Faraja kwa wanaotafuta ajira na wahitimu wa elimu ya juu

Tape measure

JF-Expert Member
Nov 26, 2015
1,980
3,577
Je kuna faida zozote za mtu kuchelewa kupata AJIRA- Jibu ni Hapana.

Binafsi nmeshuhudia wahitimu wa vyuo vikuu, wakiwemo marafiki na watu wangu wa karibu wakishindwa kustahimili hali ya kuendelea kuwa tegemezi katika familia zao kwa kukosa kazi na kuishia kwenye makundi mabaya katika jamii mf. Ulevi, ushoga, umalaya, wizi, ugaidi na wengine kwa sasa tayari wamewehuka tayari.

NI MUHIMU KUTAMBUA YAFUATAYO
Nikisema UKWELI ni kweli na UWONGO kinyume chake naamanisha kuna ukweli

UKWELI
Kwa kawaida mtu anatafuta kazi ili aweze kumudu mahitaji yake na pengine kutimiza ndoto alizokuwa nazo kwa kipindi kirefu. sizani kama mtu akiwa na uwezo wa kupata kila anachokihitaji atahangaika pia kutafuta kazi.

UWONGO
Ni ngumu zaidi kujiajiri baada ya kukaa bila kazi kwa kipindi kirefu. Kutafuta kazi ni tatizo na jawabu lake sio la moja kwa moja/multidisciplinary answer.

UKWELI
Mwenye ajira ni rahisi sana kumshauri asiye nayo kjiajiri wakati unakuta pengine yeye binafsi ana miaka mingi kazini na hana kitega uchumi kingine chochote. .. Ni tatizo pia.

UWONGO
Kukataliwa katika kazi ni jambo la kawaida ukiwa na kazi lakini ni kama Bahati mbaya kwa anayeanza mfano graduate.

UKWELI
Habari njema ni kuwa kipindi unahangaika kutafuta kazi huwa unapitia shuruba na changamoto kadha wa kadha ambazo hugeuka kuwa faida kwako pindi upatapo kazi.

UWONGO
Wafanyakazi wengi wapo kama walivyo kutokana na njia walizotumia kufikia walipo.

UKWELI
Hakuna mtumishi anaezaliwa na tabia ya kutapanya ama kuheshimu pesa, haya yote hutengenezwa na uchu pamoja na jitihada zilizoambatana na mateso,huzuni,kuweweseka/depression pindi mtu anapokuwa anatafuta kazi.

UWONGO
Watu wengi waliopitia stage nyingi ngumu kufika walipopapigania kwa kipindi kirefu wana mafanikio kushinda wenzao.

UKWELI
Tunaposema kupata kazi ni kugumu hatumaanishi kazi hazipatikani, pia tatizo la ajira halipo Tanzania tu, hata nchi zilizoendelea kuna uhaba wa ajira. Tatizo la ajira Duniani ni ngumu kulitokomeza.
 
Kama kuna anaye kua shoga sababu amekua unemployed basi huyo alikua mpenda PIPE tangu zamani
 
Back
Top Bottom