FC Lupopo wawashitaki Yanga TFF

kovai tamil taiga

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2013
Posts
1,571
Reaction score
2,192
FC Lupopo yadai Yanga imewadhulumu fedha kwa usajili wa Twite.Yanga walitakiwa kulipa dola 15, 000 kama wamemuongezea mkataba Twite lakini hawakufanya hivyo!
"Tutasonga mbele hadi FIFA".
Dawa ya deni ni kulipa tu!!
 
Najua Manji mda huu atakuwa anajuta, kwanini alikubali wanachama wamuongezee mwaka mmoja wa kuwa madarakani.
 
Huyu mh Manji wakati mwingine ni ngumu kuelewa utajiri wake! Pesa ya kulipa madeni kama haya ya Twite ni shida!alitakiwa kumalizia pesa ya usajili wa Okwi, hakufanya hivyo.Suala uwanja pale kwenye maji jangwani kimya!Halafu anaibuka na kudai anaweza kulipia wachezaji wote Simba waende Coco beach kupiga danadana!Ipo siku wana Yanga mtastuka na kuacha kumpigia MAGOTI huyu mheshimiwa!
 
Ile dhambi ya kumgeuza aden rage mtoto mdogo wakati aliishamalizana na mbuyu twite akiwa rwanda halafu yanga wakafanya ujanja ujanja kwenda kumsaininsha kongo inawarudi sasa. Mlisharudisha pesa ya simba na sasa muwalipe na fc lupopo. Poleni sana yanga. Panapofuka moshi chini kuna moto sidhani kama kweli uongozi wa yanga kwa sasa ni kitu kimoja nahisi kuna mgawanyiko kati yao au mmoja anawaburuza.
 
Movie ya Okwi haijaisha utamu,Movie nyingine mpya inaingizwa sokoni ,daah kazi ipo...
 
Nachotaka kujua hawa Lupopo walitoa ITC au hawakutoa? na kama walitoa wao kwann walikubali mkopo?akili yao ni kama ya RAGE.
 
by MKALIKENYA;
Nachotaka kujua hawa Lupopo walitoa ITC au hawakutoa? na kama walitoa wao kwann walikubali mkopo?akili yao ni kama ya RAGE.



Wewe MKALIKENYA Uwe unasoma na kuelewa!

ITC wametoa ila kwenye mkataba wao ni kuwa kila mbuyu twite anaposaini mkataba mpya na yanga lazima walipwe hicho kiwango, au mbuyu anapouzwa sehem nyingi pia walipwe kiasi hicho dola 15000/ nn usichoelewa hapo?
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…