lil wayne
JF-Expert Member
- Apr 15, 2016
- 992
- 904
Katika kipindi cha msimu wa mechi za klabu bingwa barani Ulaya kumetokea na Jambo ambalo lilikuwa likizungumzwa sana . Hasa katika mechi mbali mbali za klabu ya Barcelona ya Uhispania, yenye makazi yake jiji Barcelona .
Jambo la klabu ya Barcelona kusemekana kupendelewa katika maamuzi ya muamuzi wa Mechi . Katika kipindi kilichopita Barca imekutana na Timu kama Atletico Madrid kwenye Ligi na kwenye muchuano ya Klabu bingwa, Imekuwa ikisemekana kuwa Barca imekuwa ikibebwa sana. Mimi pia (kimakosa bila hata kutafakari) nimekuwa nikiunga mkono hili suala..
Ninekuwa nikiandika sana kuhusu Barca kupendelewa katika Mechi kubwa.
Baada ya kutafakari kwa Kina ,nimekuja kugundua kuwa "Ubora unadhihirisha Makosa". Nimegundua kuwa Barca si kweli kwamba wanapendelewa bali ni aina ya soka wanalocheza lina ubora wa kiasi kwamba ni rahisi sana kwa makosa ya mpinzani wako kuonekana.
Vivyo hivyo Ubora huo unajionyesha kwenye klabu ya Dar es salaam Young Africans SC.
Nimekuwa nikitazama mechi za hii klabu Young Africa na kuanza kuamini kuwa lawama zinazoikumba klabu hii sio sahihi. Wengi wamekuwa wakidhani Young Africans SC imekuwa ikibebwa, la hasha wala si kweli. Hili swala lilinifanya nilinganishe ubora wa vilabu hivi 2 na kufikia muafaka kuwa Ubora wa hali ya juu wa hivi vilabu viwili kwenye ligi zao unavifanya vionekane kuwa vinapendelewa.
Naomba sana Klabu ya Barcelona ya nchini uhispania iniwie radhi kwa kuwafikiria tofauti na ukweli ulio halisi.
Nilikuja kujifunza kuwa unajifunza kirahisi sana kupitia Mazingira yanayo kuzunguka kabla ya fundisho la mbali.