Fao la kujitoa

sinide

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2015
Posts
459
Reaction score
486
Morning
Kuna thread nimeona humu ndani ya mtu anayejiita sijui ni mbunge akiongelea fao la kujitoa kwenye mifuko ya hifadhi za jamii.
Maelezo aliyotoa nmeona inabidi hawa viongozi wa kisiasa inabidi wachahuliwe endapo wana elimu ya kutosha japo sina uhakika kama huyo alojiita mbunge hajaenda shule ya kutosha.
Kimsingi waTanzania wengi ajira zao ni za mikataba mifupi endapo mtu atapata ajira ya miaka mi tano kiwa na miaka 25 atamaliza akiwa na miaka 30 kwahiyo mnataka huyo mtu asubiri miaka mingine 30 akiwa mtaani anapata taabu ndo apate pesa yake? Je kwa miaka yote hiyo pesa yake itakuwa na thamani ileile then kwa nini mtu apate shda wakati pesa yake iko mahali inafanya vitu visivyo msaidia yeye binafsi?
Swala lingine siku hizi hakuna mtu anataka kuzeeka akiwa ofisini watu tunatak tumalize tukiwa vijana ili tuchukue pesa zetu tukiwa na nguvu tuweze kufungua biashara zetu tukiwa bdo damu inachemka na akili ikiwa fresh
Hii itasidia sisi kuajiri vijana wenzetu waliokosa ajira vilevile kuachia nafasi tulizokuwa nazo huko maofisini ili vijana wanao maliza shule nao wapate ajira? Mnadhani kwa nn vjana wanalalamika kuhusu wazee kutoachia maofisi ili wao wapate ajira? Ni kutokana na huu ushenzi nothing else.
Tatzo la ajira liko dunia nzima na kila nchi inajitahid kutafuta mbinu ya kulitatua, je sisi tunafanya juhudi gani kulitatua kwa kutumia hii mifuko?
Nilitegemea mifuko hii pamoja na wanaoiongoza wahamasishe watu ambao wameshawekeza huko hela ya kutosha wazichukue wafanye biashara zitakazo ongeza ajira kwa waliokosa bali wao wanataka wakae nazo wafanyie ujinga wao usio na faida kwa raia na Taifa
Then hii mifuko inapata wapi mamlaka ya kumpangia mtu matumizi ya hela yake? Non sense
Kila siku mna hamasisha watu wajiajiri watajiajiri vipi wakati pesa za mtaji mnataka kuwapa wakiwa wazee au hamjui kwamba pesa ya mshaara inatosha kupanga nyumba na kulisha familia na hakuna zaidi ya hapo? Mbona nyie mkimaliza shughuli zenu za siasa mnapewa hela zenu zote? Au nyie ndo mnashda kuliko sisi? Asee naomba tuheshimiane ningetukana ila naogopa ban na siwez kaa bila kuchungulia kwenye haka kamtandao ketu pendwa nitakonda chap
NB: Endapo ntafata pesa yangu kabla ya huo uzee mnaotaka nyie haujanifika mjiandae kuleta chakula jela mana ntafanya tukio la kihistoria
 
Saizi ipite sheria umri wa kustaafu uwe miaka 50 ili wazee waondoke maofisini na vijana waingie. Kwa kufanya hivyo tutagawana vizuri keki ya taifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amin amin nakwambia wewe ni mmoja kati ya mamilioni ya wa TZ ambao tunaumia juu ya FAO hili la kujitoa. Na wengi wanautayari wa kufanya lolote ilimladi tu wenye mamlaka juu ya mifuko hii walirudishe eidha kwa kupenda au vyovyote vile. Naamini IPO cku atatokea wa kutuunganisha kupinga udharimu huu ambao hata wabunge wameshindwa kutusaidia. Na wahusika wasipolitazama kwa jicho pevu hawataamini macho yao. Gonga like hapa kama nawewe umeguswa na hili..
 
Sio wewe tu hata watumishi wa mifuko hii hawaelewi achilia mbali wanachama. Ni sheeeeeegdaah
Alotunga hiyo sheria ni serikali au mfuko? Af kwa nini wanatuamulia juu ya pesa zetu mi iko siku ntapita na mtu kwenye hizo ofisi zao, sisi kama wenye pesa mbona hatushirikishwi au hatuna haki juu ya pesa zetu
 
Saizi ipite sheria umri wa kustaafu uwe miaka 50 ili wazee waondoke maofisini na vijana waingie. Kwa kufanya hivyo tutagawana vizuri keki ya taifa.

Sent using Jamii Forums mobile app

serikali ikifanya hivyo itafilisi mifuko... why ?
kutunza wastaafu wa miaka 50 ni gharama kubwa...

maana wataishi miaka mingi .. mifuko unapenda watu wastaafu wazee ili waishi miaka michache tu.. pensheni isiliwe miaka mingi
 
Kwani huu mfuko au hii mifuko ni Mali ya nani? Kama sio sisi wanachama? Na kwa nini huyo nani aamue kile ambacho hatukitaki kwenye mifuko yetu?
Alotunga hiyo sheria ni serikali au mfuko? Af kwa nini wanatuamulia juu ya pesa zetu mi iko siku ntapita na mtu kwenye hizo ofisi zao, sisi kama wenye pesa mbona hatushirikishwi au hatuna haki juu ya pesa zetu
 
serikali ikifanya hivyo itafilisi mifuko... why ?
kutunza wastaafu wa miaka 50 ni gharama kubwa...

maana wataishi miaka mingi .. mifuko unapenda watu wastaafu wazee ili waishi miaka michache tu.. pensheni isiliwe miaka mingi
Kuna mstaafu anayetunzwa na serikali? Labda wa vyeo vya juu serikalini. Hawa wastaafu tunao wengi sana mitaani watunzwa na mizinga wanayotupiga... Sa sijui unaongelea wastaafu gani chief?
 
Mimi nadhani kuna haja ya sisi wanachama kuwa na uamuzi mkubwa kwenye hii mifuko kuliko serikali au Mfuko wenyewe. Kuondoa hii adha ya kuamuliana juu ya jasho lako mwenyewe. Wanasheria hebu jaribuni kukupa mwanga tunaweza fanya nini hapo ili wanachama tuwe na sauti na pesa zetu kuliko hiyo SSRA au Mfuko wenyewe.
 
Kwani huu mfuko au hii mifuko ni Mali ya nani? Kama sio sisi wanachama? Na kwa nini huyo nani aamue kile ambacho hatukitaki kwenye mifuko yetu?
Mi binafsi sioni umuhimu wa hii mifuko kama wanachama hawana maamuzi na uhuru juu ya pesa tunazowekeza
 
serikali ikifanya hivyo itafilisi mifuko... why ?
kutunza wastaafu wa miaka 50 ni gharama kubwa...

maana wataishi miaka mingi .. mifuko unapenda watu wastaafu wazee ili waishi miaka michache tu.. pensheni isiliwe miaka mingi
Hivi we uko timamu kabisa alokwambia kuns mstaafu anatunzwa au anahitaj kutunzwa na serikali ni nani? Kwa nn mtu akimaliza kaz asipewe hela yake yote apite kushoto afate maisha yake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…