Familia za marehemu waliofariki kwenye maandamano ya Gen Z mwaka jana zapanga kufanya maandamano Jumatano hii!

Familia za marehemu waliofariki kwenye maandamano ya Gen Z mwaka jana zapanga kufanya maandamano Jumatano hii!

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,439
Reaction score
6,692
Familia za waathiriwa wa mauaji yaliyotekelezwa na polisi wakati wa maandamano ya Gen Z mwaka jana dhidi ya Muswada wa Fedha (Finance Bill) mwaka jana, zimetangaza kufanya maandamano ya amani jijini Nairobi na maeneo mengine nchini Jumatano ijayo kuadhimisha mwaka mmoja tangu vifo vya wapendwa wao.


Wakiongozwa na kina mama wa marehemu, familia hizo zimesisitiza kuwa maandamano yatakuwa ya amani na wanatarajia ulinzi kutoka kwa polisi.

Wameitaka serikali kuharakisha upatikanaji wa haki kwa vifo vya watoto wao, huku wakikemea wanasiasa na magenge ya kulipwa kuingilia maandamano hayo kwa maslahi binafsi.

Wakili Njanja Maina alionya kuwa siku hiyo ni ya familia zilizoathirika, si nafasi ya kutafuta umaarufu wa kisiasa.
Kwa upande mwingine, vijana wa kizazi cha Gen Z wanatarajiwa kuongoza maandamano hayo kama kumbukumbu ya maandamano ya kihistoria ya Juni 25 mwaka jana, wakidai haki na utawala bora.

Mabango yanayosambaa mtandaoni yanawahimiza vijana kufika na bendera pamoja na chupa ya maji.
Kamanda wa polisi wa Nairobi, George Seda, amethibitisha kupokea taarifa rasmi kutoka kwa waandaaji wa maandamano na akaahidi usalama kwa wote watakaoshiriki na wasiotaka kushiriki.

Hata hivyo, aliwataka waandamanaji kuzingatia sheria na kuepuka vitendo vya kuvunja amani kama ilivyoshuhudiwa awali jijini Nairobi.

=======================

Families of victims of police killings during last year's anti-Finance Bill protests will hold protest marches in Nairobi and across the country on Wednesday next week to mark the first anniversary of their kin's deaths.

The families, led by the mothers of the victims, said they expect police protection for the march, which they say will be peaceful.

At the same time, they have asked the government to expedite the search for justice for the deaths of their children.

Souurce: Citizen Digital
 
peter elias kapingu.jpg
 
Back
Top Bottom