CotterPin
JF-Expert Member
- Jul 30, 2018
- 2,398
- 5,006
Natumai wote ni wazima wa afya, licha ya kipindi hiki kigumu ambacho wengine bado tupo kwenye maombolezo na wengine tukiendelea kupambania ndoto ya uchaguzi huru na wa haki kwa taifa letu.
Leo nimekutana na simulizi ya maisha ya mama mmoja ambaye kwa heshima nitamwita Asha. Kwa kweli imenigusa sana, nikahisi ni jambo la busara na lenye maana kuiweka hapa ili tukumbushane thamani ya ujasiri, uvumilivu, na matumaini.
Hadithi ya Asha ni ushuhuda wa kweli wa mwanamke ambaye licha ya changamoto nyingi alizopitia kuanzia utoto, familia iliyovunjika, manyanyaso, maisha ya mitaani, hadi kusalitiwa na wale aliowategemea bado aliinuka, akajipambania, na hatimaye kupata mwanga wa upendo wa kweli na heshima ya maisha mapya.
Ni simulizi ya maumivu, lakini pia ni simulizi ya nguvu ya mwanamke. Ni somo kwa sisi sote kuwa hakuna giza linalodumu milele, na kuwa uzito wa sasa unaweza kuwa ushindi wa kesho ikiwa tutajipa nafasi ya kusimama tena.
Nitaiweka hapa kwa mfululizo ili wote tuweze kusoma na kujifunza. Karibuni tujifunze pamoja.
WASIFU WA MAISHA YANGU – ASHA
Nilizaliwa katika familia ya watoto wanane. Tulianza maisha ya kawaida ya kijijini, tukiishi kwa mshikamano wa familia na maadili ya kijadi. Lakini mambo yalianza kubadilika baada ya baba yetu kustaafu na kuoa mke wa pili. Ndoa hii mpya ilileta mpasuko mkubwa katika familia yetu, na hali ya upendo, mshikamano na uelewano ikapotea.
Nikiwa mdogo, niliishi kwa kaka zangu wawili kwa zamu. Kaka yangu mkubwa alinichukua nikaanza kuishi naye. Lakini maisha hayakuwa rahisi. Alikuwa na asili ya ubinafsi na uchoyo—hata nguo mpya hakuwahi kuninunulia. Nilipokuwa mkubwa kiasi, nilijikuta navaa nguo za mke wake (wifi yangu). Aibu hiyo niliibeba moyoni kimya kimya.
Nilikaa naye hadi darasa la nne, tukarudi nyumbani likizo. Kaka yangu aligombana na baba, na akaniacha bila kujali hatma yangu. Nililazimika kuishi na mama wa kambo hadi nikamaliza darasa la saba, kwani mama yangu mzazi alikuwa ameondoka kitambo.
Nilipofaulu darasa la saba, nilipangiwa shule ya sekondari ya serikali. Lakini kutokana na uhaba wa nafasi kipindi hicho cha miaka ya 2000, jina langu liliuzwa. Hakukuwa na msaada wowote kutoka kwa familia. Nikakaa mwaka mzima nyumbani, nikiangalia ndoto zangu zikififia.
Maisha yalizidi kuwa magumu. Nikaamua kutoroka nyumbani, nikiwa kijana mdogo asiyejua atakakokwenda. Katika safari yangu, nilikutana na konda wa basi la kwenda Dar es Salaam. Nikamdanganya kuwa nimetoka kwa watu waliokuwa wakinifanyisha kazi za ndani, na sasa nataka kurudi kwa kaka yangu anaishi Magomeni, Dar.
Yule konda alinielewa. Alinichukua na kunipeleka kituo cha polisi katika mkoa mmoja tulipopitia, ambapo walinisikiliza na kunipatia barua ya kupelekwa kwa Station Master wa reli. Nilipangiwa kupanda treni kuelekea Dar es Salaam siku iliyofuata jioni.
Kwa huruma yake, yule konda alinipeleka sehemu nikapate chakula, kwani siku hiyo sikuwa nimekula hata mlo mmoja, wala sikuwa na hata senti ya kujihudumia. Huo ulikuwa mwanzo wa tumaini jipya katika maisha yangu. Kutoka kwa mtu nisiyemfahamu, niliona upendo wa kweli jambo ambalo sikuwahi kulipata hata kwa ndugu zangu wa damu.
---
Jeraha la Kimya
Baada ya kula chakula cha usiku, yule konda aliniambia atanilipia chumba kwenye gesti iliyo karibu na kituo cha treni, ili nipumzike mpaka kesho yake jioni ambapo treni ingeondoka. Alisema yeye ataondoka mapema asubuhi, kurudi na basi lake mkoani. Nilimwamini. Sikuwa na chaguo jingine, na kwa macho ya mtu mgeni, alionekana ni malaika aliyenisaidia wakati wa giza.
Nakumbuka ilikuwa mida ya saa sita usiku. Niliposikia hodi mlangoni, niliamka na kufungua. Alikuwa ni yeye. Alinipatia mfuko wa plastiki wenye gauni moja, jacketi, raba, mafuta ya mwili, dawa ya meno na mswaki. Akaniambia analala hapo chumbani kwa sababu ataondoka mapema. Sikutilia shaka niliona bado yupo kwenye nafasi ya msaada.
Lakini usiku huo, hali ilibadilika. Alitumia nafasi hiyo kulipiza fadhila kwa njia ya udhalilishaji. Alinibaka. Sikumpa ridhaa. Sikujua cha kufanya. Niliumia sana kimwili na kiakili. Nikiwa bado mdogo, asiye na msaada, na mwenye deni la shukrani moyoni, sikuweza hata kupaza sauti. Nilihisi kuwa ni hatia yangu, kwa sababu nilitegemea huruma ambayo iliishia kuwa uonevu wa kishetani.
Alirudia mara kadhaa bila huruma, bila kujali machozi yangu ya kimya. Baada ya kuridhika, aliniaga, akaniachia shilingi 2500 za chakula, kisha akaondoka alfajiri.
Nilibaki peke yangu nikivuja damu moyoni, nikiumia kimya kimya. Huo ndio ulikuwa mwanzo wa mabadiliko makubwa ya nafsi yangu. Sikuamini tena watu kirahisi. Nilijifunza kuwa si kila msaada ni wa baraka. Baadhi huja na gharama nzito za roho.
Lakini nilijua safari yangu haijaisha. Hata kama nilianza kwa machozi, niliapa moyoni kuwa nitatembea hadi mwisho kwa heshima, kwa kujiheshimu, na kwa ajili ya mustakabali wa maisha yangu.
---
Mwangaza wa Matumaini
Nilipofika Dar es Salaam, kaka yangu mdogo ndiye aliyenipokea. Wakati huo alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu. Licha ya changamoto zake binafsi, alinikaribisha kwa moyo wa upendo na kunitazama kwa jicho la ndugu wa kweli.
Aliniambia kuwa kwa kuwa hajaoa, na kwa sababu hawezi kuniweka chuoni kwake, nitahamishiwa kwa kaka mkubwa nikae huko kwa muda, huku yeye akiendelea kunigharamia mahitaji na masomo yangu. Nilihisi hofu moyoni, kwani kumbukumbu za nyuma na kaka huyo hazikuwa nzuri. Lakini sikuwa na pa kwenda. Nilimwamini kaka mdogo na nikaenda.
Kaka mdogo alitimiza ahadi yake. Niliendelea na shule, nikasoma hadi kidato cha tatu. Hata hivyo, hali kwa wifi ilizidi kuwa ngumu. Alinifanya maisha yawe ya mateso ya kimya, ya matusi, dharau, na wakati mwingine kunyimwa hata mahitaji ya msingi. Hali hii iliwashtua baadhi ya marafiki wa kaka mkubwa, waliomjulisha kaka mdogo kuhusu hali halisi ya maisha niliyokuwa nayo.
Kaka mdogo hakusita. Aliniita tena Dar, akanipangishia chumba changu mwenyewe. Ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuwa na nafasi huru ya kupumua, kuishi kwa utulivu, na kuendelea na masomo bila bughudha.
Niliendelea na shule nikiwa chini ya uangalizi wake. Hapo ndipo nilianza kuelewa maana ya kuwa na mtu anayekupigania bila masharti, anayekutazama kama binadamu kamili, si mzigo. Upendo wake na msaada wake uliweka msingi mpya wa maisha yangu.
---
Vizingiti vya Ndoto
Baada ya kumaliza elimu ya sekondari, moyo wangu ulijaa ndoto mpya—kutumikia taifa kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) au majeshi ya ulinzi. Nilimwomba kaka yangu mdogo anisaidie kufanikisha hilo. Wakati huo, alikuwa tayari ameoa. Nilitegemea familia itakuwa msingi wa sapoti mpya, lakini hali haikuwa kama nilivyotarajia.
Wifi mdogo, badala ya kuwa msaada, alianza kuingilia uamuzi wa kaka. Kwa ustadi wa maneno na ushawishi wa karibu, alimshawishi kaka asinikubalie kujiunga na jeshi. Nilidhani huenda alikuwa na sababu nzuri huenda alikuwa ananiwazia mema au anaogopa nisije potea. Lakini baadaye nikagundua, alikuwa na ajenda yake ya siri.
Wakati huo, serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete ilikuwa imeanzisha fursa kwa vijana kujiunga na mafunzo ya ualimu ya muda mfupi, ambapo baada ya mafunzo hayo, vijana wengi walipewa ajira ya moja kwa moja. Hata nafasi hiyo ilipofika, wifi huyo alihusika moja kwa moja katika kunizuia. Alipanga mipango yake kimya kimya, akachukua nafasi hiyo kwa watu wake wa karibu, na mimi nikabaki nikitazama ndoto zangu zikizimika polepole.
Nilihisi kutengwa. Si mara ya kwanza, lakini kila ilipotokea iliuma kwa namna mpya. Kila mlango wa matumaini uliokuwa unafunguliwa, ulifungwa na mikono ile ile ya watu waliopaswa kuwa ngao yangu.
Lakini sikukata tamaa. Nilijua bado nilikuwa na pumzi ya kupigania ndoto zangu kwa jasho, kwa maombi, na kwa uvumilivu.
---
Moyo Usiokatika
Baada ya kukataliwa kujiunga na jeshi na kupoteza fursa ya ualimu, sikuacha kupambana. Niliamua kujifunza taaluma yenye mustakabali mzuri nikasoma Diploma ya Teknolojia ya Habari (IT). Nilijitahidi kwa kila hali kumaliza masomo hayo, nikiwa na matumaini kwamba taaluma hii itanitoa kwenye changamoto za maisha ya utegemezi.
Baada ya kumaliza, nilianza kutafuta ajira kwa bidii. Nikiwa na cheti mkononi, nilizunguka sehemu nyingi nikiwa na CV yangu, nikijitambulisha, nikijaribu kupata nafasi yoyote ya kufanya kazi. Hatimaye, nikapata sehemu ya kujitolea, kazi isiyolipwa lakini yenye thamani kubwa ya uzoefu.
Kaka yangu alipogundua kuwa najitolea, alionekana kufurahia mwanzoni. Alisema anapanga kufungua kampuni ya IT na angependa niisimamie. Alinitia moyo nikahisi huenda sasa mambo yanakwenda sawa. Lakini bado, kivuli cha wifi yangu kilikuwa hakijaniacha.
Mara nyingine tena, alipinga. Alisema siwezi kuaminika, au huenda alihofia kuwa nitakuwa karibu sana na familia yao. Kaka aliingia tena kwenye mtego ule ule akamuamini zaidi mke wake kuliko ukweli wa maisha yangu.
Baadaye kidogo, kulikuwa na nafasi za ajira serikalini, kwenye wizara aliyokuwa anafanya kazi kaka. Kwa heshima, nilimshirikisha, nikamweleza nia yangu na kumkabidhi barua ya maombi pamoja na wasifu wangu (CV). Alinikubali kimdomo, akaniambia atafanya kila awezalo kusaidia.
Mwaka mzima ulipita bila majibu. Sikuwahi kupata mrejesho wowote. Nilikaa kimya, nikiheshimu ukimya wake. Lakini cha kushangaza zaidi, mwaka uliofuata, alikuja mwenyewe kunieleza kuwa mke wake alimshauri kuwa nikipata kazi katika wizara moja naye, nitakuwa tatizo kwake. Na kwa sababu hiyo, aliamua kutonisaidia.
