Wakuu nilikua kwenye harakati za kujenga uhusiano na ndugu zangu upande wa baba ukizingatia mimi ni mtoto wa kando. Katika kutafuta mawasiliano nao nikabahatika kupata namba ya dada na kaka nikawaomba namba za ndugu zangu wengine wakanijibu hawana na ukizingatia wameshare mama na ni waliokulia huko kwenye mji wa mzee. Swala hilo likanishangaza nikawauliza wanautofauti kwanini hawana mawasiliano na ni ndugu moja sasa huyo bro akawa kimya hakunijibu. Huyo dada sasa kanipigia simu saivi ananiambia nataka nijione nawapenda sana hao hawana tofauti na wanapendana sana na hana namba zao kwa kuwa hana shida nao akiwa na shida nao atawatafuta kama nilivyomtafuta mimi nikamwambia Mimi sina shida nimetafuta ukaribu na ndugu zangu nijue na wajomba zangu inaweza tokea tukakutana kwenye mizunguko huko ukizingatia bado kijana nikajiguta na gegeda watoto wa dada zangu. Ila kwa jinsi kanipigia simu na kuniambia hivyo wakuu imebidi nifute namba zake na zoezi la kutafuta wengine nimeona liishie leo yaani kanifanya niwaze sana. Ukizingatia kuna msiba wa mke wa kwanza wa baba ulitokea sikupata taarifa wakati husika mpaka wamezika ndio napata taarifa.
Sent using
Jamii Forums mobile app