kutoka Halmashauri ya Meru.

Akizungumzia hatua ya kamati hiyo kujitoa kabla ya kufanya shughuli iliyokusudiwa, Lazaro alisema kwa vile suala hilo lina ukakasi, wananchi wa Arusha na viongozi wengine ambao hawakushirikishwa katika mchakato huo, hawatashiriki jambo lolote kuhusu fedha za rambirambi zilizobaki kwa Gambo.

"Nashukuru Mungu amesaidia leo tumehitimisha ibada maalum ya kuwaombea watoto wetu wanaotibiwa Marekani ila kwa uamuzi huo wa wazazi wetu ambao wamechukizwa na vitendo ambavyo Mkuu wa Mkoa anaendelea kuvifanya, wa kuamua kujitoa kwenye kamati, tunawaunga mkono na hatutaingilia jambo hili ambalo lilikwisha kuharibiwa,” alisema.

CHANZO: Mtanzania
 
BONGE BONGE

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
3,708

CHANZO: Mtanzania[/QUOTE]

Mzazi aliomba asitajwe gazetini lakini ukisoma hizi paragraph nilizo quote tayari anajulikana! Mwandishi jinsi alivyoandika story imemtaja!!!
 
Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,081
2,000
Aibu kubwa sana kuona serikali inagombania pesa za rambirambi. Ni vyema mkuu wa mkoa ajitoe kwenye michango na kuachia kamati wao wenyewe waamue watakavyotumia hizo pesa.
Dunia itatushangaa sana kwani hata wale watoto bila kupata msaada wa kutoka nje wasingepata matatibabu ilikuwa jukumuu ya serikali kuwatafutia matibabu wale watoto, nini maana ya watanzania kulipa kodi kama serikali inashindwa kutoa matibabu kwa raia wake.
 
majoto

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
2,194
2,000
Kuna watu wanaombea majanga makubwa makubwa yatokeee wajishibishe matumbo yao. Hakika mmelaaniwa duniani na ahera... hata shetani anawashangaaa!
 
LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
6,682
2,000
Kuna vitu vina maulizo mengi hapa. Inakuwaje kusema wanaimarisha motuary?? Nijuavyo motuary ya Mount Meru imebinafsishiwa mtu. Je mapato yatokanayo na ubinafsishwaji huo yanafanya nini hadi pesa za rambirambi zinakwenda motuary?
Jamani tunahitaji hekima sana kwenye hili jambo
 
kindafu

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
1,292
2,000
JINAMIZI la matumizi ya fedha za rambirambi kwenda kwa familia za wanafunzi limegeuka kaa la moto kwa kuamuliwa sehemu ya fedha hizo zipelekwe kukarabati Hospitali ya Mkoa wa Arusha Mount Meru.

Fedha hizo ni zinazotakiwa kuwasilishwa kwa familia za wanafunzi 33, walimu na dereva wa basi la Shule ya Lucky Vincent, waliofariki katika ajali iliyotokea wiki chache zilizopita.

Habari zinasema, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo anadaiwa kuwaita wazazi wafiwa akiwataka wakubali Sh milioni 56 walizotakiwa kupewa, zielekezwe kufanya mambo mengine tofauti.

Gumba anadaiwa kutaka fedha hizo zielekezwe katika mambo matatu ambayo ni kuboresha wodi ya wagonjwa mahututi (ICU), kujenga kitengo cha magonjwa ya akili au kuboresha chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru.

Akizungumza mjini hapa jana baada ya Ibada maalumu ya kuombea majeruhi walioko Marekani na wazazi waliopoteza watoto wao kwenye ajali hiyo, mmoja wa wazazi ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alisema wameamua kujitoa kwenye kamati ya kupanga matumizi ya Sh milioni 56 zilizobaki ili kuipa serikali fursa ya kupanga yenyewe matumizi ya fedha hizo.

Mzazi huyo aliyeomba kutotajwa gazetini kwa sababu za usalama wake, alisema wameamua kujitoa kwenye kamati hiyo baada ya kutoona sababu na umuhimu wa kuwapo kwao.

“Mambo mengi sana yalishafanywa na kukamilika, sisi tuliitwa Mei 16, mwaka huu kwa mkuu wa mkoa na kusomewa taarifa ya fedha zilizotumika.

“Baada ya kikao hicho ikaundwa kamati ya kusimamia Sh milioni 56 zilizokuwa zitumike kwa ajili ya kumbukumbu ya watu 35 waliokufa.

"Nilichaguliwa kuwa mmoja wa wanakamati tukiwa wanaume wawili na wanawake Wawili, tuungane na kamati iliyopo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa….wenzangu walikwenda kwenye kikao mimi sikwenda sikuwa na taarifa.

“Sh milioni 56 zilizobakia tuliambiwa tuangalie zifanye nini huku tayari mapendekezo yakiwa ni Hospitali ya Mount Meru kwamba zifanye maboresho chumba cha kuhifadhi maiti, chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) au kuweka kitengo cha magonjwa ya akili badala ya wagonjwa kupelekwa Hospitali ya Mawenzi au Mirembe Dodoma,” alisema mzazi huyo.

Mzazi huyo alidai kwamba Ijumaa iliyopita walikwenda Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa na kueleza nia yao ya kutoendelea kwenye kamati hiyo kama sehemu ya wazazi waliofiwa.

“Tumeona ni vema serikali iendelee na utaratibu wote kwa sababu kitendo pia cha wazazi wafiwa kuwekwa chini ya ulinzi na polisi kule shuleni Lucky Vincent kilitusukuma kuona hatuna sababu ya kuwa sehemu ya kamati,” alisema mzazi huyo na kuongeza:

“Tuliitwa baada ya mambo yote kukamilika, kwa ujumla hatukuridhishwa na fedha za rambirambi kubadilishiwa matumizi.

“Kubwa linalotusikitisha ni kuambiwa kwamba fedha hizo za rambirambi zimetokana na nguvu ya uchangishaji ya mkuu wa mkoa kwa hiyo wana haki ya kuzifanyia utaratibu wao wenyewe,” alisema.

Taarifa inayodaiwa kutolewa na Gambo iliyosambaa katika mitandao mbalimbali ya jamii jana, ilimnukuu mkuu huyo wa mkoa akisema ameona ni vema nguvu kubwa ikapelekwa kuwahudumia majeruhi watatu wanaopatiwa matibabu Marekani.

Kupitia taarifa hiyo, Gambo alisema hadi Mei 20 mwaka huu kutokana na wadau kuendelea kuchangia rambirambi, zimepatikana zaidi ya Sh milioni 67.9, hivyo fedha hizo zitatumika kuwahudumia majeruhi hao.

“Kutokana na wadau kuendelea kuchangia tumebakiwa na Sh milioni 67,993,885, kwa mantiki hiyo busara imeelekeza kuwa nguvu kubwa sasa ipelekwe kwenye kuwahudumia majeruhi maana hata tufanyeje wale ambao Mungu kwa mapenzi yake amewachukua hatuna namna tena ya kuwarudisha,” alisema na kuongeza.

"Jumatatu Mei 22 mwaka huu tutazitumia familia za majeruhi na madaktari wetu waliojitoa kuwasindikiza majeruhi Dola za Marekani 20,000 (Sh 44,720,000), kila familia itapata Dola 5,000, daktari Dola 2500 na muuguzi Dola 2500, kama sehemu ya kuendelea kuwafariji na kuwapunguzia changamoto huko ugenini".

Gambo alisema baada ya matumizi hayo zitabaki zaidi ya Sh milioni 22.2 huku hali za majeruhi zikiendelewa kuangaliwa na fedha zilizobaki zitaendelea kuwekewa utaratibu kupitia timu ya wafiwa wane walioteuliwa na wafiwa wenzao kushirikiana na serikali kuhakikisha mapato na matumizi ya suala hilo yanaeleweka kwa umma.

Alisema pia kuwa ofisi yake imehitimisha rasmi hatua ya kupokea rambirambi ili ipate muda zaidi wa kufuatilia mustakabali wa majeruhi walioko Marekani kwa

matibabu.

