Falsafa ya Dkt. John Pombe Magufuli

Falsafa ya Dkt. John Pombe Magufuli

zebedayo musibha

Senior Member
Joined
Oct 26, 2019
Posts
111
Reaction score
86
Tangia mwaka 1776, Taifa la Marekani limepitia vipindi tofauti tofauti ambavyo ndani yake vilitofautishwa na falsafa mbali mbali za uongozi katika kutekeleza sera ya nchi chini ya maraisi wao.

Lakini falsafa za maraisi mbali mbali katika taifa hili la marekani kuna zilizo kumbana na ukinzani dhidi ya azimio la mfumo fulani(x) ambao ulikuwa unatekelezwa na MaJesuit dhidi ya Mataifa ya Amerika ikiwemo Marekani
Amri ya Wajesuiti ilitimiza kiapo chao tena kwamba watatia sumu, wataua, au watafanya chochote kinachohitajika ili kuwaondoa wale wanaopinga mipango yao.

Kuanzia 1841 hadi 1857, Marais watatu wa Marekani walishambuliwa na Wajesuiti kama ilivyoainishwa katika Bunge la Vienna, Verona, na Chieri. Wawili walifariki na mmoja kutoroka (RAIS HARRISON, TAYLOR, NA BUCHANANI) akiwemo pia Rais Lincoln

Hu ulikuwa ni mpango wa Majesuit kuakikisha kuwa Hawaruhusu chochote kusimama katika njia yao ya utawala kamili wa Amerika, na uharibifu wa Katiba. Pia waliazimia kuimiliki United kwa usiri mkubwa kwa kutumia mawakala wao walio jofanya masikini na waaminifu wa kutoka kila kona ya ulimwengu, na kuwakusanya katika mioyo ya miji ya Washington, New York, Boston, Chicago, Buffalo, Albany, Troy, Cincinnati. Chini ya vivuli vya miji hiyo mikuu, Wamarekani .

Waliwatazama mawakala kama watu maskini na kwa dharau kubwa, kama wanaofaa tu kuchimba mifereji yao, kufagia mitaa yao na kufanya kazi katika jikoni zao. Hi ilikuwa ni moja ya mbinu zilizo tumiwa na hao Majesuit mda si mlefu Majesuit walipenya hadi kwenye idara nyeti za nchi hapo ndio ikawa mwanzo wa kuimiliki United.

Lakini falsafa za kizalendo za hao Marais (Lincoln, HARRISON, TAYLOR NA BUCHANANI) ziliendana ambazo zilijikita zaidi kuijenga United isiyo mpigia magoti mtu yeyote au taifa lolote ulimwenguni na kuifanya kuwa taifa huru lisiro na mfungamano wa Dini yoyote.
Ni falisafa ambazo zilikinzana na matakwa ya Majesuit na kwakuwa walipenya ndani ya serikali na idara nyeti ndio sababu walitekereza adhima yao ya kumfuta yeyote aliye ingilia njia zao na ndio maana hawa Marais waliuwawa.

Kwa mfanano huo wa Taifa la Marekani leo hii tunalitazama Taifa la TANZANIA chini ya Rais JOHN POMBE MAGUFULI
Falsafa yake ya uongozi imejikita zaidi katika uzalendo wa utaifa kwanza kulijenga taifa katika nyanja ya kiuchumi na kuziba mianya ya unyonyaji katika wizi wa rasilimali za taifa.

Kama ilivyo kuwa kwa taifa la Marekani leo hii africa tunafanywa hivyo hivyo ambapo tunashindwa kuwa na maamzi ya aina ipi ya demokrasia tunapaswa tuwenayo, tunashindwa kuwa na maamzi kwenye uchumi, Elimu na Siasa kwani hivyo vyote tumeingiliwa na mataifa ya nje(mabeberu)

