vuta subira hapa ndiyo mpango mzima majungu peleka fb kwa wale wanaotaka niweke mwendelezo hapa semeni ndiyo
sasa Endelea...JUDDY
aliondoka meza kuu na
kwenda katika jukwaa
lililotayarishwa tayari kwa
sherehe. Pale alipokaa,
alisikia kama vile kuna
mkwaruzo kwenye kipaza
sauti, akasogea ili
kumwelekeza fundi mitambo
arekebishe kasoro hiyo.
Wageni wengine wote
walikuwa tayari kwenye viti
vyao na wahudumu
waliifanya vizuri kazi yao,
vinywaji mfululizo
viliendelea kutolewa na stori
za hapa na pale zikipamba
moto miongoni mwa wageni.
Watoto wadogo waliokuwa
wakicheza muziki wa msanii
Mr Nice, uitwao Kidali Poo,
ndiyo waliokuwa wa kwanza
kumuona Tonny katika
mavazi yake ya kishetani.
Walipiga kelele kubwa na
kukimbilia upande wa watu.
Kelele zile ziliwashtua watu
wote akiwemo Juddy
aliyekuwa akizungumza na
fundi mitambo, alipotazama
mlangoni, akamuona mtu
aliyeamini ni shetani !
Mamamaaaaaa, Juddy
alipiga kelele na kuanza
kukimbia jukwaani. Akitafuta
sehemu salama ya
kukimbilia, kwa bahati
mbaya akakanyaga waya,
akaanguka na bila kutarajia,
kichwa chake kikaenda
kuangukia kwenye maungio
ya nyaya za umeme!
Waya mmoja ukachomoka,
ukaishia kwenye shingo
yake. Ndani ya sekunde
chache, mwili wake
ukabadilika rangi .
Kelele za kukimbia kwa
watoto na vijana wengine
zilidumu kwa muda kadhaa
kabla Tonny hajavua kinyago
kile na kuanza kucheka.
Shughuli ilishaharibika.
Wakati watu wanaanza
kurejea katika hali ya
kawaida, wakagundua mtu
aliyelala kimya ametulia
chini, pembeni ya jukwaa.
Ni Juddy!
Haraka watu wakakusanyika,
wakaogopa kumsogelea.
Fundi mitambo alijua
kilichotokea. Akazima
umeme wa jukwaani,
akamsogelea na kumgusa,
akawatazama watu kwa
huzuni.
Jamani tumbebe, mambo
yameshaharibika, alisema
fundi mitambo.
Hebu subiri, nini? Mzee
Komba aliuliza baada ya
kubaini utulivu aliokuwa nao
Juddy, moyoni mwake akajua
mambo hayako sawa.
Hebu watoto tokeni hapa,
sogeeni kule, alisema mzee
huyo na watoto, wakiwa
kimya, wakasogea pembeni.
Mzee Linus akasogea, mama
Juddy alikuwa amesimama
mbali, mwili ukimtetemeka!
Mmoja kati ya wageni
waalikwa alikuwa daktari, Dr
Junior. Akasogea na kwenda
kumgeuza Juddy, akamshika
moyo, akaonyesha uso wa
huzuni pia. Akatoa ishara ya
kumbeba msichana huyo.
Akabebwa na kupelekwa
kwenye gari kwa safari ya
kuelekea hospitalini.
Wakati magari yanafuatana
kuelekea hospitali ili kupata
uhakika wa nini kimetokea,
wageni waliokuwa hapo
wakaonekana wamejipanga
makundi makundi, mama
Juddy alikimbilia chumbani
kwake kujifungia, akilia kwa
uchungu.
Sijui kama atapona, fundi
mitambo aliwaambia watu
waliomzunguka kutaka kujua
nini kimetokea. Alikanyaga
waya wakati anakimbia,
bahati mbaya alipoanguka
akaangukia hapa, hizi nyaya
zikachomoka moja ikamgusa
mwilini na bahati mbaya
akailalia, alisema fundi
huyo na kusababisha vilio
kutoka kwa watu
waliokusanyika eneo hilo.
Mzee Linus, Komba, Dr
Junior na majirani wengine
kadhaa walikuwa nje ya
Hospitali ya IMTU, eneo la
Mbezi jijini Dar es Salaam
wakisubiri ripoti ya daktari,
ingawa wote walitambua
kwamba Juddy alishafariki.
Hakuna aliyekuwa akisema
chochote, wote walionekana
kujiinamia kwa huzuni.
Aliyekuwa na hali mbaya
zaidi, alikuwa ni mzee
Komba. Kijana wake ndiye
aliyesababisha tafaruku
yote, hakuelewa nini hatima
yake.
Baada ya nusu saa, daktari
wa hospitali hiyo
aliyetambulika kwa jina la
Rama, alitokea kwenye
ukumbi waliokuwa
wamejazana watu, akaomba
wahusika wa karibu
kumfuata ofisini kwake.
Poleni sana, mpendwa wetu
amefariki dunia. Inaonekana
ameunguzwa vibaya na
umeme, poleni sana, Dk.
Rama aliwaambia mzee
Linus na mzee Komba
waliokuwa wamekumbatia
mikono vifuani mwao!
Nini kitaendelea?
vuta subira hapa ndiyo mpango mzima majungu peleka fb kwa wale wanaotaka niweke mwendelezo hapa semeni ndiyo
vuta subira hapa ndiyo mpango mzima majungu peleka fb kwa wale wanaotaka niweke mwendelezo hapa semeni ndiyo
ILIYOPITA
huku akigonga kwa nguvu
mlango, hakukuwa na
majibu.
