Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,768
- 49,940
Nyumbani Tanzania, malalamiko yamekuwa mengi kuhusiana na kupanda sana kwa bei ya chakula. Wengine wakiilaumu Serikali kuwa haikuchukua jitihada za kutosha ili kuzuia mfumko wa bei ya chakula.
Mimi si mtetezi wa Serikali, sijawahi kuwa na sitakuwa. Nafurahia uhuru wangu unaozingatia ukweli kuliko kumfurahisha mtu au kikundi cha watu.
Ukweli ni kwamba, mchanganyiko wa mambo, kuanzia Covid 19, vita vya Ukraine, bei kubwa ya mafuta, matatizo ya hali ya hewa na ongezeko kubwa la watu hasa kwa mataifa masikini na yanayoendelea, vyote kwa pamoja, vimechangia sana kupanda kwa bei ya chakula na bidhaa nyingine.
Mfumko huu wa bei ni janga lakini lenye fursa kubwa ndani yake. Ni janga kubwa kwa nchi ambazo hazina ardhi nzuri ya kilimo, hazina maji ya kutosha, hazina maeneo makubwa yenye ardhi nzuri, hazina utulivu wala amani (nchi kama Ukraine), lakini ni fursa nzuri sana kwa nchi kama Tanzania. Nchi ambayo ina eneo kubwa, ardhi nzuri ya kilimo, hali ya hewa nzuri inayoruhusu ustawi wa mazao, maji mengi kila kona, watu wengi wanaozurula na vinguo vichache mabegani, mazingira rahisi ya usafirishaji.
Serikali iwekeze kwa kiwango kikubwa kwenye kilimo. Wanannchi wa kawaida na wawekezaji, twende tukawekeze kwenye kilimo. Tatizo la upungufu wa chakula haliishi leo wala kesho. Leo nipo Njombe kwenye uwekezaji, angalao kwa kuanzia nilime ekari 200, lakini ikiwezekana nilime ekari 600 zote za shamba nililolipata.
Serikali iendelee kuachia uhuru kwa wakulima kuuza mazao mahali popote ili kujenga mazingira ya wengi kwenda kuwekeza kwenye kilimo. Bei nzuri ya mazao itavutia wengi kuwekeza kwenye kilimo. Serikali, ihamasishe sana uuzaji wa mazao yetu nje ya Taifa letu ili pesa ya mataifa hayo ije nchini mwetu, iongeze mzunguko wa fedha, iongeze akiba ya pesa ya kigeni, iinue hali za wananchi wa vijijini ambao kimsingi ndio wakulima.
World food prices hit record high in 2022
World food prices dropped for a ninth month in December, but hit their highest level on record for the full year in 2022, United Nations data found.
Food prices rose to a monthly record high in March after Russia invaded Ukraine, a significant worldwide wheat and cooking oil supplier.
A grain deal brokered by Turkey and the UN in July lifted a Russian naval blockade on Ukrainian exports.
The Food and Agriculture Organisation said its price index, tracking the monthly change in international food commodities, saw a 1.9 percent drop from November.
It was also 1 percent lower than in December 2021.
But the index was 14.3 percent higher overall in 2022 compared with the previous year as it reached an all-time high of 143.7 points.