Fedha ni "Bima" ya mapenzi??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fedha ni "Bima" ya mapenzi???

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by CPU, Mar 11, 2011.

 1. CPU

  CPU JF Gold Member

  #1
  Mar 11, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  WanaJF wenzangu

  Jaribu kumuuliza kijana wa sasa umri wa 20 hadi 35 bima yake ktk mapenzi ni nini?? Atawezaje kujiamini na kujihakikishia kuwa mpenzi aliyenaye hatamuacha???
  Nane kati ya vijana kumi watakwambia kuwa "bima" ni kuwa na uwezo wa kumudu mazingira ya maisha ya kisasa, kuwa na gari, kazi nzuri na sometimes hata nyumba yenye hadhi, kinyume na hapo hakuna "kinga" ya mapenzi.


  Inawezekana jambo hilo ni kweli, imeshawahi kutokea mara kadhaa mpenzi wa muuza mitumba pale Manzese Big Brother amechukuliwa na "kula kulala" mmoja wa Mikocheni eti tu kwa sababu tu "kula kulala" anaendesha gari la nyumbani kwao na anapesa kiasi za kutoka nae. Achana na hilo, pia inaweza kutokea kwamba mpenzi wa "kula kulala" kama huyo amechukuliwa na "*****" mmoja ambaye kutokana na "upambe" wake kwa watu maarufu wa mjini pesa mbili tatu hazimpigi chenga na hubadili "magari ya watu" kila mara.

  Katika hali kama hiyo mtu aliyeporwa au kuchukuliwa mpenzi wake hujihisi ana mapungufu na pengine mawazo yake yakamfanya ahisi kwa vile hana gari au pesa za kutosha basi nafasi yake ktk mapenzi haina uhai kama mdudu mbu!! Ajabu!!!

  Hii ni imani ya vijana wengi, wengi wanaamini kuwa uhalisia wa mapenzi ktk ulimwengu wa leo unakuja tu kwa mtu kujiweza kwa kila kitu, awe na pesa, gari, na pengine hata nyumba yenye hadhi ingawa itakuwa ya kupanga tu.

  Lakin udadisi wangu juu ya mahusiano ya kimapenzi nimegundua kwamba watu wengi wanaowaacha wapenzi wao na kwenda kwa wapenzi wengine kwa sababu ya pesa au vitu vingine vya anasa, maisha yao ya kimapenzi huishia kwa mwisho mbaya sana. (Sijui Jaffarai anafit hapa??). Huishia kujuta kwa sababu mara zote wale wanaowaacha wapenzi wao wa kweli na kufuata watu wenye uwezo na vishawishi vya vitu kama magari, pesa na muonekano wa kimwili hawapati mapenzi ya kweli mara nyingi huachwa ktk muda mfupi sana.


  Matokeo yake watu wa aina hii hujuta na kutaka kurejea kwa wapenzi wao wa zamani lakin bahati mbaya kwao hukuta zile nafasi walizoziacha zimeshajazwa na watu wengine wenye mapenzi ya kweli. Ni wachache sana wanaobahatika kupata nafasi ya pili, na hata hivyo nafasi hiyo hutolewa "kimachale" kwa sababu aliyeachwa mara ya kwanzahana imani tena na mwenzie. Ubaya wa kuachwa au kuingia kwenye mapenzi ya aina hii ni kwamba taratibu mwanamke au mwanaume mwenye kushawishika kirahisi hujikuta akiishi kwenye mapenzi yasiyo na msimamo na hapa ndipo anabatizwa majina kama "kicheche" na mengineyo

  Katika hali halisi mapenzi ya kweli hayaguswi wala wala kushawishiwa na vitu vya kuvutia bali yanajengwa na udhati wa hisia za mtu mmoja kwa mwingine bila kujali uwezo wa kukabili majukumu ya kawaida ya kimaisha.


  Samahanini sana kwa maelezo marefu, lakin nimelazimika kuyaandika hivi kama mchango wangu wa kuelimishana na kurudisha hadhi ya MMU iliyopotea.

  CPU
   
 2. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Una busara sana CPU....very good analysis....

  ila hapa .........Katika hali halisi mapenzi ya kweli hayaguswi wala wala kushawishiwa na vitu vya kuvutia bali yanajengwa na udhati wa hisia za mtu mmoja kwa mwingine bila kujali uwezo wa kukabili majukumu ya kawaida ya kimaisha.

  Hapo Blue kuna mtihani mgumu sana,sijui kama kuna mtu anataka kuwa na mtu asiye na uwezo wa kukabili majukumu ya kawaida ya maisha......it will be insane......!!


   
 3. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Umri nao unaplay part kubwa sana katika analysis yako bana sipiyuu. vijana zaidi wanachemka na kudhani kwamba kila kitu kinawezekana kirahisi tu. Uwezo wa kujiwekea malengo nao una nafasi yake kwa maana kwamba kama mtu yeye yupo yupo tu basi ni rahisi sana kuwa na muda wa kuanzisha mahusiano ya mapenzi kila mara kwa sababu hana majukumu ya kumtosha. Si unajua hizo love commitment ulizoainisha hapo zinahitaji muda na mtu kuwa honest
   
 4. CPU

  CPU JF Gold Member

  #4
  Mar 11, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  My dia

  Nadhani nifafanue kidogo hapo. Ni kwamba simaanishi usiwe na chochote kabisa, ila uwe na kile kianzio ambacho kitakusogeza mbele kimaisha. Mfano kwa wengine maisha ya kawaida ni kuwa na kazi ya kulipwa angalau mil 1.5, nyumba ya kupanga vyumba vi3, corola ya kutembelea n.k.
  Kwa wengine maisha ya kawaida ni kufanya biashara ya mitumba kariakoo, kuwa kondakta, n.k
   
 5. CPU

  CPU JF Gold Member

  #5
  Mar 11, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ni kweli mkuu, age sometimes ina matter.
  Hapo kwenye blue ni kweli kabisa, hasa kwa vijana wanaochipukia
   
 6. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Watu wanajidanganya na wanadanganyika haswa!Mtu anaeweka pesa mbele hakupendi wewe anaipenda pesa yako...kwahiyo ndio inaweza kutumika kama bima ila sio ya mapenzi ila ni ya kumweka mtu pale unapotaka!Mapenzi hayana bima...unachoweza kufanya ni kumfanya mwenzako azidi kukupenda na kutamani kua na wewe basi!
   
 7. CPU

  CPU JF Gold Member

  #7
  Mar 11, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Sure mamii
  Hapo kwenye redi hivyo vitamanishi ndio haswaa kila mtu anapaswa avijue
   
 8. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #8
  Mar 11, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Tatizo wanaume wengi wa sasa wapo kingono zaidi na ndio maana mabinti nao wanakuwa kipesa zaidi.
  Ila mapenzi ya kweli hayatokani na pesa ila pesa kidogo nayo iwepo ya kubadilisha juisi.. Lol!
   
 9. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #9
  Mar 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mmh we unavijua hubby?Au nijiandae kukimbia?
   
 10. CPU

  CPU JF Gold Member

  #10
  Mar 11, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Labda ukimbie kwa kuzidiwa na mahaba mazito . . . .
   
 11. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #11
  Mar 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Oh hubby embu nimegee kidogo!Alafu mbona mahaba siyaoni?
   
 12. CPU

  CPU JF Gold Member

  #12
  Mar 11, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Leo internet inanisumbua mpaka basi, sijui ndo tsunami
  Sasa Sweetie utaonaje mahaba wakati uko posted via mobile??
  Hata PM hupatikani, nashindwa niyapenyeze wapi haya mahaba unaone??!
  Halafu ujue mi nina wivu sana, nimeambiwa unamlilia Rev Masa kwa kupigwa ban
   
 13. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #13
  Mar 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hubby achana na maneno ya kuambiwa..unaonewa wivu we hujui tu!Mmh nipe hapahapa via mobile maana nna hamu ya kuyaona!
   
 14. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #14
  Mar 11, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Aiseee this is vere vere

  The Following User Say Thank You to Lizzy For This Useful Post:

  The Finest (Today) ​
   
 15. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #15
  Mar 11, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mkuu well said and well noted
   
 16. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #16
  Mar 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Fy yani wewe tu ndo umenigongea?Hata darli kanipita?
   
 17. CPU

  CPU JF Gold Member

  #17
  Mar 11, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kwa sababu kakuona uko via mobile ndo maana kaona rahisi kukudanganya
  Nilianza kukugongea yangu hata kabla hujamaliza kuandika, ikaja ya muhosni then ya mwisho ndio ya SHAROBARO
  ona mwenyewe, tena kagonga sasa hivi baada ya kuona aibu umerudi

  The Following 3 Users Say Thank You to Lizzy For This Useful Post:

  CPU (Today), muhosni (Today), The Finest (Today) ​
   
 18. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #18
  Mar 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hahaha asante hubby maana nlidhani naanza kusifiwa na mashem wakati mpenzi haoni kama nimetoka!Me is happy now!MWUAHHHH!
   
 19. tracy

  tracy JF-Expert Member

  #19
  Mar 12, 2011
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Inahusu SPARK kwenye uhusiano,Pesa sio bima..inategemea pia na utashi na uelewa wa mtu..
  Kuna mtu amekuzwa kwenye maisha ya kuona pesa ndo kila kitu(too much of fantasies)iwe mwanaume au mwanamke,.Ye mwanaume ataona kwa pesa zake atapata mwanamke yeyote na mwanamke anaeza kupata mwanaume yeyote au mwenye pesa.
  Kama mwanamke atashindwa kujua capabilities zake na kujua kua hata yeye ana role kwenye hizo pesa then PESA itakua ndo bima kwenye mahusiano yake,sio tu kwa mwanaume but hata kwa marafiki wa kawaida ndo hapo tunawapata maGold digger and the like..atafanya chpochote aonekane,SIO KWA NGUVU ZAKE BALI KWA MGONGO WA MWINGINE!
  Wapo maskini lakini wana furaha ndani ya relationships zao and hawahitaji zaidi..
  Tusiwasahau wale walioumizwa sana kwenye relaitionships hadi wanaona bora kupata kimoja,either pesa or true love kuliko kukosa vyote,nao PESA ni bima kwao.
  So it depends na mtu mwisho wa siku but i personally believe on the SPARK!what new things you do for each other and the depths you two go just to make each other happy,having a mutual feeling that makes your bond stronger kila siku..
   
Loading...