Faraja yako weekend hii

Faraja yako weekend hii

Jozee mkunaji

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2017
Posts
459
Reaction score
614
• Baadhi ya watu wamechagua kutokua kwenye mahusiano kwa sababu wamechoka kuwa kwenye mahusiano ambayo wamejitoa kwa kila kitu lakini mwisho wa siku wameambulia maumivu. Mapenzi ya kweli yanatakiwa yawe ya 'kutoa na kupokea' yasiwe ni barabara ya manyanyaso na mauti.
_
• Baadhi ya watu wamechagua kuwa SINGLE sio kwa sababu hakuna watu wa kuwapenda tena, ila ni kwa sababu watu siku hizi ni wanafiki, wana mapenzi ya uongo, badala ya kukutengeneza uwe mtu mzuri, wao hukubadilisha kuwa mtu mbaya!
_
• Baadhi ya watu wako SINGLE na Alone, lakini hawako wapweke, kwa sababu wamechoka kuwa na watu ambao wapo nao kwenye mahusiano lakini ni wapweke zaidi kuliko wakiwa wenyewe.
_
• Baadhi ya watu wako SINGLE sio kwa sababu hawataki tena kuingia kwenye mahusiano, ila wanajifunza kuwa watu wazuri zaidi, ili watakapoingia kwenye mahusiano tena, yawe mazuri zaidi tofauti na yale ya mwanzo.
_
• Kuwa SINGLE haimaanishi umepoteza nafasi au hakuna anayekupenda, ila ni kuwa na nafasi ya kujijenga kiakili na kuwa mtu bora zaidi, ili baadae utakapoingia katika mahusiano mengine, mpenzi wako akupende zaidi na afurahie kuwa na wewe.
_
Ni bora zaidi kuwa SINGLE, kuliko kuwa katika mahusiano yaliyojaa maumivu kila siku. Siku yako inakuja. Kama nilivyokwisha kusema "Siku njema zaja upesi, tofauti na unavyofikiri, kuna majuto ktk kukurupuka, ila siku zote kuna manufaa katika kusubiri"

Inuka, inuka, inuka, utu wako una thamani sana tofauti na unayofanyiwa!

Better days are coming quicker than you think!!!

Nawatakia Weekend Njema, play safe, na Mwenyezi Mungu awabariki sana wikeñdi njema

Usilié tena. Kisa mapénzí
 
Asante kwa maneno yenye faraja angalau nimecheka kwa furaha ...
 
Back
Top Bottom