Nilibaki kimya. Nilihisi kama dunia imenimeza. Nilijitahidi kwa kila hali kufanya mambo kwa heshima, kwa uaminifu, bila chuki. Lakini bado nilionekana kuwa mzigo kwa wale waliopaswa kuwa mabega yangu.
Lakini ndani ya yote hayo, nikajifunza jambo moja muhimu wema wa kweli hauwezi kufungwa kwa hofu au maneno ya wengine. Nikaapa kuendelea kupigana, kwa ajili yangu, kwa ajili ya mustakabali wangu, na kwa ajili ya watoto wangu wa baadaye, ambao sitawahi kuwaangusha kama mimi nilivyoangushwa.
---
Kupigania Nafasi Yangu
Baada ya kuona kuwa kila jaribio la kujenga maisha chini ya mwavuli wa kaka lilikuwa linawekewa vizingiti, niliamua kujisimamia. Sikuwa na kisasi moyoni, ila nilihitaji nafasi ya kupumua. Nikaanza kujitafuta kwa bidii, safari hii bila kumshirikisha mtu yeyote katika familia.
Siku zangu zikawa ndefu nikitoka asubuhi saa kumi na moja, nikitekeleza majukumu ya nyumbani kabla ya kuondoka. Nilihakikisha nimejaza mapipa ya maji kama ilivyotarajiwa. Lakini niliporudi jioni, sikuwa nakuta chakula. Wala sikukuta hata maji ya kuoga. Nilihisi kama mpangaji wa kulazimishwa, si ndugu wa damu. Hali hii iliniumiza kwa miaka miwili niliyokaa kwa kaka baada ya kuoa.
Hatimaye, nikaamua kuondoka. Nikapanga chumba changu mwenyewe huko Mburahati. Nikiwa peke yangu, nilihisi huru hata kama maisha yalikuwa magumu, angalau nilijua kinachotokea ni kutokana na juhudi zangu mwenyewe.
Niliendelea kujitolea ofisini, nikiweka juhudi kubwa na kujifunza kila kitu nilichoweza. Sikuchoka, sikukata tamaa. Jitihada zangu zikaanza kuonekana. Mkurugenzi wa ofisi hiyo, baada ya kuona bidii na uaminifu wangu, aliamua kunipa nafasi ya ajira ya muda.
Nikaanza kulipwa shilingi laki mbili kwa mwezi, kwa kazi ya siku sita kila wiki. Ilikuwa ndogo, lakini kwangu ilikuwa ni zaidi ya mshahara ilikuwa ni heshima, ni matumaini, ni uthibitisho kuwa kazi yangu haikuwa bure.
Nilianza kujiona tena. Sauti yangu ya ndani ilianza kuninong'oneza kuwa sina budi kuamini ndoto zangu tena. Na hapo ndipo safari mpya ya kujijenga ilipoanza.
---
Upendo wa Kweli Baada ya Maumivu
Baada ya kupata kazi ya muda, nilihisi dunia inaanza kubadilika kwa upande wangu. Lakini nyuma ya fursa hiyo, kulikuwa na kivuli kingine. Mkurugenzi wangu alianza kunionesha dalili za kunitamani kimapenzi. Hakuwa mtu wa maneno mengi, lakini vitendo vyake vilianza kuleta tafsiri tofauti.
Nilipoanza kupata nafasi nyingi za kwenda kwenye safari za kikazi, meneja alibadilika. Baadaye nikagundua kuwa yeye alikuwa ana mahusiano ya kimapenzi na huyo mkurugenzi. Aliona kuwa mimi ni tishio kwake. Majungu yakaanza, baridi ya ofisi ikageuka joto la chuki. Nilikataa kabisa kumkubalia huyo mzee, kwani nilikuwa nimeshaelezwa tabia zake mwanamume wa wanawake wengi, anayewapa mimba na kuwaacha. Sikutaka kuwa sehemu ya majeruhi wake.
Wakati huo, moyo wangu ulikuwa umechoka. Mzigo wa maisha ulikuwa mzito sana, na nilihisi kuwa peke yangu. Ndipo nikakutana tena na rafiki wa zamani kutoka shule ya sekondari mwanaume tuliokuwa marafiki wa kawaida, hatukuwa wapenzi.