Lakini falsafa ya Dkt. MAGUFULI ni kupambana na Diplomasia ya uchumi katika kulijenga Taifa ambapo katika nyanja hii ya uchumi ndipo kuna mizizi ya wanyonyaji ambao mpango wao ni kuliangamiza Taifa kuendelea kuwa masikini hivyo ni vita ambayo ni kari sana ambapo kama watanzania inatupasa kusimama pamoja na Rais wetu pasipo kujali tofauti zetu za kisiasa na kidini tuwe mstari wa mbele katika kumwombea Rais wetu na Taifa letu kwa ujumla (Yanayo endelea huko duniani ni makubwa sana kwa kuwa yanaendelea kwa siri kubwa ila matokeo yake ni kunyongwa kwa uchumi na kutaabika katika umasikini sana sana zawadi ambayo tunaweza pewa ni vita kuuwana sisi kwa sisi)

Watanzania tubadilike tuwaelewe viongozi wetu leo hii mifumo mingi ya nchi inashikiliwa na watu wachache ambao adhima yao ni kuitawala Dunia tuna tengenezewa majanga mbali mbali vita, magonjwa na njaa lengo lao ni nchi ziyumbe kiuchumi na tutumbukie kwenye mikopo ambayo tutaendelea kuwa wategemezi na hatuta weza kujikwamua KIUCHUMI mfano mwaka jana na mwaka huu wametengeneza janga la CORONA lakini wazuia nchi zingine kutengeneza chanjo lakini chaajabu wametengeneza wao chanjo na leo inapigwa promo ili mataifa yanunue au wapewe kama msaada kwa njia ya mkopo kupitia WB na IMF.

Sasa pale tunapo pata Rais ambaye kila njia za hawa watu anapambana kuzikwepa huyo ndie SHUJAA na MZALENDO wa kweli wa Taifa letu. Huyu ndie Raisi aliye weza kuonyesha falsafa ya uongozi wa kizalendo na ujasiri mkubwa katika kulijenga Taifa.


JE DEEP STATE IMEHUSIKA KATIKA KIFO CHA HAYATI DKT JOHN POMBE MAGUFULI?


Makala yangu hapo juu ilimlika kuhusu Falisafa ya aliye kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA HAYATI DKT JOHN POMBE MAGUFULI.
Jinsi gani Falisafa yake ya uongozi ilivyo kuwa mwiba kwa MABEBERU pamoja na baadhi ya vigogo ndani ya nchi.

Je DEEP STATE imehusika?
Nianze kutolea mfano utawala wa D. TRUMP aliye kuwa Raisi wa Marekani, ukisoma katika vitabu vya
- IN DEEP by David Rhode
(THE FBI, THE CIA AND THE TRUST ABOUT AMERICA'S DEEP STATE)
- DONALD TRUMP Vs. THE UNITED STATES INSIDE THE STRUGGLE TO STOP A PRESIDENT. BY Michael s Schmidt
-RAGE BOB WOODWARD
-DISLOYAL by Michael Cohen

Utagundua kuwa ilikuwa razima Rais DONALD TRUMP asiendelee na pia utagundua kuwa mbali na mamlaka ya Rais kwa nchi ya Marekani ipo mamlaka ya siri (DEEP STATE) ambayo ndio ina control Marekani moja ya sababu kadhaa ambavyo vilisababishwa Rais TRUMP ang'olewe ni
-Biashara yake ya siri na urusi (Moscow)
-ubaguzi na mengineyo mengi ambayo yameorodheshwa kwenye hivyo vitabu hapo juu.

Nini na maanisha kwa mfano huu,
Ipo nguvu ya ziada ambayo ni ya siri inayo control baadhi ya nchi Duniani kutokana na mazingira yake na huitaji wake kwa agenda za nchi na watu wake.

Endapo hii nguvu ikiamua kumuondosha Rais madarakani wasipo tumia njia ya uchaguzi basi kuna hatari ya kuuwawa kama ilivyo kuwa kwa baadhi ya maraisi wa Marekani walivyo uwawa kama nilivyo elezea kwenye makala iliyo tangulia.

Nguvu hii hata africa ipo na kipindi nchi nyingi za africa zinapata uhuru zilikabidhiwa kwa makubaliano maalum hivyo upandikizwaji wa hii nguvu yaan DEEP STATE iliendelea kustawi kwa kuhusiha baadhi ya viongozi wa maeneo (nchi) husika kutokana na huitaji wa nchi yenyewe.
Mfano tumeshuhudia uchaguzi wa DRC ulio pita pale kuna nguvu ya ziada ili husika kumuweka Raisi wasasa kuwa madarakani.

Je kwa Tanzania DEEP STATE inahusika? Pengine kifo cha HAYATI DKT JOHN POMBE MAGUFULI

Tukitazama baadhi ya matukio kuna namna ya mfumo wa siri.

1. Tukianzia kwenye uchaguzi 2020
kabla ya uchaguzi kulikuwa na vuguvugu fulani kama vile Rais MAGUFULI lazima ang'oke madarakani na hi vuguvugu ilianzia ndani ya chama chake na baadae nje ya chama.
Swali la kujiuliza je lile kundi ambalo liliitaji kusimamisha mgombea ndani ya chama wachuane na Raisi aliyepo madarakani hiyo nguvu hilo kundi na huyo mtu waliitoa wapi? Na hadi kufikia kuaminisha na watanzania

Lakini baadae huo mpango ulivyo shindikana baada ya Rais MAGUFULI kufanya maamzi magumu kama mwenyekiti wa chama kwa kuwafuta na kuwafungia uwanachama baadhi ya makada.
Tunaona kwenye uchaguzi kuna kete nyingine inachezwa baada ya kada na mwanadiplomasia nguli BERNARD MEMBE kujiunga ACT WAZALENDO hii ilikuwa ni hesabu ya kuwa lolote lingetokea kwenye uchaguzi kutokana na vuguvugu la uchaguzi lilivyo kuwa na pengine hesabu za matokeo ingekuwa kama ilivyo kuwa DRC walipo kabizi madaraka kwa mtu wa tatu badala yule wa upinzani mkuu
Sasa kwa endapo lolote lingetokea kwa ccm kulemewa njia ya CHADEMA ilikuwa wazi lakini wasinge kabidhiwa badala yake wange kabidhi kwa MEMBE (ACT).
Shida hesabu za MEMBE zilialibiwa na chama chenyewe kwa kuungana na CHADEMA na ndio maana CCM alifurahi sana pale walipo ungana.

Ingawaje haikutokea lakini mtambue kuwa ACT ni planned hiki kimekuja kushusha tempa ya upinzani bara na visiwani (Note kifo cha self kuna miujiza ya penetration za ACT ili ku stabalize visiwani)
Hivyo ACT ni sumu na mwiba ambao sasa watu wengi hamta elewa lakini ipo siku mtaelewa.



2. Kufeli kwa plan ya uchaguzi ndipo tunashuhudia kifo kina mkuta MAGUFULI
Kifo ambacho kimeacha maswali mengi sana kwa watanzania.
Lakini kabla ya kifo tulishuhudia taasisi ya kidini tena kubwa ulimwenguni wao wakitoa walaka kwa waumini wao maana yake walikuwa kinyume na maamzi ya serikali kuhusu CORONA.

Pia awali ya yote Rais MAGUFULI alikuwa akikaliliwa akisema tumuuombee mtangulize MUNGU na kama amejitoa kafara kwa watanzania kana kwamba kuna mfumo ambao wazi alikuwa akipambana nao au kwenda nao kinyume na ndio maana bali na katiba alikasimisha madaraka yote ya nchi mikononi mwake hadi kutowaamini baadhi ya watendaji wake wa karibu.

Lakini kinyume cha watangulizi wake alichukua mda mwingi kuendèsha shughuli za kiserikali Chato kuliko Magogoni au chamwino hi hali kama ilileta wasiwasi pengine kulikuwa na siri nyuma ya haya matukio yote.

Mwisho. Pengine Falisafa ya Raisi MAGUFULI kama nilivyo elezea kwenye makala ya mwanzo huwenda ikawa sababu ya kifo chake na kama ni hivyo huwenda tukawa na nguvu ya ziada inayo control Tanzania yaani DEEP STATE
 
Hizo nadharia za kusingizia mabeberu juu kushindwa kwetu ni kutaka kulikimbizia tatizo kwa kuwalaumu wengine.

.Tunapowekeza kwenye miradi isiyozaliza hatupaswi kuwalaumu mabeberu.

.Tunapouwa sekta binafsi

Kusomeshwa namba watu

.Kuuwa demokrasia

. Kutaifisha pesa na Mali za watu

. Kuzuia mzunguko wa pesa mtaani

Hatupaswi kutupia lawama wengine.

Note v8 moja ni sawa na trekta 6 horse power 75 na majembe yake unapojenga uchumi kipi bora v8 au trekta.

Tuendelee kuwalaumu mabeberu juu ya kushindwa kwetu
 
Coca-Cola, Revis Strauss jean,Big G gum,Kentucky fried Chicken, Ford Motor cars,Hollywood na Broadway, Las Vegas,Boeing n.k ni juhudi za mtu mmoja mmoja au kundi sio serikali.Ndio wakaleta mapinduzi ya maendeleo makubwa Marekani.

Magufuli japo ana mambo mengi anajaribu kuyafanya sio juhudi ya watu binafsi. Ile nguvu au uwezo wa binadamu umekabidhiwa mtu mmoja! Which is quite wrong.

Serikali iwe wazi kuwawezesha au kuwapa uhuru wazawa katika kujenga nchi yao.Na huo ndio muarobaini wa maendeleo, wala haitakiwi propaganda uchaguzi ulisha isha.
 
Tangia mwaka 1776, Taifa la Marekani limepitia vipindi tofauti tofauti ambavyo ndani yake vilitofautishwa na falsafa mbali mbali za uongozi katika kutekeleza sera ya nchi chini ya maraisi wao...
Magufuli is a country bumpkin.

Hana falsafa yoyote, anaendesha nchi kwa mabavu.

Case in point.

Hakufanya homework yake kabla ya kuingilia biashara ya korosho.

Kwa mujibu wa ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania ya Septemba 2019, mapato ya bidhaa za kilimo zilizouzwa nje mwaka ulioishia Agosti 2019 yalishuka kwa asilimia 55 ukilinganisha na mwaka ulioutangulia.

Hili ni anguko kubwa sana. Na sehemu kubwa ilichangiwa na Magufuli kuingilia kwa papara biashara ya korosho, zao la kilimo la pili kwa kuingiza fedha za kigeni wakati huo.

Sasa huyu mtu anayeangusha mapato ya mazao ya kilimo kwa asilimia 55 katika mwaka mmoja, kwa papara zake zisizo na mkakati, unaweza kusema ana falsafa ya uchumi?

Huyu anaelewa hata mambo ya msingi tu ya uchumi?
 
We ndio "Musiba" wa Tanzanite Newspaper, a.k.a "Msifiaji aliyekosa uwakilishi Dodoma?"
 
We ndio "Musiba" wa Tanzanite Newspaper, a.k.a "Msifiaji aliyekosa uwakilishi Dodoma?"
Mbona sijakunyishea kidole wewe na kukuita ROGART KATAPILA walio imba Mchinga sound na Badi Bakude?

Maana yangu ni hii sio ukiona jina lina milikiwa na mtu mmja hapana
Yule ni Musiba Cypirian, mimi ni Musibha Zebedayo huoni hata spelling zinatofautiana.
Please tune your mind.
 
Mbona sijakunyishea kidole wewe na kukuita ROGART KATAPILA walio imba Mchinga sound na Badi Bakude?

Maana yangu ni hii sio ukiona jina lina milikiwa na mtu mmja hapana
Yule ni Musiba Cypirian, mimi ni Musibha Zebedayo huoni hata spelling zinatofautiana.
Please tune your mind.
Sawa Boss!
 
Tangia mwaka 1776, Taifa la Marekani limepitia vipindi tofauti tofauti ambavyo ndani yake vilitofautishwa na falsafa mbali mbali za uongozi katika kutekeleza sera ya nchi chini ya maraisi wao...

Mayagi Mulaga aka Mwanaharakati huru katika ubora wako.
 
Humu ndani Kuna viumbe wanajifanya kuwafahamu Majesuit Sana. Wanakuja na vi theory vyao vya uongo kutaka kutimiza azima yao. Halafu ukiulizwa Majesuit (members of the Society of Jesus) ni akina nani na Je, iyo Tanzania ya Magufuli hawapo? Na Je, unajuaje Kama Spiritual director wa Magu si Padre Mjesuit Kama ilivyokuwa kwa spiritual director wa Kenyata na aliyekuwa director wa Mgabe?

Na uyo Spiritual director wa Mugabe ndo yule aliyesimamia makubaliano ya wanajeshi waliompindua Mugabe na Upande wa Mugabe, tendo ambalo lilisaidia mabadiliko ya kiuongozi wa Zimbabwe bila kumwaga damu? Huoni kazi nzuri za Hawa vijana wa Yesu waliojitoa maisha kujenga mfumo unaotetea haki iletayo usawa?

#MAGIS
 
Humu ndani Kuna viumbe wanajifanya kuwafahamu Majesuit Sana. Wanakuja na vi theory vyao vya uongo kutaka kutimiza azima yao. Halafu ukiulizwa Majesuit (members of the Society of Jesus) ni akina nani na Je, iyo Tanzania ya Magufuli hawapo? ...
#MAGIS
Kama ni wazuri embu rejea kwenye visa vifuatavyo
Establishment of federal reserve bank
Sinking of titanic
First and second world wars
Secret of ant-communism
Death of Patrick lumumba, Tom mboya, Nkwame Nkuruma

Hivyo ni kwa uchache tu,niishie hapo kwa kuwa argument yako sio msingi wa mada husika!
Rejea msingi wa mada tajwa.
 
Umesahau namba za simu we Pimbi , Zanzimana mwenyewe hata neno falsafa hajui maana yake , sembuse awe na falsafa yake?
 
Jiwestone Falsafa yake ni kuhakikisha watz wanaishi kishetani thus maendeleo ya watu sio kipaumbele chake. Yupo bize kupambana na watu kuliko kupambana na maendeleo.

Furaha yake ni kuona watu wote wawe fukara dhoofu Hali ikiwezekana wafe kabisa kwa njaa, umasikini, corona, wasiojulikana, nk. Kuhakikisha watu wanahangaishwa usiku na mchana Ili apate furaha ya ndani kupitia kuumiza watu. Laiti angepewa haki ya kugawa pumzi duniani hakuna ambae angebakia hai.
 
Kama mtu ajawahi hata soma somo la uchumi au Development Study, knows nothing about economic atakuwa vipi na falsafa ya uchumi sasa. Uchumi unataka reasoning capacity sayansi inataka claiming capacity na sio reasoning. Hapa ni kuchanga viungo vya pilau.

Tuhesabu tu ni loss tujipange tu kwa ajae. Kama biashara zinapata hasara tuamini wakati mwingine nchi inapata hasara pia.
 
Mbona sijakunyishea kidole wewe na kukuita ROGART KATAPILA walio imba Mchinga sound na Badi Bakude?

Maana yangu ni hii sio ukiona jina lina milikiwa na mtu mmja hapana
Yule ni Musiba Cypirian, mimi ni Musibha Zebedayo huoni hata spelling zinatofautiana.
Please tune your mind.

Majina ufanana tabia.Kwa uzi huu reasoning yako haipo mbali na ya mulaga Majura musiba
 
Humu ndani Kuna viumbe wanajifanya kuwafahamu Majesuit Sana. Wanakuja na vi theory vyao vya uongo kutaka kutimiza azima yao. Halafu ukiulizwa Majesuit (members of the Society of Jesus) ni akina nani na Je, iyo Tanzania ya Magufuli hawapo?...
Unawajua Majesuit wwe sio vilaza Kama unavyofikiria Labda Majesuit wa TISS.
 
Maguful hana falsafa yeyote anayotumia kuongoza hii nchi.
 
Back
Top Bottom