Falcao kadanganya umri?

Falcao kadanganya umri?

Mourinho

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2012
Posts
4,619
Reaction score
2,328
Kumbe sio wachezaji wa kiafrika tu hasa wa West Africa wanaodanganya umri, kina Okocha, Essien, Taribo West, Martins et al.

Moja kati ya washambuliaji wakali zaidi katika ulimwengu wa soccer bwana Ramadel Falcao inasemekana kadanganya umri.

Hii ni kutokana na documents za shule ya msingi aliyosoma huko kwao Colombia zinazoonesha kuwa jamaa alizaliwa 10/02/1984 hivyo kumfanya kuwa na umri wa miaka 29 na sio umri wake ambao ndio official wa miaka 27.

Hii inaweza kuelezea kwanini jamaa kaamua kwenda Monaco kuvuta pesa ndefu na kukacha club kubwa kama Madrid au Chelsea. Moyoni mwake anajijua kuwa tayari maji ya jioni so kamuua kuvuta tu mpunga before its too late!

Kwa habari zaidi chungulia hapa

http://www.dailymail.co.uk/sport/fo...-suggest-Monacos-53million-striker-29-27.html
 
Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1374607221.361652.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1374607221.361652.jpg
    41.6 KB · Views: 116
  • ImageUploadedByJamiiForums1374607240.061132.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1374607240.061132.jpg
    52.8 KB · Views: 106
  • ImageUploadedByJamiiForums1374607258.527810.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1374607258.527810.jpg
    37.4 KB · Views: 98
Ha ha nmeipenda hiyo Mkuu ya Ramadeo Falcao-kumbe mifupa imeshakomaa kama tayari kama zege

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Ndio maana kakimbilia zake Ufaransa kwenye ligi nyanya
 
Wakati report zikidai Falcao kadanganya umri, huko England mshambuliaji mahiri wa Newcastle United, Pappis Cisse ambaye amekataa kuvaa jezi ya club yake yenye nembo ya Wonga, kampuni ya kukopesha pesa, alipigwa picha akiwa casino inayoitwa Aspers mwaka jana mwezi November

Cisse alikataa kuvaa jezi zenye nembo ya hiyo kampuni kwa sababu za kiimani/dini yake uislam, akidai kuwa zinaenda kinyume na mafundisho ya dini yake na akajitoa kwenye safari ya maandalizi ya ligi, ambayo team yake inaendelea nayo huko Portugal akidai apewe jezi isiyokua na nembo ya hiyo kampuni.

Sasa hili la kwenda casino limemvulia heshima yake kama mwanasoka na kama muislam safi, kwa sababu huko kwenye macasino wote tunajua huwa kunakua na biashara gani, kama kamali, kubet, ma-stripers( wacheza uchi) n.k

Baadhi ya mashabiki wa Newcastle na wachambuzi wanadai Cisse alikua anajaribu kulazimishwa kuuzwa kwa club tajiri ambazo zimeonesha kumuhitaji hasa za Russia, na akatumia kigezo cha dini kama kisingizio ili aforce kuuzwa.

Kwa sababu wapo wachezaji waislam kwenye team ambao hawakua na tatizo na kuvaa hizo jezi, kina Ben Arfa, Sissoko na Tiote ila yeye akataka kudanganya watu kuwa ni muislam safi, sasa yatamtokea puani!
 
Huko South na Latin America ndio zao kama Africa tu...........
 
Haaaaah jmbe la ukweli limeamua kula mpungaaa kabla hajawa pub
 
Huko South na Latin America ndio zao kama Africa tu...........

Kwa hiyo unataka kusema wale kina Messi, Aguero, Hulk, Ramires, Cavani, Suarez n.k ni wakubwa zaidi ya tunachoambiwa?
 
Nilijiuliza sana huyu jamaa kwa nini anaenda Monaco,kumbe yale yale ya kina Gyan,jua linazama! pesa mbele.
 
Usikute na Cavani naye ana 30's huko lol! Hahahahahaaaa, uzee nyoko!
 
Wakati report zikidai Falcao kadanganya umri, huko England mshambuliaji mahiri wa Newcastle United, Pappis Cisse ambaye amekataa kuvaa jezi ya club yake yenye nembo ya Wonga, kampuni ya kukopesha pesa, alipigwa picha akiwa casino inayoitwa Aspers mwaka jana mwezi November

Cisse alikataa kuvaa jezi zenye nembo ya hiyo kampuni kwa sababu za kiimani/dini yake uislam, akidai kuwa zinaenda kinyume na mafundisho ya dini yake na akajitoa kwenye safari ya maandalizi ya ligi, ambayo team yake inaendelea nayo huko Portugal akidai apewe jezi isiyokua na nembo ya hiyo kampuni.

Sasa hili la kwenda casino limemvulia heshima yake kama mwanasoka na kama muislam safi, kwa sababu huko kwenye macasino wote tunajua huwa kunakua na biashara gani, kama kamali, kubet, ma-stripers( wacheza uchi) n.k

Baadhi ya mashabiki wa Newcastle na wachambuzi wanadai Cisse alikua anajaribu kulazimishwa kuuzwa kwa club tajiri ambazo zimeonesha kumuhitaji hasa za Russia, na akatumia kigezo cha dini kama kisingizio ili aforce kuuzwa.

Kwa sababu wapo wachezaji waislam kwenye team ambao hawakua na tatizo na kuvaa hizo jezi, kina Ben Arfa, Sissoko na Tiote ila yeye akataka kudanganya watu kuwa ni muislam safi, sasa yatamtokea puani!

Baada ya bwana Cisse kuumbuka na picha za Casino, sasa kakubaliana kuvaa jezi yenye nembo ya wadhamini (Wonga) ambayo mwanzoni alikataa katakata kuvaa akisisitiza kuwa kufanya hivyo ni kinyume na imani yake kidini.

Wanasema, "ukiwa muongo, usiwe msahaulifu"
 
Back
Top Bottom