Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,499
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) mkoa wa Kagera, Faris Buruhani, amesema chama hicho kitaendelea kubaki madarakani na hakitotoka kamwe.
Akizungumza Februari 14, 2026 wakati akihojiwa na Chief Odemba kupitia kipindi cha Medani Kuu, Buruhani amesema, “Hata iweje CCM haitatoka madarakani hadi mwisho wa dunia. CCM haijatoka madarakani, haitatoka madarakani, na hata ikibidi milele CCM itaendelea kuwa madarakani.”
Aliongeza kuwa hatimiliki ya nchi ni ya Watanzania wote, lakini akasisitiza kuwa chama hicho kimebeba historia, hadhi na heshima ya taifa pamoja na waasisi wake. “CCM kimejipanga kimuundo, ndiyo maana nasema hakitaondoka leo, hakitaondoka kesho, na hata ikibidi milele hakitaondoka,”