Fastjet kupunguza wafanyakazi

Fastjet kupunguza wafanyakazi

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
KAMPUNI ya ndege ya FASTJET Tanzania ina mpango ya kupunguza wafanyakazi wake katika viwanja vya ndege vya Mwanza na Kilimanjaro.

Barua iliyosambazwa hivi karibuni na wafanyakazi wa kampuni hiyo iliyoandikwa na Mkuu wa Operesheni za ardhini wa Fastjet, Tanzania Dickson Kunambi, ilisema kuwa"Ninaamini tunaweza kukutana wakati fulani kwa sababu bado mna mali za kampuni mnazotakiwa kuzirejesha. Labda kama mmeamua kubaki nazo bila kampuni kujua, vitu kama vitambulisho, funguo na makabrasha yoyote ya kampuni."

Hatua hiyo ya hivi karibuni inaleta maswali zaidi juu ya mustakabali wa kampuni hiyo yenye mchango mkubwa kwenye uchumi tangu ilipoanzisha huduma zake miezi michache iliyopita.

"Hatuwatarajii ninyi kufanya kazi za kawaida katika viwanja hivi vya ndege kwa sababu tayari mmeshaarifiwa kuhusu kupunguzwa katika mikutano na tayari mchakato huo unaendelea," alisema Kunambi kupitia barua hiyo.

Mmoja wa wafanyakazi alimuuliza mkuu huyo wa operesheni katika barua pepe kuwa"Mtaendeleaje kutujali sisi katika kipindi hiki? Je, sisi bado ni wafanyakazi wa Fastjet au? Kwa sababu tangu ulipokuja na uamuzi wakati wa mkutano wetu wa mwisho Dar, sidhani kuna kitu chochote tunaweza kukaa na kujadili na kukamilisha kwa wakati huu. Kwa hiyo kinachotakiwa hapa ni kampuni kufanya mpango wa haki."

Mmoja wa wafanyakazi ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema haikuwa halali wao kupunguzwa wakati biashara ndiyo ilikuwa imeboreka zaidi.

"Tumekuwa tukifanya kazi katika masharti magumu sana tukijua kwamba kampuni itatuongezea malipo wakati mambo yakiwa mazuri, lakini kilichotokea kinakera sana," alisema.

Alipopigiwa simu kuzungumzia tuhuma hizo, Kunambi alisema alikuwa anafahamu mchakato huo ulikuwa unaendelea, lakini hakuweza kuelewa ni jinsi gani habari hizo za ndani zimeweza kuvuja.

"Ulipataje hizi habari? Haya ni mambo ya ndani ya kampuni na bado tunaendelea na mchakato. Hata hivyo mimi si msemaji wa kampuni. Unaweza kuwasiliana na kitengo cha rasilimali watu," alisema.

Alipobanwa kutaja sababu za kampuni kupunguza wafanyakazi na idadi yao wakati inafanya vizuri katika biashara zake Kunambi alisema ni kitengo cha rasilimali watu ndicho kinafahamu idadi.
 
Nauli buku 30, alafu mnategemea mshahara mzuri?

Asikudanganye mtu wala usidanganywe na matangazo ya tv na magazeti. Hakuna nauli kama hiyo kokote kwenye kampuni hii. Nenda nayo hiyo buku 30 uone kama utapata tiketi hata kama utafanya booking miaka mitatu kabla.

Well nauli yao iko chini kuliko PA lakini siyo kama ina yotangazwa. Mza- dar 150 k kama sikosei then 15k za mzigo, jumla ni ngapi? Chezea matangazo wewe!!!!
 
Majanga hayo mana Precision nao watapunguza wafanyakazi 200 mwezi october mwaka huu.
 
wapunguze na ndege zao pia maana zinaleta traffic sana angani tukiwa kwenye mambo yetu ya kamati ya ufundi
 
Majanga hayo mana Precision nao watapunguza wafanyakazi 200 mwezi october mwaka huu.

