Mchele wa brown ni nafaka iliyo na faida kubwa kwa afya ya binadamu. Huwa na aina nyingi zaidi za vitamini kuliko zinazopatikana kwenye mchele mweupe.
Pia, kiasi cha nyuzilishe, madini ya zinc, magnesium na phosphorus kinachopatikana kwenye aina hii ya mchele ni kikubwa zaidi kuliko kile kilichopo kwenye mchele mweupe.
Huwa na faida hizi;
Hufaa kwa watu wenye ugonjwa wa kisukari
Hupunguza hatari ya kuugua magonjwa ya moyo
Huwa na viondoa sumu vingi vinavyofaa kwa kulinda seli hai za mwili hivyo kusaidia katika kupambana na magonjwa sugu, mfano saratani
Husaidia kutunza uzito sahihi wa mwili
Pamoja na kuwa na changamoto inayotajwa na watu wengi ya “Kukosa radha”, Mchele huu hufaa kwa watu wa makundi yote pasipo kujali umri na hali ya afya.