FBI wakabidhi nyaraka 30,000 za Clinton Bungeni

FBI wakabidhi nyaraka 30,000 za Clinton Bungeni

Malcolm X5

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2013
Posts
1,643
Reaction score
2,769
Anatuhumiwa kutumia anuani yake binafsi kwa mawasiliano ya shughuli za Serikali,
Washington,marekani.Nyaraka za shirika la upelelezi la marekani (FBI) Kuhusu uchunguzi unaomhusu mgombea urais kupitia chama cha Democratic,Hillary clinton zinapitiwa upya kwenye jengo la bunge la nchi hiyo.

FBI walikabidhi majalada yenye nyaraka hizo juzi na ndani yake kuna barua kadhaa ambazo zinadaiwa kuandikwa na clinton,akitumia anuani yake binafsi ya barua pepe,wakati huo akiwa waziri wa mambo ya nje.

Wajumbe wa republican waliomba kupewa majalada hayo,baaada ya FBI Kusema kuwa hawana sababu ya kumfungulia mashtaka ya kukiuka itifaki ya mawasiliano,mgombe huyo urais anayewania kumrithi Rais Barrack Obama.
Matumizi ya anwani yake binafsi kwa mawasiliano ya kiofisi,yamekuwa silaha kubwa iliyotumiwa na wapinzani wake wa kisiasa.

Machi 14,2012 mjini washington,clinton alipata barua pepe kutoka shirika la ujasusi la marekani(CIA) ikiwa na kichwa cha habari,siri ikitokea kwa mnadhimu mkuu wa shirika hilo,Dave petraeus.

Ujumbe huu ni miongoni mwa zaidi ya baruapepe 30,000,pamoja na nyaraka nyingine zilizowekwa hadharani na CIA.

Aidha,ni moja ya maelfu ya ujumbe zilizowekwa alama ya SIRI ambazo kwa sasa zinafanyiwa uchunguzi,hatua inayoweza kufifisha ndoto za Hillary clinton za kushinda kinyang'anyiro hicho cha urais.

Barua pepe zilizotoka shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) ni miongoni mwa nyingine 65,zilizowekwa nembo ya siri,ambazo pia hazikuhaririwa kwa umakini.CIA ilisema kuzuiwa kwa baadhi ya barua pepe kulihusiana na sababu za kiusalama wa taifa.

Kuwekwa hadharani kwa baruapepe alizotuma na alizozipokea Clinton kati ya mwaka 2009 na 2013 ,kulisababisha FBI kuanzisha uchunguzi kuanzisha uchunguzi na kuanza kuwahoji watu wa karibu zaidi na mwanasiasa huyo ambaye anapewa nafasi kubwa ya kuwa Rais wa marekani

Chanzo: Mwananchi
 
Kumekucha mambo gani tena haya ya kuharibiana wakati huu bibi wa watu anakaribia kuukwaa urais
 
Hawa wagombea wote marekani wamepunguza kabisa uhalali wa kuwa wagombea wa vyama vyao,wote wana migogoro.
 
Trump anabeba kombe huku akicheka kwa dharau huyu mama anajutia sana kwanini alifanya ujinga huu ila ndo ishakuwa..na mmarekani huwa hataki ucheze na usalama wa nchi yake
 
Marekani hadi raha kila sector inasimama kivyake haiwezi kuingiliwa na nguvu ya rais! Ingekuwa ni hapa kwetu du! Polis huko hawaengemei upande wowote wapo kwaajili ya maslai ya nchi! Hapa kwetu wapo kwaajili ya maslai ya ccm na watu binafsi
 
Marekani hadi raha kila sector inasimama kivyake haiwezi kuingiliwa na nguvu ya rais! Ingekuwa ni hapa kwetu du! Polis huko hawaengemei upande wowote wapo kwaajili ya maslai ya nchi! Hapa kwetu wapo kwaajili ya maslai ya ccm na watu binafsi
Kweli mkuu,huwezi andaa mkuu wa nchi hamjui kwanini anaficha hata mails zake,ila nimeona leo kumbe waziri wa ulinzi enzi hizo,collin powel aliruhusu yeye kufanya hivyo,kajitetea,hilary clinton.
 
Back
Top Bottom