Harakati za CDM sana sana ni kuwabeba vijeba vya CDM ili waonekane wanafanya kaziakati ni pamoja na maandamano na migomo inayoshabikiwa sana a wapambe wa CDM.
Sioni jinsi unvyoweza kuendeleza nchi kwa kugoma.
Hata hivyo kwa info yako wewe unawezakuwa canon fodder wa kuwawezesha watu kupata ulaji tu bila kujijua.
Hey! Give me a break. Hivi nchi inaendelezwa kwa kuiba na kupora mali ya umma na kunenepesha ma-account uswis? Inaendelezwa kwa kwenda kusaini mikataba ya uchimbaji madini nnje ya nchi tena guest? Kwa kunyang'anya wananchi ardhi iliyoandaliwa miundombinu ya umwajiliaji na kuwapa mabepari huku wenyenchi wakifa kwa njaa? Ilhali tunayo mapori kibao yenye rutjba na hayajaendelezwa. Ama kweli imeandikwa kuwa watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa
Pamoja na yote umenivunja mbavu kweli, Nakubali ipigwe stick.Mheshimimiwa Freddy Sanga,
Kwanza kabisa hongera na asante sana kwa uzi huu, ambao ni wa kipekee kabisa hapa JF.
Uzi huu umefanikiwa ktk mambo mengi lakini kubwa zaidi ni kuwa umetenga usiku na mchana ktk siasa za Tanzania. Kwa maana ya msingi wa falsafa, sera, dira, maono na uwezo ktk dhana nzima ya kushika dola na kuleta maendeleo.
Bila kuongeza chumvi, kupitia uzi huu imethihirika kuwa CCM ni wepesi sana, ni wapumbavu, ni watu wasio na maono wala uwezo wa kuiongoza Tanzania yetu; na ndio maana kama vile Mwenyekiti wao Jakaya Kikwete alivyosema Oktoba 2010 "...Nataka nijulikane kuwa niliitoa Tanzania hapa nikaifikisha hapa.....". Maana yake NOWHERE!
Hivyo basi kwa kuwa:-
- uzi wako huu una umri wa zaidi ya mwaka mmoja na nusu mpaka sasa;
- na kwa vile wana CCM hapa JF tena kwa wingi wao wameshindwa hata kudiriki kufikiria kutaja falsafa yao ni ipi,
- wao wako katika kuchumia tumbo zaidi ya kufikrisha bongo zao
Hitimisho:Uzi uwe sticky, tena kwa maandishi ya rangi ya dhahabu (ikiwezekana MODS).
Ili uzi huu uwe shule na mafundisho kwa kila mwenye kuitembelea JF kwa nia au lengo la kupanua elimu na ufahamu.
unapaswa kuwa umekufa au haujawahi kuishi Tanzania ndio uwe hauifahamu Falsa ya CCM, maana hata ukilitaja jina hili kwa kirefu utapata majibu.
Naomba kuuliza swali moja tu, hivi hii imesomwa na wale wasomi waliopo kwenye pay roll yenu kama akina baregu na Kitilla? hivi hata maana ya falsa nayo mfundishwe?
Niliondoka CCM kwa sababu ya huu uchwara.Una maana hawana kabisa, duh:embarassed2:
Ujenzi wa ujamaa si lelemama bali ni mapambano, mapambano ya kudumu dhidi ya ubepari na unyonyaji, dhidi ya wapinga maendeleo na wababaishaji wa kisiasa, dhidi ya wahujumu uchumi, majambazi, wezi, wazururaji na wazembe. Msimamo sahihi wa mapambano unaotokana na nadharia sahihi ya ujamaa ungelituepusha na maamuzi na vitendo ambavyo vimerahisisha kuoteshwa kwa
mizizi ya ubepari, kinyume cha msimao wa mapambano dhidi ya ubepari. Leo ubepari, una vishawishi vingi zaidi nchini kuliko ulivyokuwa kabla ya Azimio la Arusha kwa sababu pamoja na kwamba sasa tuna sekta kubwa ya umma lakini kutokana na udhaifu wa kutopambana nao, ubepari umefaulu kujipanua na
kujipenyeza hata ndai ya sekta yenyewe ya Umma. Na ndiyo maana ubepari sasa unathubutu kujitokeza hadharani kuukashifu ujamaa, kubabaisha baadhi ya viongozi na kututaka tubadilishe siasa yetu.
Hii inanichanganya saidia wana JF.
Sijui kama wanaelewa?ccm haina tena falsafa, labda nyimbo za mh komba, jogoo limewika dodoma
tulifanya kosa kutomchagua mrema mwaka 1995Kolimba alishasema zamani sana kuwa hawa jamaa wameshapoteza dira