Hussein Massanza
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 1,016
- 2,195
Ujumbe mzuri kwa wanaoamini na wasioamini.
Great message to believers and Non-believers.
===========
Chorus!
Fanya Hisab Kamili
Upime zako Amali
Upatalo ndilo kweli
Amua Mwenye Akili
Verse
Mja Fanya Hisabu,
Upate yako Majibu,
Muovu yake Adhabu,
Motoni Ataingia,
Safisha Chako Kitabu,
Kwa mola uwe karibu,
Adhabu yake Wahabu,
Huwezi kuvumilia
*Repeat Chorus*
Kibwagizo
Mwanadamu Tafakari
"Fanya Hisab"
Juwa kuna Dafutari
"Fanya Hisab"
Yanaandikwa ya Kheri
"Fanya Hisab"
Huandikwa na ya shari
"Fanya Hisab"
Pumzi zitakatika
Hesabu zimachafuka
Ubaki kuhuzunika
Umri umeuchezea
*Repeat Chorus*