Sasa hawa afadhali wapunguze maana Mbuko alikuwa ananisumbua sana najua sasa ntambandua kirahisi maana atakuwa majalala na hivi tunaenelke mwisho wa mwaka lazima atataka kwenda moshi tu...ndo hapo hapo nampakaza gundi...kudadadeki
 
Hahah,,,gundi yaMayonisse au?
 
dah! 200? Mbona wengi Mungu wangu,ss hao wote wanaenda wapi?
..ndo mwanzo wakurogana ili kubaki kazini
 
Sasa hawa afadhali wapunguze maana Mbuko alikuwa ananisumbua sana najua sasa ntambandua kirahisi maana atakuwa majalala na hivi tunaenelke mwisho wa mwaka lazima atataka kwenda moshi tu...ndo hapo hapo nampakaza gundi...kudadadeki
Gundi tena!!!!!!!daa, teh,teh,teh,teh.
kazi kweli kweli wadada mna kazi kila wakati ni kuwindwa tu kama chita na swala mbugani.
 
Sasa hawa afadhali wapunguze maana Mbuko alikuwa ananisumbua sana najua sasa ntambandua kirahisi maana atakuwa majalala na hivi tunaenelke mwisho wa mwaka lazima atataka kwenda moshi tu...ndo hapo hapo nampakaza gundi...kudadadeki

teh teh nimecheka sana yaani unamuombea mabaya ili umbandue, mpe kauli thabiti utambandua tu na hiyo hela na wewe utaila sio usubiri mpaka awe majalala
 
dah si waondoke kabisa maana kuna wengine tunapigiwa naomba nauli ya 32,000 kama tunafanya fastjet lohANYWAY MSIWAZE SANA KWA WANAOJUA AIRLINE HAYA NI MAMBO YA KAWAIDA KAMPUNI MOJA YA NDEGE YA TANZANIAA IJIITAYO NATION CARRIER ILIPUNGUZA WATU 150 KAMA SIKOSEI LAKINI ALIPOINGIA BOSI MMOJA ANAJIITA CHIIZI AKAAJIRI 90 MPAKA ANAFUKUZWA BAADA YA HAPO AKALETWA MWINGINE SIKUMBUKI JINA NAE KAAJIRI KAMA 45 HIVI SO NI SWALA LA AKUPANDA NA KUSHUKA NA NYIE MNAOPEWA CHENU MTUKUMBUKE WACHUNGAJI KWENYE ZAKA VINGINEVYO KAMPUNI IKIKUA INAITA WENGINE NA KUWASAHAU
 
gundi tena!!!!!!!daa, teh,teh,teh,teh.
Kazi kweli kweli wadada mna kazi kila wakati ni kuwindwa tu kama chita na swala mbugani.
mpwa asiwkambie mtu fastjet mabinti wamelambwa mabinti wameolewa loh!!!mpaka haya naificha mwenyewe
 
dah si waondoke kabisa maana kuna wengine tunapigiwa naomba nauli ya 32,000 kama tunafanya fastjet lohANYWAY MSIWAZE SANA KWA WANAOJUA AIRLINE HAYA NI MAMBO YA KAWAIDA KAMPUNI MOJA YA NDEGE YA TANZANIAA IJIITAYO NATION CARRIER ILIPUNGUZA WATU 150 KAMA SIKOSEI LAKINI ALIPOINGIA BOSI MMOJA ANAJIITA CHIIZI AKAAJIRI 90 MPAKA ANAFUKUZWA BAADA YA HAPO AKALETWA MWINGINE SIKUMBUKI JINA NAE KAAJIRI KAMA 45 HIVI SO NI SWALA LA AKUPANDA NA KUSHUKA NA NYIE MNAOPEWA CHENU MTUKUMBUKE WACHUNGAJI KWENYE ZAKA VINGINEVYO KAMPUNI IKIKUA INAITA WENGINE NA KUWASAHAU
Kupanda na kushuka au kupanda na kuvuna daaa!!!kama DEC vile.
 
Dickson kunambi uyu jamaa itakuwa ni special kwaajili ya kupunguza watu makampuni yakitaka kufanya ivyo
 
Back
Top Bottom