Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,221
- 2,425
Unajua app ya message uliyonayo inaweza kufanya jambo zaidi ya unavyofikiria kabisa ? Kuna mambo mengi ya siri unaweza kuyafanya kwenye app yako ya Message ambayo hukutegemea kabisa.
5️⃣ Message schedule
Hivi unajua app ya Google message unaweza kuandika ujumbe na kuchagua ni muda gani mtu unayetaka kumtumia huweze kumfikia kwenye simu yake, ambapo app itaweza kutuma ujumbe automatiki bila wewe kubonyeza kitufe cha kutuma.
🚀 Fungua app ya message >> andika sms yako >> sehemu ya kutuma ishikirie kwa sekunde kadhaa utaona jedwali la schedule utachagua.
4️⃣ Pin message
Kuna wakati unataka kumtumia mtu ujumbe utakuta mpaka utafute kwenye sehemu ya ku search inaboa sana, sasa wewe Kwenye app ya Message Kuna jinsi ya ku pin message zako muhimu ziwe za mwanzo kuonekana kila unapofungua app ya message.
Unachotakiwa kufanya ni kwenye app ya message>> chagua message unayotaka ku pin >> shikiria >kisha chagua alama hii 📍 Utaweza ku pin message yoyote.
3️⃣ Zuia Message za Utapeli
Hii ni njia Rahisi ya kuweza kukulinda dhidi ya message za Utapeli kwenye simu yako kwa kuweza kuweka on Feature ya spam protection , Google itakusaidia kukulinda dhidi ya message yoyote ya Utapeli kwenye simu.
Fungua app ya message>> settings>> kisha spam protection & safety weka On.
2️⃣ Chagua kila namba itumie sounds notification yake
Hii ni feature ya kuweza kuchagua sound notification ya kila namba ya simu uliyonayo kwenye simu yako kwa kuweza kujua mlio fulani unajua ni namba ya mtu fulani kupitia app ya message.
Fungua message ya mtu unayochati naye>> juu chagua jina lake>> chagua notification>> sehemu ya sounds chagua sound gani unahitaji kila ujumbe Toka kwa mtu wako ukija uwe unasikia.
1️⃣ Rcs chat
Inaitwa Rich communication service (Rcs) inakupa uwezo wa kuweza kutuma picha, video, emoji, files Toka simu moja kwenye nyingine kwa njia ya Message, kikubwa zaidi feature hii lazima u enable kwanza ndo ifanye kazi kwenye simu yako.
Ingia settings kwenye Message kisha >> General>> Rcs weka on enjoy Google message kwenye simu yako.