Kwa Sasa ata Feitoto akienda CAS mpaka shauri lake lipangiwe ma jaji, lianze kusikilizwa, wahusika waletewe ujumbe Ili Kwa maandishi, uwakilishi, au wahusika wafike kwenye usikilizwaji wa shauri,
Haitapungua miezi mitatu.
Najua hii ya kuchangiashana mitandaoni ni kutafuta huruma tu kwakua aliye nyuma ya hili ni mtu mwenye fedha ndugu Yusufu Bakresa.
Baada ya muda upo uwezekano mkubwa wa kumpatia iyo fedha.
Baada ya kusikilizwa ilo shauri Kuna muda wa kusubiri hukumu nao haupungui wiki mbili mpaka mwezi kwakua alisikilizwi swala la Feisal pekeyake, uwa yanafika mpaka mashauri kumi tofauti Kwa wakati mmoja.
Mpaka swala lake liishe itakua mwakani na itategemea uharaka wa kulipeleka CAS na kama ameshinda au ameshindwa.
Kama angekwenda Yanga upo uwezekano mkubwa swala lake lingeisha ndani ya wiki Moja.
Kupanga ni kuchagua, kiburi Cha Fei kinaletwa na Yusufu Bakresa.