Akijibu hoja za fedha kuchepushwa na kupelekwa katika ujenzi wa hospitali, Gambo aliwashangaa watu wanaojadili hewa kwani hakuna fedha iliyopelekwa katika ujenzi.“Mnajadili hewa badala ya taarifa sahihi. Hakuna hela iliyokwenda Mount Meru Hospitali. Mtu ukiwa mnafiki ukiwa kijana ukizeeka unakuwa mchawi,” alijibu Gambo katika moja la magropu ya mtandao wa kijamii wa WhatApp

MEYA
Katika ibada ya jana, mbali na wazazi na walezi waliopoteza watoto wao katika ajali hiyo, wengine weliokuwapo ni Meya. Calist Lazaro madiwani wa Halmashauri ya Jiji hilo na wengine kutoka Halmashauri ya Meru.

Akizungumzia hatua ya kamati hiyo kujitoa kabla ya kufanya shughuli iliyokusudiwa, Lazaro alisema kwa vile suala hilo lina ukakasi, wananchi wa Arusha na viongozi wengine ambao hawakushirikishwa katika mchakato huo, hawatashiriki jambo lolote kuhusu fedha za rambirambi zilizobaki kwa Gambo.

"Nashukuru Mungu amesaidia leo tumehitimisha ibada maalum ya kuwaombea watoto wetu wanaotibiwa Marekani ila kwa uamuzi huo wa wazazi wetu ambao wamechukizwa na vitendo ambavyo Mkuu wa Mkoa anaendelea kuvifanya, wa kuamua kujitoa kwenye kamati, tunawaunga mkono na hatutaingilia jambo hili ambalo lilikwisha kuharibiwa,” alisema.

CHANZO: Mtanzania

Haya ni mambo ya aibu sana! Yanamuaibisha Gambo kama Gambo, yanamuaibisha Gambo kama RC, yanamuaibisha aliyemteua asipochukua hatua stahiki, na analiaibisha Taifa la Tanzania! Hata ukisoma ile ripoti inadaiwa kutolewa na RC ya matumizi ya fedha za rambi rambi unabaki na maswali mengi kuhusu matumizi ya fedha zetu za kodi zinazotengwa kwenye bajeti ya maafa & majanga! Haya maswala yanapandisha duku duku na hasira hata kwa wananchi wasiopenda kujishughulisha na maswala ya siasa!!
 
ndayilagije

JF-Expert Member
Nov 7, 2016
7,487
2,000
Haka katabia hakaso kufiwa ni dili eeh,wazazi jamani indeed mnalilia rambirambi !!aisee arusha kiboko.
 
QUIGLEY

JF-Expert Member
May 23, 2015
27,705
2,000
Mzazi huyo aliyeomba kutotajwa gazetini kwa sababu za usalama wake, alisema wameamua kujitoa kwenye kamati hiyo baada ya kutoona sababu na umuhimu wa kuwapo kwao.

"Nilichaguliwa kuwa mmoja wa wanakamati tukiwa wanaume wawili na wanawake Wawili, tuungane na kamati iliyopo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa….wenzangu walikwenda kwenye kikao mimi sikwenda sikuwa na taarifa.

CHANZO: Mtanzania

Mzazi aliomba asitajwe gazetini lakini ukisoma hizi paragraph nilizo quote tayari anajulikana! Mwandishi jinsi alivyoandika story imemtaja!!![/QUOTE]
Nami najiuliza mbona kajitaja mwenyewe?
 
Kihava

JF-Expert Member
May 23, 2016
4,300
2,000
Ibara 4 (1) ya ilani ya CCM 2020 itasomeka hivi: " Haya yote tunayoyaahidi tutayatekeleza kwa mapato toka vyanzo vya kuaminika vifuatavyo"
1. Rambirambi za misiba na majanga watakayoyapata wananchi wetu. Tuna uhakika mkubwa wa chanzo hiki cha mapato.
2. Makusanyo ya vyanzo vingine vya mapato kama vile Sigara na pombe.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom