Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,350
- 26,166
Mimi nawashukuru MCC kwa kutugutusha watanzania na kuturudisha nyuma kifikra ili tujijue tumetoka wapi.Hatimaye Tanzania imekosa fedha za Millenium Challenge Corporation (MCC) zilizotarajiwa kutolewa kwa lengo la kupunguza umaskini nchini. MCC ni shirika la Kimarekani linalolenga kupunguza umaskini barani Afrika. Njia inayotumiwa na shirika hilo ni kutoa fedha za kimsaada kuelekeza katika sekta za kimaisha ili kupunguza umaskini.
Nchi mojawapo iliyokwishanufaika na fedha hizo ni Tanzania. Mara hii Tanzania imesitishwa kupewa msaada huo wa MCC kwakuwa kuna masuala ya kiutawala yanapaswa kufanyiwa kazi. Masuala hayo ya kiutawala yanayopaswa kufanyiwa kazi ndiyo hasa masharti ya kutimizwa na Tanzania kama nchi katika kupata msaada huo.
Katika taarifa ya MCC, masuala hayo ya kiutawala hayakutajwa. Hatahivyo, wachambuzi wa mambo wameyataja kama ni mgogoro wa kikatiba na kisiasa Zanzibar pamoja na Sheria ya Makosa ya Kimtandao. Ndiyo kusema, Tanzania ikishughulikia mgogoro wa Zanzibar na 'kuweka sawa' baadhi ya vifungu vya Sheria tajwa, Tanzania itapata fedha za MCC.
Iko wazi kuwa Tanzania Tanzania inazihutaji fedha hizi za MCC ili kusaidia katika sekta mbalimbali za kimaendeleo. Ndiyo maana hata Serikali ilikuwa ikijivunia kuwekwa kwenye orodha ya kupata fedha za MCC kwa kupitishwa kwenye vikao vya MCC (kumbuka kauli ya mmoja wa viongozi wa Serikali wakati wa sakata la Escrow).
Tunapaswa kama nchi kutatua mgogoro wa Zanzibar. Kama kilichoripotiwa leo ni kweli, kwamba Rais Magufuli amekutana na Maalim Seif Sharrif Hamad Ikulu, basi kuna dalili kuwa Serikali imedhamiria kuutatua mgogoro wa Zanzibar. Mgogoro wa Zanzibar unapaswa kutatuliwa kwa kutenda haki na kusonga mbele kama Taifa.
Kuutatua kwake ni aidha kuendelea na mchakato wa kutangaza matokeo (kwa kuachana na kauli ya Mwenyekiti Jecha wa ZEC kufuta uchaguzi wote Zanzibar) au kwa kukubali kufanya uchaguzi upya. Ifahamike kuwa mgogoro haupo kwenye Urais tu. Upo pia kwenye Uwakilishi na Udiwani kwakuwa wote hao wameathirika na kauli ya Mwenyekiti Jecha.
Lakini, kwanini Dr. Shein naye asifanye mazungumzo na Rais Magufuli au wote watatu kwa pamoja? Kuhusu sheria, inapaswa kurekebishwa Bungeni na mambo mengine kuendelea. MCC wakijiridhisha juu ya hilo, Tanzania itapata fedha ambazo inazihitaji. Yote yasemwe lakini fedha za MCC zinahitajika na masharti yaliyowekwa yanatekelezeka.
Unasahau pia kuwa Mwalimu yalimshinda akaachia ngazi na fedhanyetu ikashuka thamani! Hiyo nguvu kwa dunia ya sasa hatuna. Afadhalimkidogo wakati hule wa vita baridi, lakini siyo sasa!Mimi nawashukuru MCC kwa kutugutusha watanzania na kuturudisha nyuma kifikra ili tujijue tumetoka wapi.
Ukishaingia katika tabia ya kiinchi kuvaa tai kumfurahisha mfadhili ili ndo uendelee, utakuwa na matatizo daima.
Watanzania lazima turudi nyuma na kujiona ni wapi tumekosea hadi kuingia hizi tabia za kijinga za kumfurahisha mfadhili , ati ndo utaendelea.
Haikuwa hivyo chini ya Mwalimu,
Inabdi watanzania tujifunze kukaza mikanda, tukope hiyo pesa na miradi iendelee.
Hata waswahili waliseam , mtumai cha nduguye hufa masikini.
Hiyo miradi iliyokuwa ifadhiliwe na MCC, tunaweza kabisa kuifadhili sisis wenyewe , tena kwa kodi zetu-tukiwa serious!
Na tunaweza kuachana kabisa na MCC, na kudhalilishwa huku.
Kodi ikusanwe, watu wafanye kazi maisha yaendelee, MCC wabaki na hela yao.
Mnafik mkubwa wewe. Eti unaishi bila umeme tangu nchi hii ipate uhuru wakati unashinda hapa JF usiku kucha kuperuzi na kumwaga pumba. Achana na hiyo lugha ya kuzungusha mikono aisee, imepitwa na wakati....Waathirika wakuu wa kukosekana kwa msaada huu ni sisi tunsoishi vijijini ambao tunaishi bila umeme tangu nchi hii ipate uhuru
Hatimaye Tanzania imekosa fedha za Millenium Challenge Corporation (MCC) zilizotarajiwa kutolewa kwa lengo la kupunguza umaskini nchini. MCC ni shirika la Kimarekani linalolenga kupunguza umaskini barani Afrika. Njia inayotumiwa na shirika hilo ni kutoa fedha za kimsaada kuelekeza katika sekta za kimaisha ili kupunguza umaskini.
Nchi mojawapo iliyokwishanufaika na fedha hizo ni Tanzania. Mara hii Tanzania imesitishwa kupewa msaada huo wa MCC kwakuwa kuna masuala ya kiutawala yanapaswa kufanyiwa kazi. Masuala hayo ya kiutawala yanayopaswa kufanyiwa kazi ndiyo hasa masharti ya kutimizwa na Tanzania kama nchi katika kupata msaada huo.
Katika taarifa ya MCC, masuala hayo ya kiutawala hayakutajwa. Hatahivyo, wachambuzi wa mambo wameyataja kama ni mgogoro wa kikatiba na kisiasa Zanzibar pamoja na Sheria ya Makosa ya Kimtandao. Ndiyo kusema, Tanzania ikishughulikia mgogoro wa Zanzibar na 'kuweka sawa' baadhi ya vifungu vya Sheria tajwa, Tanzania itapata fedha za MCC.
Iko wazi kuwa Tanzania Tanzania inazihutaji fedha hizi za MCC ili kusaidia katika sekta mbalimbali za kimaendeleo. Ndiyo maana hata Serikali ilikuwa ikijivunia kuwekwa kwenye orodha ya kupata fedha za MCC kwa kupitishwa kwenye vikao vya MCC (kumbuka kauli ya mmoja wa viongozi wa Serikali wakati wa sakata la Escrow).
Tunapaswa kama nchi kutatua mgogoro wa Zanzibar. Kama kilichoripotiwa leo ni kweli, kwamba Rais Magufuli amekutana na Maalim Seif Sharrif Hamad Ikulu, basi kuna dalili kuwa Serikali imedhamiria kuutatua mgogoro wa Zanzibar. Mgogoro wa Zanzibar unapaswa kutatuliwa kwa kutenda haki na kusonga mbele kama Taifa.
Kuutatua kwake ni aidha kuendelea na mchakato wa kutangaza matokeo (kwa kuachana na kauli ya Mwenyekiti Jecha wa ZEC kufuta uchaguzi wote Zanzibar) au kwa kukubali kufanya uchaguzi upya. Ifahamike kuwa mgogoro haupo kwenye Urais tu. Upo pia kwenye Uwakilishi na Udiwani kwakuwa wote hao wameathirika na kauli ya Mwenyekiti Jecha.
Lakini, kwanini Dr. Shein naye asifanye mazungumzo na Rais Magufuli au wote watatu kwa pamoja? Kuhusu sheria, inapaswa kurekebishwa Bungeni na mambo mengine kuendelea. MCC wakijiridhisha juu ya hilo, Tanzania itapata fedha ambazo inazihitaji. Yote yasemwe lakini fedha za MCC zinahitajika na masharti yaliyowekwa yanatekelezeka.
Mimi nawashukuru MCC kwa kutugutusha watanzania na kuturudisha nyuma kifikra ili tujijue tumetoka wapi.
Ukishaingia katika tabia ya kiinchi kuvaa tai kumfurahisha mfadhili ili ndo uendelee, utakuwa na matatizo daima.
Watanzania lazima turudi nyuma na kujiona ni wapi tumekosea hadi kuingia hizi tabia za kijinga za kumfurahisha mfadhili , ati ndo utaendelea.
Haikuwa hivyo chini ya Mwalimu,
Inabdi watanzania tujifunze kukaza mikanda, tukope hiyo pesa na miradi iendelee.
Hata waswahili waliseam , mtumai cha nduguye hufa masikini.
Hiyo miradi iliyokuwa ifadhiliwe na MCC, tunaweza kabisa
kuifadhili sisis wenyewe , tena kwa kodi zetu-tukiwa serious!
Na tunaweza kuachana kabisa na MCC, na kudhalilishwa huku.
Kodi ikusanwe, watu wafanye kazi maisha yaendelee, MCC wabaki na hela yao.
Mnafik mkubwa wewe. Eti unaishi bila umeme tangu nchi hii ipate uhuru wakati unashinda hapa JF usiku kucha kuperuzi na kumwaga pumba. Achana na hiyo lugha ya kuzungusha mikono aisee, imepitwa na wakati.
Uchaguzi mpya ufanyike haraka iwezekanavyo mambo yaishe, maalim naye aheshimu sheria aache mambo yake ya kujitangaza utafikiri yeye ndo ana mamlaka
Haya, sawa.Punguza hasira, jamaa hautumii umeme wa TANESCO anatumia wa sola!