FC Lupopo kutua kesho

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
266
MSAFARA wa nyota 19 na viongozi watano wa mabingwa wa soka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, FC Lupopo, unatarajiwa kutua nchini kesho tayari kuivaa Yanga katika mechi ya hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu, wageni wao watawasili kwa ajili ya mechi hiyo itakayopigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Sendeu alisema kocha Kostadin Papic, anaendelea kuwanoa vijana wake ili kuvuna ushindi katika mechi hiyo ya kwanza kabla ya kurudiana wiki mbili baadaye nchini DRC.

Alisema kwa lengo la kukusanya nguvu, wenyeviti na makatibu wa matawi ya klabu hiyo kwa Mkoa wa Dar es Salaam, watakutana leo kujadili maaandalizi ya mechi hiyo na marekebisho ya katiba.

Sendeu alisema mkutano huo utafanyika makao makuu ya klabu hiyo ambayo jana iliingia mkataba rasmi wa mwaka mmoja na Kampuni ya African Medical Investment, inayomiliki Hospitali ya Trauma.

Akizungumza katika hafla fupi ya utilianaji saini mkataba huo iliyofanyika makao makuu ya klabu hiyo makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Mwenyekiti wa Yanga, Iman Madega, aliishukuru

kampuni hiyo kwa niaba ya wanachama wa Yanga kwani wachezaji wao watakuwa wakipatiwa matibabu.

Alisema chini ya mkataba huo, Yanga itaokoa fedha nyingi zilizokuwa zikitumiwa kwa ajili ya kuwatibu wachezaji.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom