Fangasi Ukeni Husababishwa Na Nini?

Fangasi Ukeni Husababishwa Na Nini?

Dr isaya febu

Member
Joined
Jan 17, 2023
Posts
68
Reaction score
343
https://www.facebook.com/sharer.php?u=https://isayafebu.com/fangasi-ukeni-husababishwa-na-nini/
READ NEXT
pid

PID Kwa Mama Mjamzito.

Fangasi ukeni (vaginal yeast infection) husababishwa na kuongezeka kupita kiasi kwa fangasi aitwaye Candida albicans. Fangasi hawa kwa kawaida huishi ukeni bila kusababisha madhara (normal flora), lakini wanapoongezeka kupita kiasi, huleta maambukizi. Hali hii husababisha muwasho ukeni, kutokwa na uchafu mzito mweupe (kama jibini) ukeni, maumivu wakati wa kujamiiana au kukojoa, uwekundu na kuvimba maeneo ya uke.
fangasi ukeni

Fangasi ukeni wanaweza kusababishwa na mambo yafuatayo ikwemo:

1) Mabadiliko Ya Homoni.

Wakati wa ujauzito, hedhi, au kutumia vidonge vya uzazi wa mpango, mabadiliko ya homoni huathiri usawa wa bakteria na fangasi ukeni, na kuruhusu fangasi kukua zaidi.
mabadiliko ya homoni

2) Matumizi Ya Dawa Za Kuua Bakteria (Antibiotics).

Dawa za kuua bakteria (antibiotics) huua bakteria wabaya na wazuri, wakiwemo wale wanaodhibiti ukuaji wa Candida. Hii huacha fangasi wakikua bila kudhibitiwa.
antibiotics

3) Kinga Ya Mwili Kudhoofika.

Wanawake wenye magonjwa yanayoshusha kinga ya mwili kama vile kisukari kisichodhibitiwa, HIV, wanaopata matibabu ya saratani au wanaotumia dawa zinazodhoofisha kinga (kama steroids), huwa katika hatari kubwa zaidi ya kupata fangasi ukeni.
kinga ya mwili

4) Mavazi Ya Kubana Au Yenye Unyevunyevu.

Nguo za ndani zisizo za pamba (chupi za nailoni) au za kubana sana huongeza unyevu na joto ukeni — mazingira yanayochochea ukuaji wa fangasi ukeni.
Mavazi Ya Kubana

5) Kusafisha Uke Kwa Sabuni Kali Au Dawa Zenye Kemikali.

Kusafisha uke kwa sabuni kali au dawa zenye kemikali huua bakteria wazuri (normal flora) na kuvuruga usawa wa pH, hivyo kuruhusu fangasi kushamiri.
vaginal douching

HITIMISHO:

Ikiwa unapata dalili za fangasi ukeni, ni vyema kumuona daktari kwa uchunguzi na kupata matibabu sahihi, kama vile matumizi ya krimu au vidonge vya antifungal.
 
Attachments

  • 20090123_oaf_pwalsh_2_5_290x218.jpg
    20090123_oaf_pwalsh_2_5_290x218.jpg
    14.6 KB · Views: 21

Fangasi inatibiwa kienyeji ukitumia dawa haiwezi kuisha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom