Falsafa ya urembo,uzuri na ubaya

mwamba c

JF-Expert Member
Jan 2, 2017
690
2,362
Habarini,

Moja kwa moja niende katika hoja ya falsafa ya uzuri na ubaya kwa kulenga wanaume katika kuchagua wanawake kwani kumekuwa na mitazamo tofauti katika kuchagua wa kuishi nao au kujiburudisha nao. Kila mwanaume huwa ana mtazamo wake katika kuchagua, baadhi ya wanaume huchagua wanawake wanene, wenye makalio makubwa, matiti makubwa, weusi, weupe, maji ya kunde, warefu au wafupi, wenye pesa, mali au hata ulemavu wa ngozi.

Ikitokea ukaona mtu ameamua kuishi na yeyote yule ambae kwa mtazamo wako unahisi amekosea, basi wewe ndio utakua umekosea kwani uzuri wa mtu haupimwi kwa vigezo vya mtu mmoja mmoja au kikundi cha watu. Uzuri wa mtu unapimwa kwa mboni za macho za yule anayemtazama ambaye anafikiri ni sahihi kwake.

Kwa kifupi sana hakuna mwanamke ambaye ni mbaya wala mzuri na hii ni kutokana na mitazamo tofauti ya wanaume jinsi wanavyowachukulia wanawake, hivyo kila mwanamke anaweza akawa mzuri kulingana na mtazamo wa mtu fulani na pia akawa mbaya kulingana na mtazamo wa mtu mwingine pia.

Enyi mawifi, mashemeji, marafiki, mama mkwe, baba mkwe waacheni jamaa zenu wawe na watu ambao wao wenyewe wanafikiri na kuona ni sahihi kwao, acheni kukosoa mitazamo yao kwa kudhani wanakosea, hapana ninyi ndio mnakosea.

Nawasilisha
 
Hakuna mwanamke mbaya duniani, wote ni wazuri tu, ila kila mtu ana kigezo chake cha uzuri kama mkia, macho, hips nk
 
Hata vichaa wana wake na waume zao pia


Umerudi lini toka Madagascar..?? Mbona umerudi kimya kimya..?? Hope balozi Mwambopa mumempata...! Njoo umalizie story weye,, kama ulicopy tunga umalizie mwenyewe...... Alaaa
 
Back
Top Bottom