Alikuja Dar kwa likizo akitokea Arusha alikokuwa anaishi na kufanya kazi kama mwalimu. Nilimkaribisha kwangu kwa upendo wa kirafiki. Sikuwa na matarajio yoyote. Lakini tulipoangaliana machoni, tulihisi kitu tofauti. Hakuniambia maneno ya mapenzi tulihisi tu. Tukajikuta tumekumbatiana, tukavunjika kimya kimya, tukapendana kwa undani ambao haukuhitaji maneno mengi.
Ndani ya miezi sita, alitangaza ndoa. Hakunitia masharti. Hakunihoji kuhusu maisha yangu ya nyuma. Alinipokea kama nilivyo. Tukafunga ndoa. Leo hii, tunao watoto watatu. Maisha yanaendelea, si mazuri kupita kiasi, lakini yenye heshima, upendo, na ushirikiano. Hatukuanza na magari wala nyumba, bali tulianza na moyo mmoja.
Lakini kama ilivyokuwa kawaida, hata siku ya ndoa yangu, hakuna ndugu hata mmoja aliyehudhuria. Wala mama, wala baba, wala mmoja wa wale ndugu saba. Nilihisi uchungu, tena mkubwa sana maana harusi ni jambo la furaha, lakini nilijikuta peke yangu. Niliomba baba mmoja wa kanisani anisimamie. Alinifanya nihisi kuwa bado kuna watu wa kujaza nafasi za waliokosekana.
Mwaka 2019, niliamua kupeleka watoto kijijini, ili wakamjue babu na bibi yao. Niliona ni haki yao. Baba alitaka wafikie kwa mke mdogo, mama alitaka wafikie kwake. Nilichagua kuwapeleka kwa mama yangu mzazi. Uamuzi huo ulimchukiza baba kiasi cha kukataa kuja kuwaona. Mama naye alikataa kabisa kuwapeleka kwa baba yangu.
Tuliwasalimia wote kwa heshima. Mimi na mume wangu tulimfuata baba, tukampa zawadi, tukamkumbatia kwa moyo mweupe. Lakini hakuwahi kuja kuwaona wajukuu zake. Mpaka leo, mume wangu hatambuliki upande wa kwetu. Hana mawasiliano na ndugu zangu. Wote wamemkataa bila sababu ya msingi.
Lakini ndani ya yote hayo, nimejifunza kuwa familia si damu tu. Familia ni wale wanaokuamini, wanaokuombea, wanaokuinua bila masharti. Na kwa hilo, mume wangu na watoto wangu ndio familia yangu ya kweli.
---
Hitimisho
Safari ya maisha ya Asha si hadithi tu ya huzuni, bali ni alama ya matumaini. Kutoka kwenye familia iliyovunjika, mateso ya utotoni, manyanyaso ya kijinsia, na vizingiti vya elimu na kazi, Asha alisimama kidete akajitambua, akajitegemea, na hatimaye akajijengea familia yenye upendo na amani.
Licha ya kukataliwa na damu yake mwenyewe, aliweza kujenga kizazi kipya kilichojaa heshima na maadili. Mume wake, aliyeingia kwenye maisha yake kwa njia ya kipekee na ya upole, alimpa kile alichokikosa maisha yake yote mapenzi ya kweli, heshima, na ushirikiano.
Asha hakurudi nyuma. Hakuruhusu chuki, huzuni, wala majuto kuwa urithi wake. Alichagua kusamehe, kusonga mbele, na kuwa nguzo ya nguvu kwa familia yake mpya. Katika maisha yenye giza, aliweza kuwa taa.
---
Funzo kwa Wengine
Kila mtu ana mapito. Maisha hayaendi sawa kwa wote, lakini ndani ya kila maumivu kuna nafasi ya ukuaji. Simulizi ya Aisha inatufundisha kwamba:
-Vatican 😭
- No reform, no Election 😭
- watesi wetu 😰

- Maisha yanaanza upya kila siku – hata ukishindwa leo, bado una nafasi kesho.
- Familia ni wale wanaokujali, si lazima wawe damu yako.
- Kusamehe hakuondoi uchungu mara moja, lakini kunaweka huru moyo wako.
-Vatican 😭
- No reform, no Election 😭
- watesi wetu 😰