FAMILY

Wilhelm Johnny

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2016
Posts
1,369
Reaction score
1,338
Wakuu nilikua kwenye harakati za kujenga uhusiano na ndugu zangu upande wa baba ukizingatia mimi ni mtoto wa kando. Katika kutafuta mawasiliano nao nikabahatika kupata namba ya dada na kaka nikawaomba namba za ndugu zangu wengine wakanijibu hawana na ukizingatia wameshare mama na ni waliokulia huko kwenye mji wa mzee. Swala hilo likanishangaza nikawauliza wanautofauti kwanini hawana mawasiliano na ni ndugu moja sasa huyo bro akawa kimya hakunijibu. Huyo dada sasa kanipigia simu saivi ananiambia nataka nijione nawapenda sana hao hawana tofauti na wanapendana sana na hana namba zao kwa kuwa hana shida nao akiwa na shida nao atawatafuta kama nilivyomtafuta mimi nikamwambia Mimi sina shida nimetafuta ukaribu na ndugu zangu nijue na wajomba zangu inaweza tokea tukakutana kwenye mizunguko huko ukizingatia bado kijana nikajiguta na gegeda watoto wa dada zangu. Ila kwa jinsi kanipigia simu na kuniambia hivyo wakuu imebidi nifute namba zake na zoezi la kutafuta wengine nimeona liishie leo yaani kanifanya niwaze sana. Ukizingatia kuna msiba wa mke wa kwanza wa baba ulitokea sikupata taarifa wakati husika mpaka wamezika ndio napata taarifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole mkuu ndo maana wakasema watu ni wengi binadamu wachache.
 
Km maisha yako unaweza kuyaendeleza bila wao nakuomba endelea na maisha yako.
Unachokitafuta ni kujiongezea mzigo usio na sababu maisha haya tuliyonayo ni magumu sana hayahitaji kuongeza matatizo ya watu wengine tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, futa namba lakini usikose kufuatilia ndugu zako kwa kuwa lengo lako ni jema na huo ndiyo utu.

Ukiondoa huyo dada kidomodomo, ambaye kibusara ndiye unatakiwa uanze naye kumuonesha upendo mkubwa, maana wale wengine wenye busara ni rahisi kuwaunganisha.

Kitu kimoja ambacho unatakiwa ukae ukikielewa ni kwamba, watoto mnapozaliwa kwa kushare baba, mama zenu wakawa tofauti ama mkashare mama, baba zenu wakawa ni tofauti, malezi pamoja na makuzi yenu yakawa pia ni tofauti, basi huwa ni kazi sana kupatanana kuwa wamoja.

Ni rahisi kujenga mahusiano mkaelewana na mtu baki kuliko ndugu wa namna hiyo.

Kinacholeta tatizo hapo ni mambo mengi madogomadogo ikiwemo dharau, uchoyo na upendeleo kwa mama zenu kila mmoja kujali kwa kuona kuwa, watoto wake ni bora sana kuliko wa wenzake.

Pia kuna mila potofu za kimaskini zinazolenga na kuangalia jinsi ugawanaji wa mirathi pindi wazazi wenu watakapokuwa wamefariki nk nk.

Ndiyo maana wao hawajihangaishi kukufuatilia hadi sasa, siyo kwamba hawakujui, bali upendo haupo miongoni mwao.

Hapo sasa, wewe jishushe sana kwao na utumie busara sana namna ya kuhandle hao ndugu zako, wajali kwa zawadi ndogondogo na kauli za upendo, mwishowe watajisuta.
vinginevyo haiwezekani kuwafanya muwe wamoja na kujenga undugu ulio imara.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ni mtoto wa kando unataka ujuane nao wakati mama yako alikua anamnyima mama yao usingizi. Yaani wewe ni mtoto wa mchepuko. Msma yako alikua mwizi wa wanaume wa watu wewe watakuamini vipi
 
kuchangia damu hakumaanishi ni ndugu..

ndugu wa kweli ni yule anayekujali kwa dhati... na ndio maana rafiki anaweza kuwa mtu wa thamani kwako kuliko uliozaliwa nao tumbo moja!
 
Wewe ni mtoto wa kando unataka ujuane nao wakati mama yako alikua anamnyima mama yao usingizi. Yaani wewe ni mtoto wa mchepuko. Msma yako alikua mwizi wa wanaume wa watu wewe watakuamini vipi
una uhakika mkuu?
 
Komaa na hao ndugu zako wachache mnaofahamiana wengine achana nao!! kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchukuzi!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…