FastJet is way too expensive

FastJet is way too expensive

SIRI NI HII:
Ukifanya booking online kwa kutumia online especialy simu, bei inaongezeka kuliko ile bei yao halisi. mfano kiwango chao cha nauli ya juu zaidi kwa domestic flight ni 324000 lakini unaweza kuta kwenye online especially simu inaonyesha 487000, na ukichukua PNR hiyohiyo ukaenda kuuliza ofisin kwao unaambiwa inqinyesha laki mbili na kitu au laki tatu na kidogo. (Hapa nahisi kuna mchezo unachezwa) na ukilipia M.Pesa au Tigopesa basi ujue imekula kwako. Nikija kujaribu kwenye PC kidogo naona kuna afadhali, sijajua kuna tatizo gani mpaka iwe hivyo.
1. Inabidi waweke wazi nauli hizi kama wanapata hasara na wameamua kupandisha tujue
2. Precision wana bei rahisi pia hasa kwa safari za Kilimanjaro na Arusha hata z.bar pia.

CC: Uswe Kigogo Njalamatata gesselle
 
Last edited by a moderator:
SIRI
2. Precision wana bei rahisi pia hasa kwa safari za Kilimanjaro na Arusha hata z.bar pia.

CC: Uswe Kigogo Njalamatata gesselle

i agree, nimejaribu siku tofauti tofauti nipate a bargain price nyingi naona PW wana ticket poa kuliko FJ

Nakubaliana nawe kwamba FJ wameongeza bei, hasa kwa route ya kilimanjaro.

TIP:
PW wakati unabook, changua BY BEST FARE!
 
What I don't understand is you using all that energy defending Precision Airways on this ticketing prices. Naona hao PW wamekutuma humu uwatengenezee PR. Thank God FJ brought the competition on the Table. Tuachie tuchague wenyewe!!

Kingdom_man ni uvivu wa kufikiri kumshutumu mtu bila hata kufanya ka-uchunguzi kafupi, wakati ule nafuu wanaanza nilianzisha uzi wa kuwasifia, ilikua bei rahisi, hawa-cancel route hovyo hovyo kama PW na pia kwa sababu ndege zao ni kubwa, hutumia muda mchache angani, wakati ule nilitumwa na FastJet?

Toka kipindi hicho FJ imekua chaguo langu, hadi nilipogundua naweza kupata ticket kwa laki moja pungufu kutoka precision.

Sasa hapa ni wewe kuchagua, ulipe 100 zaidi au ukubalianena ukweli PW inaruka kwa mrefu zaidi na chances za kuhairisha route ni kubwa zaidi kuliko FJ....kwa mimi nimeona nisave hiyo laki na elfu tano.
 
Mpaka asubuhi hii nimelipia 51200 +13200=64400 online,hebu angalia vizuri

basi kuna kitu, nisaidie hivi viwili

1. ulibook online au ulienda kwa agent?
2. umebook kwa tarehe ngapi, i mean unasafiri lini?
 
Si kweli. fastjet wako cheap sana ukilinganisha na Mashirika mengine ya ndege nchini kikubwa ni kufanya bookinng yako mapema ni kweli unaweza ukawa hukupata nauli ya elfu 32,000 kwa mwezi wa kwanza lakini kama unakumbuka mwezi Novemba fastjet walikuwa na punguzo kubwa la bei ambapo waliuza tiketi kwa bei ya tsh 32,000 tiketi hi9zo walitakiwa wazisafirie mwezi wa kwanza hadi wa tatu sasa nadhani unaweza kuona kuwa kuna wateja walinunua tiketi kwa bei hiyo ya 32,000 siku nyingi na wanazitumia sasa. Jitahidi kufanya booking maema na utapata nauli ya bei ya chini.
 
Jitahidi kufanya booking maema na utapata nauli ya bei ya chini.

mapema kiasi gani Lucy? maana hata ukibook miezi miwili mbelebei inaanzia 67300 bila kodi, ukiweka kodi inakuwa 76,000

note: hii ni kwa DAR - KIA
 
Kwakweli fast jet sazingine wanagharama kuliko Precision. Mie nilienda kubook kwenda kia ni 325000 one way,nikasema ngoja nipite precision nikapata kwa 20000.

Mmh, huyu atakua amebook ile Bajaji ya PW ya kusambaza barua!

cc stineriga
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom