Fainali za Kagame: Kaseja aliiponza Simba

Makoye Matale

JF-Expert Member
May 2, 2011
6,491
2,104
Katika gazeti la 'Jibu la Maisha' Toleo namba 146, Jumapili 17-23, Julai 2011 katika ukurasa wake wa mwisho limechapisha habari yenye kichwa tajwa hapo juu.

Imeelezwa kwamba kufungwa kwa Simba bao 1-0 na Yanga kulitokana na kipa wao namba 1 Juma Kaseja kujiinua dhidi ya Mwenyezi Mungu kwa kujiita 'Alfa na Omega' jina ambalo imedaiwa kuwa linatumiwa na Mungu Mwenyezi pekee.

Baadhi ya watu walioongea na gazeti hilo wamedai kuwa, kile alichokifanya Kaseja kilikuwa sawa na kufuru ambayo wote walioifanya walishindwa vibaya na kuanguka katika anguko baya. Umetolewa mfano kuwa kipindi Tyson akiwa katika kiwango cha juu katika masumbwi wakati wa pambano lake na Evander Holyfield aliingia ulingoni kwa mbwembwe za kujitumainia huku akichangizwa na neno 'takbir' na mwenzake Evander aliingia ulingoni akiwa na andiko la neno la Mungu 'Nayaweza mambo yote katika yeye anitaiye nguvu'. Katika pambano hilo Tyson alipigwa vibaya mbele ya macho ya mamilioni ya watu kutoka pande mbalimbali duniani. Imedaiwa kuwa Evander hakujipa utukufu binafsi wala kujiinua nafsi yake.

Gazeti hilo limeendelea kuandika kuwa, Kaseja katika mechi ya fainali kati ya Simba na Yanga alivaa fulana kwa ndani iliyokuwa na maneno 'Alfa na Omega' na kufunikwa na jezi yake. Awali katika pambano mojawapo Kaseja baada ya timu yake kushinda alifunua jezi na kuonesha fulana ilyokuwa imeandikwa 'There is only one Kaseja' akimaanisha kuwa kuna Kaseja mmoja tu.

Gazeti hilo limehitimisha kuwa, Simba waliokuwa wakijisifu sana kabla ya pambano tena majigambo yakiongozwa na Kaseja ilifungwa bao 1-0 na Yanga kaitka kipindi cha pili cha nyongeza baada ya timu hizo kutoka suluhu ndani ya dakika 90. Matokeo haya yalimfanya Kaseja kuangua kilio kama mtoto mdogo.

Swali hapa ni:
Je, ni kweli majigambo ya Kaseja yalimfanya Mnyama aache manyoya na kuonekana kwamba ameliwa?
 
Weka picha ya hiyo fulana yenye hayo maandishi, sio kutuletea maneno tu.
 
Daima mungu anasema ajikwezae atashushwa na ajishushae atakwezwa, kaseja alikweza na ndo mana alishushwa, na asipokuwa makini unaweza kuwa mkosi moja kwa moja, mungu hataniwa na yeyote
 
sio kweli kabisa...tulibaniwa penalt yetu moja ya wazi kabisa
St. Ivuga hamkunyimwa penati, Kiiza alipiga bao refa kaminya, ingekuwa ninyi ndo mmenyimwa lile bao waamuzi wasingetoka uwanjani. Hata hivyo kateni rufaa mtashinda tu mezani maana uwanjani hamwezi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom