Faida za vyakula vya nyuzi nyuzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Faida za vyakula vya nyuzi nyuzi

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Nov 9, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 9, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  ​CHAMOS, H.J
  KULA vyakula mchanganyiko ni moja kati ya kanuni muhimu za lishe bora. Vyakula vya nyuzinyuzi ni mchanganyiko wa vyakula mbalimbali vya wanga ambavyo haviyeyushi kama vyakula vingine. Nyuzinyuzi hizi huwepo kwenye gamba la nje la seli. (cell walls).

  Nyuzinyuzi hizi hupatikana katika vyakula ambavyo havijapitia kiwandani au utayarishaji kama kukoboa, kusaga (n.k.) ambavyo ni
  nafaka , mizizi, kundekunde, matunda, mbegu za mafuta na mboga za majani.

  Kuna aina mbalimbali za nyuzinyuzi ambazo zimegawanyika katika makundi mawili. Zinazoyeyuka na zisizoyeyuka. Vyakaula vya mimea vinaweza kuwa na aina zote mbili au mojawapo. Kwa mfano kundekunde na matunda zina nyuzinyuzi zinazoyeyuka. Nafaka zingine huwa na nyuzinyuzi zisizoyeyuka. Pia kuna wanga ambao hauyeyushwi unapofika kwenye utumbo mpana. Hii huwa inaifanya kazi kama za nyuzinyuzi.


  Mwili hauwezi kuyeyesha nyuzinyuzi au kufyonza kama ambavyo hufanya kwa vyakula vingine. Nyuzinyuzi hubakia katika utumbo na hata baadaye hata kama makapi. Zile zinazoyeyuka hufyonzwa na mwili .


  Nyuzinyuzi ni irutubisho muhimu kwa sababu zifuatazo:


  Nyuzinyuzi hupunguza kasi ya uyeyushaji wa chakula kuanzia mdomoni hadi tumboni. Vyakula ambavyo vihavijakobolewa au kupitia viwandani huwa hizi nyuzinyuzi ambazo hubakia mdomoni au tumboni kwa muda mrefu. Hivyo humfanya mtu asisikienjaa haraka. Hii husababishwa na ugumu wa kuzitafuna na kuzisagasaga nozi za vya vyakula hivi
  (cell walls) tofauti na

  vyakula vilivyokobolewa na kupitia viwandani huwa rahisi kutafunwa kusagwa na hata kuyeyushwa.

  Nyuzinyuzi husaidia chakula kufyonzwa taratibu. Nyuzinyuzi zikiloana hubeba maji na kusababisha chakula kuwa kizito tumboni. Hii husababisha ufyonzwaji wa virutubisho kuwa wataratibu. Ni vizuri kwa mwili kufyonza virutubisho pole pole na kwa ufanisi kuliko haraka haraka kama chakula kinavyokuja.

  Nyuzinyuzi husaidia chakula kuwa kingi. Hii huwasaidia sana watu wanene na wenye uzito mkubwa kupunguza kula.Kwani huon achakula kingi hali ni nyuzinyuzitu. Lakini hii ni hasara kwa watoto wadogo kwani watakula chakula kingi cha kuongeza nguvu tu badala ya kula vyakula mchanganyiko. Kwani hushiba haraka.


  Nyuzinyuzi husaidia kinyesi kuwa laini na kingi. Hii ni faida kuu mojawapo ya nyuzinyuzi. Kutokana na tabia ya nyuzinyuzi kufyonza maji, hutoka na kinyesi kupitia utumbo mpana. Kinyesi kikiwa laini na kingi hutoka kwa wepesi na kuzuia
  "constipation" matatizo ya kupata choo. Hii pia husaidia utumbo kubaki na afya wakati wote na hata kuzuia magonjwa
  mbalimbali ya utumbo kama sarakani, vidonda n.k.


  Nyuzinyuzi husaidia hulowesha wadudu wowote wanaolowana na kuwatoa nje na kinyesi, hii huzidi kuuacha utumbo msafi na kuukinga na magonjwa.

  Vile vile nyuzi nyuzi husaidia kupunguza kiasi kolesteroni katika damu ambayo husababisha magonjwa ya moyo.

  Kwa upande mwingine, nyuzinyuzi huzuia ufyonzwaji wa madini ya chuma na mengineyo. Kwa hivyo tunashauri
  wajawazito na watoto wadogo ambao wanaweza wakapata "anemia" upungufu wa damu wanashauriwa wasile sana.

  Na kwa vyakula vya watoto, nyuzinyuzi zipunguzwe, kwani watashiba haraka na kuelekea wasile vyakula vingine vyenye virutubisho mbalimbali.


  Vyanzo muhimu vya nyuzinyuzi ni kama karoti, matunda aina zote, nkabeji, mboga za majani maharage na jamii yake, mahindi mabichi, unga wa mahindi usiokobolewa sana, viazi n.k.

  Hasa hasa utapata 'fibre" kwenye vyakula asilia.
   
 2. i

  igwe sr. Member

  #2
  Nov 9, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  umeeleweka mkubwa,asante kwa kutujuza hzo faida,mungu akuzudishie moyo huo2 wa kutupa dondoo zaidi.
   
 3. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #3
  Nov 9, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Shukurani sana; tusaidii na madhara ya kuvikosa kabisa vyakula hivi!
   
Loading...