The Consult
JF-Expert Member
- Jan 20, 2017
- 220
- 252
Biashara ya samani (furniture industry) ni biashara inayokua kwa kasi, na imekuwa ikinyooshewa kidole kama ni njia muhimu (important tool) katika kufikia uchumi wa viwanda ambao ni lengo la Mpango wa miaka mitano (Five Year Development Plan) 2015/2020). Kutokana na kuonekana umuhimu wake; bado juhudi za makusudi hazijafanywa kuhakiksha ukuaji wa biashara hii.
Utekelezaji/ufanyaji wa biashara hii kwa mazingira ya Tanzania unakutana na vikwazo mbalimbali. Vipo vikwazo ambavyo hutokana na mazingira ya nje (Business challenges), ambayo mfanyabiashara hana uwezo wa kuyadhibiti, pia vipo vikwazo vinavyosababishwa na mfanyabiashara mwenyewe (Operations Weakness/Poor Business Management)
Kabla ya kuendelea mbele; ni vyema tukajua maana ya biashara ya samani (Funiture Industry); hii inatafsiriwa kama mkusanyiko wa viwanda/makampuni yanayojishughulisha na kubuni (design), kutengeneza (manufacturing), kusambaza (distribution) na kuuza (selling) samani za ndani kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na maofisini pia.
Bidhaa za samani hujumuisha viti (chairs, sofas, stools), vitanda (beds), madawati (desks), makabati (cupboards, shelves) na nyingine nyingi.
Makampuni yanayojihusisha katika biashara hii ni pamoja na Elegance Furniture Limited, City Furniture, Classic Furniture Limited n.k
Pia kwa Dar es Salaam; biashara hii inafanyika kikanda (in clusters),kanda maarufu (clusters) inajumuisha Keko, Bugurunu-Malapa na Mbezi Beach kwa Komba.
Tukianza na changamoto zinazoikabili biashara hii, zinajumuisha;
- Ukosefu wa wafanyakazi wenye ujuzi stahiki (skilled labors)
- Ukosefu/kutozingatia umuhimu wa huduma ya ushauri wa kitaalamu (Consultancy services)
- Ukosefu wa malighafi zenye ubora hususani mbao.
- Ukosefu wa technolojia stahiki.
- Na nyingine nyingi.
- Eneo la biashara (hususani show rooms); hakikisha unachagua eneo zuri, maeneo pendekezwa ni jirani na makazi (residential areas) jirani na maeneo ya manunuzi (shopping centres/malls). Pia ni vyema ukazingatia huduma ya usalama na wepesi katika usafiri pindi ujaguapo eneo
- Tumia pschographic katika ku-segment wateja wako; hii ni science ya kutumia saikolojia na watu (demography) katika kuwaelewa wateja wako. Kwa kutumia science hii; utaweza kuwagawa wateja wako kutokana na mitindo yao ya maisha (life styles), utu wao (personality) na uthamani wao (value). Hivyo ubunifu wa samani zako unapaswa kuakisi sifa hizi za wateja wako.
- Gawa eneo lako la biashara katika "zones" hii itakurahisishia katika utendaji na hakikisha kila "zone" inakuwa na msambazaji anaejitegemea (Independent distributor)
- Kuwa na utaratibu wa kudhamini (sponsoring) matukio ya kijamii ambayo hukusanya watu mbalimbali;hii itafanya bidhaa zako kujulikana kiurahisi zaidi hivyo kuongeza idadi ya wateja.
- Uzinduzi wa bidhaa mpya (Product launching) kwa mfano umekuja na samani mpya yenye ubunifu wa kipekee; itambulisha samani hiyo kwa uzinduzi ambao utajumuisha watu, hii itasaidia kuvuta hisia za watu juu ya bidhaa zako na kujiongezea wateja.
- Andika makala katika magazeti au majarida; tafuta gazeti ambalo lina maudhui ya masuala ya samani au jarida na kuwasilisha makala yahusuyo samani kila baada ya kipindi fulani. Hii itakusaidia kujitangaza kiurahisi zaidi.
Hakikisha unakuwa na mpango mkakati wa biashara yako (Strategic Plan) ambao utakuwa unakuonyesha wapi unaelekea na namna gani utafika. Vitu vilivyopo hapo juu ni miongoni mwa vitu ambavyo vitapaswa kuwa katika huo mpango mkakati wa biashara yako.
The Consult ; +255 719 518 367
Dar es Salaam
Tanzania