Inabidi uvunjwe, askari
alisema. Mzee Komba
akatikisa kichwa kukubali.
Kazi hiyo ikafanyika,
kitasa kikavunjwa na mara
mlango ukawa wazi.
Tonny alionekana akiwa
amelala sakafuni.
SASA ENDELEA...
ASKARI alimsogelea Tonny,
akamwangalia vizuri usoni
mwake, mwili ulionekana
kuloa maji. Mzee Komba
naye akaingia chooni na
kumtazama mwanaye. Askari
akamgeuza uso ukatazama
juu.
Dr Junior, jirani yao ambaye
kwa muda wote amekuwa
karibu na tukio hili,
akawaomba wambebe kijana
huyo na kumtoa nje, kwa
sababu ya nafasi ndogo
ndani ya choo.
Tonny akatolewa na kulazwa
kwenye korido. Dr Junior
alimtazama, akamshika
kifuani kupima mapigo ya
moyo wake.
Amepoteza fahamu,
nadhani ataamka baada ya
muda mfupi, aliwaambia
watu ambao sasa
walishakuwa wengi ndani ya
nyumba ya mzee Komba.
Apepewe, askari aliamuru
na mara moja, ndugu zake
Tonny wakaanza kumpepea
kwa khanga na vitenge.
Baada ya dakika chache za
kupepewa, Tonny
alijitingisha, dalili kuwa
fahamu zinaanza kumrejea,
kisha akafunua macho,
akainuka na kukaa. Wote
walimtazama kwa hofu.
Unajua nini kimetokea?
Baba yake alimuuliza
mwanaye huku ameingiza
mikono kwenye mifukoni ya
suruali yake.
Ndiyo baba, Tonny alijibu,
machozi yakimlengalenga
machoni mwake.
Nini kimetokea?, mzee
Komba alimuuliza tena.
Kule kwa kina Juddy
baba ., Tonny akashindwa
kumalizia, akaanza kulia kwa
sauti.
Mbadilishieni nguo, askari
alisema, akachukuliwa na
kuingizwa ndani,
akabadilishwa nguo.
Mzee, poleni kwa matatizo,
inauma sana. Hata hivyo,
huyu kijana itabidi twende
naye kituoni kwa mahojiano
zaidi. Mambo mengine
nadhani mtayajua huko,
askari alimweleza mzee
Komba aliyetingisha kichwa
kukubaliana naye!!!
***
Baada ya gari la polisi
kuondoka alfajiri ile, huzuni
ilirejea upya. Mama yake
Tonny alikuwa akilia pamoja
na mama Juddy, ni tukio
ambalo halikutarajiwa na
liliwagusa wote kwa pamoja.
Dada hata sijui nikuambie
nini, naumia sana yaani..,
mama yake Tonny
alimwambia mama Juddy,
akimfuta machozi wakati
yeye mwenyewe akiwa
analia.
Usijali dada, mipango ya
Mungu, ni bahati mbaya,
sote nafsi zetu zitaonja
mauti, naye alimjibu
mwenzie, kitu ambacho
kilimfariji sana.
Siku hiyo ilitumika
kusambaza habari kwa
ndugu jamaa na marafiki
sehemu zote duniani. Msiba
huo uliwashtua watu wengi.
Aliyeumia zaidi alikuwa ni
Asfat, dada yake Tonny
aliyekuwa swahiba mkubwa
wa Juddy.
Alikuwa Birmingham nchini
Uingereza anakosoma,
akisubiri kupanda treni
kuelekea London kumpokea
shosti wake alipopokea simu
ya kaka yake, Amani. Ilikuwa
ni saa moja na nusu asubuhi
kwa saa za huko.
Usiniambie ameshapanda
ndege tayari kaka, Asfat
alimwambia Amani mara tu
alipoweka simu yake sikioni.
Si bora hata angepanda
baadaye, hatapanda tena,
Amani aliongea kwa sauti
ndogo, yenye majonzi,
iliyomshtua sana dada yake.
Heee, imekuaje tena kaka
Amani mbona unanishtua,
baba amegoma kwani ,
aliuliza kwa hamaki.
Dah, dada wee acha tu,
Juddy amefariki,
Ni...ni...ni...?!!
Amani alimtuliza dada yake,
akamwelezea kisa kizima
kilivyokuwa, habari ambazo
zilimsikitisha na kumliza
sana. Aliyekufa ni rafiki yake
wa kufa na kuzikana na
aliyeua ni mdogo wake wa
damu!
Shughuli za msiba
zikaendelea, ukapangwa
kufanyika siku nne baadaye
ili kuweza kuwakusanya
ndugu na marafiki
waliokuwa mbali.
Kama ilivyo kawaida ya siku
zote, licha ya msiba ule
kusababishwa na wao, lakini
walishiriki kwenye shughuli
kama kawaida, wote
wakionyesha kuwa na
uchungu. Katika hali ya
kawaida, hakuna mtu
aliyetegemea yaliyokuwa
yakitokea.
Mzee Komba na familia yake
walishiriki kila hatua ya
tukio lile na mzee Linus na
familia yake nao
hawakuonyesha kinyongo
chochote, wote waliamini
kilichotokea ilikuwa ni
mipango ya Mungu.
Je, nini kilitokea?